Ni kweli kabisa ukizoea hela tangu utoto wala hazikupi shida zikiwa nyingi kwako pia
Nakumbuka Baba yetu tulipokuwa wadogo akiwa anataka kusafiri ataniita na kusema haya zipange hizi hela
Unakuwa umezizoea wala ile hali ya kuiba unakuwa huna kabisa wala hujui hiyo tabia
Sasa na sisi tumekuwa tumefuata zile tabia za wazazi walizotufundisha
Watoto wangu wana account zao za Bank niliwafungulia wakiwa wadogo sana
Vijana kama baba yako hakukuweka pazuri basi wewe waweke wanao pazuri au wewe mwenyewe jipambanie
Kwenye ngozi hii ina tatizo kubwa sana
Angalia mpaka majuu weusi ndio wamejaa jela kwa sababu hawajafundishwa
Leo mtu anakimbia majukumu ya mwanae aliezaa nje kisa hawezi kumuhudumia
Wengine wakataa ndoa
Yote haya ni kukosa nidhamu ya maisha
Kwa baba zenu mmekaa miaka zaidi ya 20 mnajaza Vyoo tu leo eti unaogoapa kuoa
Mwenye nidhamu ya hela utakuta hata mtoto wake wa miaka 10 ameisha muandalia nyumba yake na kumwambia mke hii ni nyumba ya flani
Kweli haya mawazo mtu aliemkimbia mtoto ataweza?
Pambana kijana huwezi kuwakuta hao wamejaa jela au wamekaa vijiweni siku nzima