jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Mimi ni mkristo na nina ndoa ya kikristo lakini kuna jambo moja nimeliona linanifikirisha saana kuhusu ndoa zetu hizi
Kuna dogo namfahamu ana miaka 27 lakini miaka miwili nyuma alifunga ndoa ya kikristo. Miezi kama sita nyuma ndoa yake imevunjika yaan ndoa ilidumu kwa mwaka mmoja na nusu tu. Saivi kila mtu ana maisha yake na dogo hana mpango wa kurudiana na huyo mwanamke na uzuri au ubaya ni kwamba katika ndoa hii haikupata mtoto
Kinacho nifikirisha na tunalojadili ni kua kwa mujibu wa dini ya kikristo huwezi kufunga ndoa nyingine na mtu mwingine kama uliefunga nae ndoa yupo hai au mpk afe ndo ufunge ndoa nyingine,
Na ukianza kuishi na mtu mwingine ambae hujafunga nae ndoa mnaonekana ni wazinzi na huwezi kupata huduma za kanisa maana unaishi nje ya utaratibu wa kidini
Je hawa vijana walioachana wanaweza kuishi bila kua na wenza wengine maisha yao yote kwa ndoa iliyodumu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu pekee.
Nadhani ipo haja ya dini zetu hizi kurudi kulitazama upya
Hizi dini zilipaswa ziendane na tamaduni zetu za asili hapa ndipo tulipokosea