Vijana wengi wa KATAA NDOA hawajielewi

Vijana wengi wa KATAA NDOA hawajielewi

Kwamba malezi yanakua na tofauti gani ? Mbona tunaona vibaka wa mali za uma na banya Road kibao wametokea familia za baba na mama ?

Na unauhakika gani watoto wako mda wote wataishi na wewe na mke wako kwa pamoja mpaka watoke mikononi mwenu?
Unaweza nambia kuwa mtoto aliyelelewa na wazazi wote2 analingana na aliyelelewa na na mzazi 1? Kama huna familia tulia hujui kitu wewe

Mfano wa panya rodi hayo ni matokeo ya ugomvi ndani ya familia na mtoto mwenyew wengine ni watukutu tu Kuna mifano Mingi ya watu maarufu hapa Tz na kwingineko Watoto wao wametumbukia kwenye madawa ya kulevya nk

Mfano mmoja wapo fatilia maisha ya mtoto wa Obama yule binti mkubwa anaitwa Sasha Obama kama sijakosea.
 
Sina cha kukujibu kwasababu umeonyesha kunijua sana , unalofikiri ndio jibu sahihi .
 
Ndoa zinazopigwa ni hizi za kitapeli hasa kwa wanaume wapambanaji ,ndoa za cheti na kutiana saini ,then badae inatumika kukumaliza.
Hayo ni yenu huko mnaooa kisomi. Mimi hata ikitokea tumegawana na tuna Watoto hainipi shida. Ukiona eneo unaloishi Kuna issue za hivo kwann utumie majina Yako kuamdikisha miradi Yako? Huna Watoto? Huna mama mzazi? Tumieni hata akiri za shemeji Zenu basi kama Zenu zimeshafikia kikomo walio waolea dada Zenu vile wanavyoishi nao hata Leo.
 
Cha kusitikisha zaidi ukija kuangalia sababu zao hazina mashiko Wala umhimu wowote wengi wameegemea kwenye Mali.
mali zenyewe wazitolee wapi kama upeo wao mdogo tu... zaidi watakupa mifano ya watu wengine ila sio wao hapo alipo anaandika kataa ndoa akiwa keshatoka kuwekewa mjegeje karudi kwenye chumba chake cha 20k hakina hata umeme.
 
Enyi watu mlioko kwenye ndoa,ishini kulingana na viapo vyenu,msivikiuke waziwazi na kufanya ambao hawajaingia kwenye ndoa,wakakata tamaa.
Una poo a ah kuolewa halafu bado unasaliti ndoa,unadhani unaleta picha gani kwa ambaye hajaoa au kuolewa?
Una pooa au kuolewa halafu unakula njama ya kumuondoa mwenza wako ili umiliki mali mwenyewe,inaleta picha gani kwa wale ambao hawako ndoani?
Unapoolewa na unaifanya ndoa yako inakua na watoto mseto,unadhani wanaojua siri hiyo wanaichukuliaje ndoa?
Tuishi kimaadili ili wale ambao hawamo kwenye ndoa,wahamasike kuingia.
Ahsantee Kwa ujumbe mzuri.

Lakini ukaenukijua kuwa hapa ni duniani hayo hayana budi kutokea hata kipindi Cha Musa Hadi yesu na mtume wazinzi walikuwepo tu
 
Hayo ni yenu huko mnaooa kisomi. Mimi hata ikitokea tumegawana na tuna Watoto hainipi shida. Ukiona eneo unaloishi Kuna issue za hivo kwann utumie majina Yako kuamdikisha miradi Yako? Huna Watoto? Huna mama mzazi? Tumieni hata akiri za shemeji Zenu basi kama Zenu zimeshafikia kikomo walio waolea dada Zenu vile wanavyoishi nao hata Leo.
Tatzo lako haujibu hoja kama hoja unaenda kwenye kushambulia binafsi kama unamjua mtu , apo unapoteza sifa za kujadiliana kwa sababu unakua kihisia zaidi badala ya akili 🙏
 
Ahsantee Kwa ujumbe mzuri.

Lakini ukaenukijua kuwa hapa ni duniani hayo hayana budi kutokea hata kipindi Cha Musa Hadi yesu na mtume wazinzi walikuwepo tu
Kama inajulikana kua wanandoa wataweza kua na watoto mseto,watakua wanafanya mapenzi nje ya ndoa,wanaweza kuuana ili kumiliki mali wenyewe(yaani mmoja wao) na mengine mengi,kuna haja ya viapo?
Viapo vingetolewa,nadhani wale wa sogea tukae waliwaza sana,hawakutaka kumdanganya Mungu wala hadhara inayokusanyikaga wakati wa ufungaji ndoa,unaoambatanaga na viapo.
 
Kuoa ama kutoa kuoa ni maamuzi tu kama vile maamuzi mengine sio sheria wala sio kanuni ya kila mtu kwenye maisha.

Wapo watoto wenye madili mazuri walilelewa na mzazi mmoja na wapo wenye maadili mazuri waliolelewa na wazazi wote wawili, vivyo hivyo kwa ubaya .

Ndoa zililindwa na mifumo dume kwa sasa hakuna mifumo hiyo tena na vijana wakaona hakuna sababu ya kuoa tena kama kinachopatikana kwenye ndoa kinaweza patikana kirahisi bila hata ndoa.

Sababu za kusema wapinga ndoa wakwepa majukumu na ni upinde nisababu za kiwaki, sisizo na kichwa wala miguu kwa sababu kuna upinde kibao wapo na ndoa na wakwepa majukumu kibao kwenye ndoa, wanaachia mke majukumu yote ya familia yeye anabaki kama baba jina tu.
 
Back
Top Bottom