Vijana wekezeni, fainali umri mkubwa!

WACHA WALE MAISHA WANGALI VIJANA UNAJUAJE KAMA WATAFIKA UZEENI?
 
Hapo Ndio kipengere!
 
Pana Mzee walikuwa wanamcheka mwaka 1993 akiwa bize kununua mashamba dar wanamwambia we umechelewa kweli yaani unalima dar,tumekimbia mashamba kijijini, Mara Dar napo unalima kweli,mwaka 2010 yeye ndio akawa anawacheka wenzake,ukimgusa tu 20 kwa 20 anakwambia bila milion 40 usinisumbue,akawa anaporomosha majumba ya Sasa ya msauzi ma fremu Leo ni mtu mwenye pesa sana waliomcheka mkulima masikini Leo wamestaafu wamechoka mbaya ye ndie boss wao wanamlilia shida
 
Uzi fikirishi sana neno wekeza nimelishika
 
Upo sahihi haswa
 
Ila tofauti ya life expectancy ya waafrika ni ndogo sana ukilinganisha na wenzetu kufika 90 ni kawaida sana na wao hawadhulumiwi pensions zao na wana raha mpaka wanazeeka kuliko waafrika
Nasikai dp world wanakuja kuongeza life expentancy.
 
Aiseee umenikumbusha mbali sana kuna tajiri mmoja kariakoo anaitwa Mushi, aiseee jamaa ana maeneo Dar kama alijua. Yaani kuanzia Mbezi beach, Masaki , Upanga na pale Kariakoo. Halafu huyu mzee yupo simple tu na landcruiser yake ya zamani. Na kuna yule alikuwa mmiliki wa Tommy milk. Jamaa ana ranch Iringa na maeneo ya kutosha hapa mjini. Ana Mijengo kariakoo,Mbagala na kwingineko aisee acha tu. Hawa wazee wamenifundisha mengi sana. Yaani wanakopesheka any time wakitaka. Wana real estate profile ya kutisha. Halafu nae huyu wa Tommy milk yupo simple tu. Kwa kumalizia hawa jamaa hawajawahi kufanya kazi serikalini. Mzee Lymo wa Tommy milk amenifundiaha mengi sana. Ishu ya ardhi ni muhimu sana pale ambapo unahitaji kukopa hela bank. Kuna matajiri ambao bank zinawabembeleza kuchukua mkopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…