Vijana wengi wenye Digrii waliojiajiri na bado wanawaza ajira wanapata faida chini ya milioni 3, hawajaonja utamu wa biashara wa kuwasahaulisha ajira

Vijana wengi wenye Digrii waliojiajiri na bado wanawaza ajira wanapata faida chini ya milioni 3, hawajaonja utamu wa biashara wa kuwasahaulisha ajira

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Wengi huwa wanafanya biashara huku wakiwaza ajira kwasababu biashara wanazofanga haziwalipi hasa ukizingatia wengi uwanja wa biashara hawana uzoefu nao na wana bagua biashara za kufanya.

Nataka niseme kwamba kwa kijana mwenye degree ili aachane na ndoto za ajira ni lazima awe kaonja utamu wa biashara in terms of profit.

Biashara ukija kuanza kulamba faida hata 150K kila siku ni kazi sana kuanza kuzikumbuka ajira.

Graduate anawaza ndoto kwamba kwenye ajira ipo siku atafikia mishahara ya milioni 4, na hiyo ni ndoto maana wapo wanaopata hio mishahara ila ni wachache. Ili aache kuwaza ajira inabidi azime ndoto za huo mshahara...
 
Ni sahihi kulingana na uwezo wa elimu yako, graduate wengi tena wazoefu wa miaka 15 wanalipwa below 2m, ni kichaa tu anaweza pata faida 3m akawaza ajira
 
graduate wengi tunakwama kwa mazingira kama manne hivi:-
  1. wengi wetu hatujawahi kutegemea kujiajiri hivyo hatujiamini katika biashara.
  2. uaminifu
  3. hatuko tayari kufanya kazi na kujituma
  4. hatuwezi kuungana na kukusanya mtaji wa pamoja
 
kuna muda tuacheni mada za kis****ge sasa. Utoto huu na kutokufikiria
 
Wengi huwa wanafanya biashara huku wakiwaza ajira kwasababu biashara wanazofanga haziwalipi hasa ukizingatia wengi uwanja wa biashara hawana uzoefu nao na wana bagua biashara za kufanya...
Biashara ni kwa aliezaliwa nayo, wavivu wote chaka lao ni kuajiriwa serilalini maana humo ukishaingia hata kma huzalishi ama umetia hasara mshahara wako uko palepale tu[emoji3]
 
Back
Top Bottom