Vijana wenzangu wa Zanzibar tuwe makini, wengi wanatepeliwa kwa kuambiwa wanatafutiwa safari ya nje ya Nchi

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Huku Zanzibar kumeibuka tabia ya Watu ‘kupigwa’ sana pesa kwa kisingizio cha kutafutiwa safari za kwenda nje ya Nchi.

Wengi ninaowafahamu waliokutwa na changamoto hiyo wameingizwa mjini kwa kuambiwa wanatafutiwa safari ya kwenda Nchini Canada, wanashawishiwa kuwa watakuwa na maisha mazuri, wanatoa fedha ya kutengenezewa 'mchongo', baadaye mambo jiiiiii kimya

Kuna mtu anaitwa Edi Cool sijui jina lake kamili lakini wenyewe wanamuita Balozi wa Vijana anahusishwa sana na huo wizi.

Kibaya zaidi wanaofanyiwa utapeli huo na kuumizwa hawasemi baada ya kuaibika, wanaona haya. Vijana wenzangu tuache tamaa, maisha mazuri unaweza kuyapata hata ukiwa hapa nyumbani, lakini ni vizuri kufuata njia halali kama unataka kwenda nje ya Nchi, hizi mambo ya njia za panya matokeo yake huwa sio mazuri sana.

Pia soma ~ Kuajiriwa Nje ya Nchi: Njia ya Mafanikio au Mwisho wa Ndoto za Ndani?
 
Oya vipi kaka ajira za vikosi unguja bado au?
 
Haya mambo yapo sana Nairobi Kenya.

Na kwa vile watanzania bado ni wajinga, Hii ni fursa ya kuwaokota mazuzu.

Kijana anamiliki Smartphone anashindwa hata ku Google " Ways to go to Canada, USA au Ulaya"

Anasubiri Agent aje amwelezee. Lazima atapeliwe.

Kwa teknolojia ilipofika sasa, ukitapeliwa fahamu wewe ni mjinga wa mwisho.
 
Back
Top Bottom