Vijana wekezeni, fainali umri mkubwa!

Vijana wekezeni, fainali umri mkubwa!

Tuache tule bata, hakujenga baba wakati mfuko wa cement sent 20 nihangaike mie sasa hivi mfuko unakaribia 20 elfu.
Nijenge nyumba ya nini, mimi niwe na nyumba na kobe awe na nini.
Pondamali kufa kwaja, nani alizikwa na mali zake🤣

Komenti hii ni kwa hisani ya BALIMI
Subiri yakukute utalia peke Yako,tutakusikia ila hatutakusaidia!
 
Habari wanaJf,Niende moja kwa moja kwenye mada hapo juu.Mimi kwa Sasa Nina umri wa miaka Hamsini na tatu(53)Niliajiriwa kwenye kampuni moja wakati huo nikiwa na miaka Ishirini na sita(26).Tukiwa vijana na rafiki zangu tulifurahia sana Maisha na kampuni yenyewe ilikuwa inalipa vizuri sana .

Wenye ufahamu mzuri walijiwekeza kwenye ardhi, biashara,mifugo, nyumba,nk.Sasa umri umesonga nayo magonjwa nyemelezi yamekuwa tatizo!Ukimpigia simu mwenzako,utasikia Naumwa kisukari mara huyu,Kansa,mara,huyu viungo vimechemka,mara pressure nk.

Shida inakuja pale hukuwekeza gharama za matibabu ziko juu hata marafiki huwaoni na hata ukiwaona nao wanachangamoto zao Tulikuwa na msemo wa kijinga wa''Uza Nyumba Jenga Heshima Bar .Nisiwachoshe, Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Well said 👏. Kama mtu hajafika huko anaweza asielewe unaongea nini hapa lkn huo ndio ukweli. Kuna umri ukifika utatamani urudishe miaka nyuma ili uweke mambo sawa lkn inakuwa too late. Kudos kwa wazee wazamani, unaweza ukamuona mzee yupo yupo tu, kawaida tu, kumbe bank ana akiba ya kutosha
 
Pole mzee, kama ulifanya kazi na hukuwekeza pole zaidi. Mtaa mgumu saivi ajira hakuna ila bado tunalisongesha huku tukiwa na matarajio makubwa bado
 
Kama mtaani ndio kugumu kiasi hiki!! Hiyo ya kuwekeza naitoa wapi bro? Au tuache kuzihudumia familia na madogo wasisome...
 
Back
Top Bottom