Vijana wekezeni, fainali umri mkubwa!

Vijana wekezeni, fainali umri mkubwa!

Ardhi ni mali,ardhi ni uhai!
Ardhi pekee ndio njia rahisi ya kukata umasikini kwenye familia au ukoo.
Pana wachaga walikuwa masikini kabisa vibarua wa kukata nyasi za ng'ombe na kusaidia kuchoma chips mjini miaka 30 iliyopita wakilipwa Hicho Hicho kidogo waliwahi maeneo Leo wameuza wamepiga pesa mingi sana wamejenga majumba ya kisasa,malodge,ma frem wanakula uzee mateso ya ujanani.
We endelea kusema tu wachaga wezi wakinga wachawi .
We umeshindwa Nini kuiba au kuwa mchawi uwe tajiri.
Ardhi haimtupi mtu.
Wakinga walikuwa masikini sana wazazi wao waliwapandia miti watoto wao Leo wakavuna wakapata si chini ya milion 100 na zaidi mtaji tosha wa biashara.
Ukiwa masikini wekeza kwenye ardhi.
 
Habari wanaJF,

Niende moja kwa moja kwenye mada hapo juu. Mimi kwa Sasa nina umri wa miaka Hamsini na tatu(53). Niliajiriwa kwenye kampuni moja wakati huo nikiwa na miaka Ishirini na sita (26). Tukiwa vijana na rafiki zangu tulifurahia sana maisha na kampuni yenyewe ilikuwa inalipa vizuri sana.

Wenye ufahamu mzuri walijiwekeza kwenye ardhi, biashara, mifugo, nyumba, nk. Sasa umri umesonga nayo magonjwa nyemelezi yamekuwa tatizo. Ukimpigia simu mwenzako, utasikia naumwa kisukari mara huyu, kansa, mara, huyu viungo vimechemka, mara pressure nk.

Shida inakuja pale hukuwekeza gharama za matibabu ziko juu hata marafiki huwaoni na hata ukiwaona nao wanachangamoto zao. Tulikuwa na msemo wa kijinga wa ''Uza Nyumba Jenga Heshima Bar. Nisiwachoshe, Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Asante Mzee wangu.
"Save to Invest"

#YNWA
 
Mnnnh.

Mstari upi kwenye maandiko unasema
Masikini hawawezi urithi ufalme wa Mungu?
Screenshot_20230814-141618.png
Screenshot_20230814-141452.png
 
Sio wenye nguvu ya pesa.

Ingekuwa hivyo hii chini mistari isingekuwa na maana

"Yesu aliposikia haya, akamwambia, “Bado unahitaji kufa nya jambo moja. Nenda ukauze vitu vyote ulivyo navyo, uwagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.” 23 Aliposikia hayo alisikitika, kwa maana alikuwa tajiri sana"

"Yesu alipoona yule kiongozi amesikitika, akasema, “Jinsi gani ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu! 25 Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”

Kwahiyo zinazozungumziwa hapo sio nguvu za kimwili wala kifedha.
 
Tunavyofanya mambo ya ovyo watakao ufikia huo uzee wa fainali ni wachache mno ,wengi tutatoka hatua ya makundi tu.
 
Ardhi pekee ndio njia rahisi ya kukata umasikini kwenye familia au ukoo.
Pana wachaga walikuwa masikini kabisa vibarua wa kukata nyasi za ng'ombe na kusaidia kuchoma chips mjini miaka 30 iliyopita wakilipwa Hicho Hicho kidogo waliwahi maeneo Leo wameuza wamepiga pesa mingi sana wamejenga majumba ya kisasa,malodge,ma frem wanakula uzee mateso ya ujanani.
We endelea kusema tu wachaga wezi wakinga wachawi .
We umeshindwa Nini kuiba au kuwa mchawi uwe tajiri.
Ardhi haimtupi mtu.
Wakinga walikuwa masikini sana wazazi wao waliwapandia miti watoto wao Leo wakavuna wakapata si chini ya milion 100 na zaidi mtaji tosha wa biashara.
Ukiwa masikini wekeza kwenye ardhi.
Nipo Dodoma hapa kuna jamaa katoka Moshi kama msaidizi wa duka la jamaa wa kwao Moshi .ujira akipewa ananunua ardhi kwa Wagogo Mara pap,Magufuli Katia timu.Viwanja watu wanataka!Jamaa Sasa ni wakala wa bia,sigara,soda nk.Tumebaki tunamsifia tuu na macho tunayo na akili tunazo ,zililala.
 
Pana watu wanatembea kwenye mkondo wa baraka
 
Back
Top Bottom