Vijana wetu 10 waliokuwa kwenye mafunzo ya JWTZ wamepoteza maisha

Vijana wetu 10 waliokuwa kwenye mafunzo ya JWTZ wamepoteza maisha

Eti pushup wanapiga kwenye godoro.
Hebu imba ule wa kuwananga police.
Ila wote ni wanajeshi ingawa wanatumikia majeshi tofauti

Ile chenja naikubali sana.. ila Jwtz usiwafananishe na police mkuu.. lile bakabaka lione kama lilivyo.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ile chenja naikubali sana.. ila Jwtz usiwafananishe na police mkuu.. lile bakabaka lione kama lilivyo.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Kutoka sitoki mpaka nimalize depot X2
Kazi ya jeshi ni ngumu kama sio polisi
Push up kwenye godoro, huku kwenye Kokoto.
Nalela kumanya, tatantalala X 2.
But all in all police nawaheshimu sana, wengi ni watu makini kuliko wanajeshi
 
Jana CDF alisema wakati wa mazoezi walianza kuishiwa nguvu na wakazidi kuishiwa tena mpaka wakapelekwa kwenye hospital Yao ya kambi na wakati wanawapeleka hospital kubwa wengine wakafia njiani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajeshi 10 wa Tanzania wapoteza maisha wakati wakifanya mazoezi

Feb 03, 2020 14:09 UTC

[https://media]

Jeshi la Ulinzi la Tanzania limetangaza kuwa askari 10 wa jeshi hilo wamepoteza maisha wakati wakifanya mazoezi.

Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya nchi hiyo (CDF), Jenerali Venance Mabeyo ambapo ameongeza kuwa sampuli za wanajeshi hao waliopoteza maisha katika mazoezi ya kijeshi zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi. Mabeyo ameyasema hayo leo katika ikulu ya Dar es Salaam baada ya Rais John Pombe Magufuli kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hapo Januari 31, 2020. Kwa mujibu wa Mabeyo, wanajeshi hao walikuwa kwenye mazoezi ya kawaida ya kutembea. Ameendelea kubainisha kuwa baada ya saa mbili hali zao kuanza kubadilika wakiwa eneo la Msata, walipelekwa hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

[https://media]Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya nchi hiyo (CDF), Jenerali Venance Mabeyo ameendelea kufafanua kuwa baada ya kulazwa hospitalini hapo, baadhi yao walifariki dunia na wengine hali zao ziliimarika na kwamba hadi sasa kuna majeruhi watano. Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais Magufuli alitoa pole kutokana na vifo vya watu 20 katika kongamano la mhubiri wa Kikristo, Boniface Mwamposa vilivyotokea mjini Moshi, vifo vya watu 21 mkoani Lindi baada ya nyumba zao kusombwa na maji na vifo vya wanajeshi hao 10. "Tunahisi walikula chakula chenye sumu, labda wakati wanatembea walinunua vyakula barabarani vikawadhuru. Mazoezi yalikuwa ya kawaida tu. Tumepeleka sampuli za waliofariki kwa Mkemia Mkuu ili kubaini chanzo hasa cha vifo," amesema Mabeyo akizungumzia vifo hivyo vilivyotokea Januari 30, 2020.





4bv61177c7680a1lafv_800C450.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni sana Wafiwa ni bahati mbaya Mungu awapokee mashujaa wetu wamekufa huku wakitekeleza majukumu
 
Inawezekana huko kwenye route match walikula matunda pori yenye sumu!
Au wana mazoea ya kununua vyakula eneo fulani na pengine kuna wauzaji wenye visasi nao waliamua kulipa kisasi kwa kuwalengeshea vyakula vyenye sumu maeneo hayo na baada ya kuwauzia hao wenye visasi wakasepa pasipo kuwauzia raia wengine ndiyo maana hakujaripotiwa vifo vya raia eneo hilo. Au kuna mmoja wao aliyechoka na kuhenyeka huko kambini aliamua kufanya hujuma kwa wenzake na kuwawekea sumu kwenye mess tins zao au gudulia la uji waliokunywa kabla ya kuanza route match.
 
panga kali 2

cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
 
Hivi wanaposemaga chakula chenye sumu hiyo sumu ni ya Aina gani inawekagwa! Ya panya au
Maana nijuavyo mbongo alivyokuwa mgumu yeye ni kula chakula chochote tu

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka intake moja walikimbilia shamba ili kukwepa usaili wa police
Zamani ilikuwa unakwenda JKT ili uajiriwe na Taasisi yoyote ila ukimaliza six week tu hutaki kazi nyingine zaidi ya JESHI
Umenikumbusha mbali sana..sasa ilikuwa ikipigwa hii chenja mida ya mkesha mtu ushavurugwa na mapenzi ya nyoka anaeimbisha anapiga kukatia hapa eh polisi tanzaniaaa..watu wanamind sana kwanini ututabirie tutaenda polisi? Watu walikuwa wanapenda useme bakabaka..[emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom