Vijana watajitokeza kwa wingi sana kumpigia kura Rais Samia uchaguzi Ujao, Ni uchaguzi utakaoweka Historia ya vijana kujitokeza kwa wingi kupiga kura

Nipe connection namimi nipost nilipwe mkuu, mtaani hakueleweki.
Kalibu tulime,, Mimi silipwi na mtu zaidi ya kulima tu, wakulima Tunamshukuru Rais Samia kwa namna alivyotusaidia wakulima suala la pembejeo baada ya kutoa mabillioni ya Ruzuku pamoja na upatikanaji wa soko la uhakika kwa mazao yetu ya mahindi
 
Mama amedhamiria kuwasaidia Vijana πŸ‘‡
 

Attachments

  • Screenshot_20221005-104854.png
    210.4 KB · Views: 3
  • Screenshot_20220805-093409.png
    337.4 KB · Views: 4
  • Screenshot_20220726-180947.png
    230.3 KB · Views: 2
UPUMBAVU mtupu! Umelipwa sh ngapi hapo Lumumba? Vijana wa Hovyo sana nyie ni aibu kwa taifa
 
Labda wale wanaofaidika na buku 7 za Lumumba! Ni vijana wangapi wamemaliza vyuo wako bila!!
Kila Leo wateuliwa ninwalewale hadi wastaafu ambao wanakula pensheni!!
Naona uneagiza na Shaka na kakuandikia haya! Kalaghabaho!!
 
Labda wale wanaofaidika na buku 7 za Lumumba! Ni vijana wangapi wamemaliza vyuo wako bila!!
Kila Leo wateuliwa ninwalewale hadi wastaafu ambao wanakula pensheni!!
Naona uneagiza na Shaka na kakuandikia haya! Kalaghabaho!!
Ajira mh Rais anaendelea kutoa kwa kadri Hali ya uchumi inavyoruhusu Kama ambavyo alitoa ajira za ualimu Afya kilimo na TRA, japo hawezi kumaliza kuajiri vijana wote lakini juhudi zake zinaonekana ndio sababu vijana tuna Imani na matumaini makubwa Sana na mh Rais
 
Atamaliza kwa sababu anajua wasio na ajira ni 12% so atamaliza kwa kuwaajiri ajira rasmi,kwa kuwawekea mazingira ya kujiajiri hasa kwenye kilimo Cha umwagiliahi,block farming,ufugaji na biashara..πŸ‘‡
 

Attachments

  • Screenshot_20221013-151351.png
    228.2 KB · Views: 2
  • Screenshot_20220805-093409.png
    337.4 KB · Views: 3
  • IMG-20221018-WA0001.jpg
    58.3 KB · Views: 3
Naona unahangaika sana, muda bado sana.
Subiri angalau 2024, ndio uanze kusema yote unayoyasema. Wiki mbili tu watu husahau kila kitu.
Kwahiyo, sasahivi we tulia tu endelea kuusoma upepo na kusoma attitudes za vijana, kufikia 2025 utakuwa umewajua vijana vizuri.
 
Vijana wameshatambua kwenda na mama Samia uchaguzi ujao na hawana sababu ya kusubiri upepo mwingine maana aliye upande wao wameshamtambua kuwa Ni mama Samia
 
Sawa..
Na sisi kwenye sekta ya Mifugo atukumbuke hizo ajira aisee..
πŸ˜€πŸ˜€
 
[QUOTE="Lucas mwashambw
Ndugu zangu kwa miaka mingi na kwa kipindi kirefu na kwa chaguzi nyingi vijana wa kitanzania wamekuwa wakijitokeza kwa kiasi kidogo Sana kupiga kura na kushiriki katika uchaguzi, Japo wakati mwingine wamekuwa wahudhuriaji Wazuri wa mikutano ya vyama vya siasa lakini wamekuwa wa mwisho linapokuja suala la kujitokeza siku ya kupiga kura.

Hii Ni kutokana na kukatishwa Tamaa na baadhi ya watu au viongozi waliokuwa wanawaamini Mara wanapokuwa wamepata nafasi za uongozi, vijana wamekuwa wakiona Ni Kama wanatumiwa tu pasipo kupata faida yoyote, vijana wamekuwa wanaona ni Kama hawapewi kipaombele hasa suala la ajira na mikopo, vijana wamekuwa wakiona ni Kama hata wakijaribu nafasi za uongozi hawachaguliwi kutokana na kuwa na uwezo mdogo wa kifedha ambazo baadhi ya wajumbe Ni Kama wamekuwa wakiangalia kina Cha mfuko wa pesa kumpa mtu Kura

Jambo hili limekuwa likiwakatisha Tamaa vijana, kuwavunja moyo,kuwa fanya waichukie siasa, kuwachukia baadhi ya wanasiasa wanaokuwa wakitoa lugha zinazo chukuliwa Kama dharau kwa vijana hasa wanapoona mtoaji wa kauli katika maisha yake yote hajawahi kujiajiri Wala kuwa machinga Wala kuwa muuza karanga Wala kushika jembe Wala kuendesha bodaboda Wala kulima matikiti maji Wala kuwa na biashara ya aina yoyote Ile zaidi ya kuhudumiwa kwa Kodi za Watanzania wavuja jasho ambao hawana uhakika wa kupata hata Milo mitatu kwa siku Wala kuelewa Ni vipi watalipa Kodi ya nyumba.

Lakini Tangia Rais Samia aapishwe na kuwa Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ni Kama vijana wamechanua kimatumaini, wamepata Imani ya kuwa Sasa ndoto zao zitaweza kutimia, Sasa vijana wanajionaa wanaweza kugombea na kuwa viongozi hata Kama hawana fedha ilimradi tu wawe na sifa na vigezo vya kiuongozi na kukubalika na kuaminika na wapiga kura, Sasa vijana Wana Ari mpya na nguvu mpya ya kuijenga nchi yao, Sasa vijana na kila kijana anaona kuwa inawezekana kuinuka kiuchumi bila tatizo lolote,

Sasa vijana wanaona ukiwa hata na kiasi kidogo Cha mtaji unaweza ukafungua biashara na ikakua na kustawi na kuchangia katika ujenzi wa nchi yao, Sasa vijana wanaona kuwa keki ya Taifa inawafikia walipo, Sasa vijana wanaona kuwa serikali Ni yao, inawatumikia wao na inawapa kipaombele.

Wanaona serikali yao inavyopambana kuweka mazingira wezeshi kwao, wanaona namna serikali yao inavyotaka kuhakikisha kuwa halmashauri zinatoa mikopo kwao pale wanapokuwa wamefuata taratibu na kukidhi vigezo, wanaona namna ambavyo hakuna ubaguzi katika kupata ajira au fursa ya aina yoyote Ile ya kiuchumi, wanaona namna serikali yao inavyojitahidi kutengeneza fursa za ajira kila Siku kupitia miradi mbalimbali Inayochipua kila siku

Rais Samia kawasha Taa ya matumaini katika mioyo ya Vijana wa kitanzania, Kaonyesha njia ya kufika katika mafanikio, kaonyesha upendo kwa vijana wake ambao hupenda kuwaita WANANGU kwa namna anavyo wapenda na kuwajari vijana wa kitanzania,

Hii imepelekea vijana kujiandaa kwa Hamu kubwa Sana kuja kumpigia kura nyingi Sana za ndio Rais Samia ili aendelee kuwatumikia vijana, ili aendelee kuwapa neema na fursa za kiuchumi maana vijana wameona kuwa Rais Samia Ni kiongozi aliyeonesha dhamira ya dhati katika kuwabeba vijana na kuwakuza na kuwastawisha kiuchumi, Rais Samia ameonyesha Dhamira yake ya kuona fursa yoyote inayopatikana inakwenda kuwagusa kwanza vijana na kuwanufaisha

Rais Samia anahitaji kuona vijana wanajitegemea kiuchumi na kuwa na uwezo wa kujihudumia na kuwasaidia wazee wao wanaohitaji msaada wa kusaidiwa na kulelewa, Rais Samia Ni kipenzi Cha vijana ambaye amepelekea uchaguzi ujao kuwa mwepesi Sana kwake na kwa CCM kwa kuwa vijana wameamua kumpigia kura na kumuunga mkono

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
[/QUOTE]sio bure umetumwa wewe vijana ambao mnawanyima mikopo elimu ya juu ajira mnawanyima wakijajir kuwa machinga mnawafurusha kama nchi sio yao kwa kwel vijana hawawez kumchagua Huyo Samoa wako
 
Sawa..
Na sisi kwenye sekta ya Mifugo atukumbuke hizo ajira aisee..
πŸ˜€πŸ˜€
Hakuna secta itakayobaki bila kuguswa na kuwapa fursa za ajira vijana, Ndio sababu vijana tuna Imani kubwa Sana na mh Rais wetu mpendwa mama samia
 
sio bure umetumwa wewe vijana ambao mnawanyima mikopo elimu ya juu ajira mnawanyima wakijajir kuwa machinga mnawafurusha kama nchi sio yao kwa kwel vijana hawawez kumchagua Huyo Samoa wako
[/QUOTE]
Kipindi hiki Ni kipindi ambacho vijana wengi Sanaa wanapata mikopo ya Elimu ya juu bila shida yoyote Ile. Pia Hakuna machinga aliyefukuzwa Bali waliwekwa katika mpangilio mzuri na maeneo mazuri yanayofikika vizuri na wateja na yaliyo na Miundombinu yote tofauti na awali walipokuwa Wana hatarisha usalama Wao kwa kupanga vitu Hadi Barabarani, Zoezi hili lilikwenda vizuri Sana kwa kuwa machinga walishirikishwa vizuri na katika Hatua zote kupitia viongozi wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…