Vijana wengi wenye Digrii waliojiajiri na bado wanawaza ajira wanapata faida chini ya milioni 3, hawajaonja utamu wa biashara wa kuwasahaulisha ajira

Vijana wengi wenye Digrii waliojiajiri na bado wanawaza ajira wanapata faida chini ya milioni 3, hawajaonja utamu wa biashara wa kuwasahaulisha ajira

Biashara bwana ni kama ilivyo michezo mingine mpira,golf,riadha,nk ili ufanikiwe huko katika hiyo michezo kwanza lazima tu uipende.

Kuna watu wanapenda jambo flani na bila kuja level ya elimu yake analivaa jambo analolipenda mzima mzima, Napenda spirit ya wanamuziki,mtu ana degree yake lakini humwambiii kitu na mziki yupo radhi akashinde studio kwa laizer na degree yake ipo mfukoni.

Biashara ipo hivyo,ili ufanikiwe uanze ingiza hayo mapesa ishu sio capital maana unaweza pewa capital hata ya Millions of money na bado ukashindwa ingiza hiyo 150k per day.

Biashara kwanza ipende yani bila kujali una degree una Masters yako wewe ni wa biashara tu,hata atokee nani akwambie njoo ntakulipa kiasi fulani akili yako iseme hapana mimi ni Biashara tu.

Ukishakua na mahaba ya biashara ndipo hapo utakapoanza tengeneza hizo 150k per day na zaidi na zaidi kwa mtaji wa kawaida kabisa kabisa.

Ukiipenda biashara hautaongozwa na matamanio ya pesa huwa ukiwa katika biashara pesa inakufata yenyewe automaticaly kulingana na mahaba unayoyaonyesha kwenye hiyo biashara uliyoichagua.

ukianza kusema naingia kwenye biashara ili nipate pesa (huzipati ng'o) wengi tulio kwenye biashara kwanza ni watu tunaotaka uhuru binafsi,akili zina mambo mengi kuliko mtu anavyoweza nitazamaa.

sehemu pekee ya mimi kufungua mipaka ya mawazo yangu ni kwenye biashara tu,hata kama nitaanza na biashara ya mtaji wa 50,000 naamini kadri siku zinavyoenda kupitia faida nitakayopata kwenye hiyo biashara nitafanya kitu kingine kikubwa zaidi.

tofauti na Ajira hata kama utaongezwa mshahara majukumu yako yatabadilika kidogo tu lakini kila siku utakua unafanya kitu kile kile kama mwanafunzi, Kuajriwa ni utumwa na kuishi chini ya maelekezo.Home n Mzazi una familia lakini kazni una behave kama Jitoto,akiingia Boss eti na wewe unatetemeka unaogopa..maisha gani hayo!

ipende biashara anza biashara yoyote bila kujali halafu utaona namna hela inavyokutembelea,mwanzo ni mgumu lakni hakuna mwanzo mrahisi kama ukiamua kuwa mfanyabiashara unaefanya unachokipenda.

ishi maisha ya level yako,maisha unayoyamudu kisha anza biashara...Kuna watu wanaishi nyumba kodi above 100k halafu anawaza leo aanze biashara (huyu mtu hata iweje ataonaga biashara hailipi na ngumu tuu)

Switch aina ya maisha uliyonayo yapeleke kibiashara hata life style lako,ishi kama mfanya biashara Calculate Profit and Loss ili uweze furahia biashara.

nina watu kibao nawajua wanaaanza biashara na zina kufa,na pesa wanazo mtu anaanza biashara ana gari anaenda nalo kazini na kurudi nalo... (unafikiri huyu mtu atatoboa)

gari linahitaji mafuta daily biashara ndio mpya bado hujui itakulipa au haitokulipa na itakulipaje,Sikatai kuna watu wanashtuka kuingia katika biashara wana magari lakini si kwa ubaya unapoingia ktk biashara,Gari (paki home) tumia miguu hiyo.

Tuache kuingia kwenye biashara na akili ya ku gain hapo hapo,tujipe muda Hakunaga biashara yyte inayoweza kukupa faida ya kuonekana ndani ya mwaka mpk miaka miwili ya mwanzo,kila pesa kwa kipindi hicho inatakiwa kurudi kwenye biashara unayoifanya.

Atleast utaanza kula faida ya biashara yako tena kidogo sana kuanzia mwaka wa 3 ila kama una NIA kweli ya kutamani ufike siku uingize 1m and above per day Faida ya biashara utayoianzisha leo utaanza iona baada ya miaka 10 mbele. Hapa kati kati hela zote utatoa yako ya kula,mahitaji muhimu nyingine yote inarudi kwenye biashara.

no gari,no kiwanja,no nyumba,no usafiri ila baada ya miaka kuanzia 8 kwenda mbele kugusa 500k per day ni kugusa tu TAP hii hapa.

Bishara INALIPA japo inahitaji Uji katae na uvumilie mabonde na milima.
 
Back
Top Bottom