Mrengwa wa kulia
JF-Expert Member
- Mar 21, 2022
- 1,091
- 3,695
Uvamizi huo umefanywa na vikosi maalum vya Israel kwenye "kituo cha kutengeneza makombora cha Hezbollah" nchini Syria.
Serikali ya Israel haijasema lolote kuhusu operesheni hiyo ambayo kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Marekani, ilifanyika mwanzoni mwa wiki.
Vyombo vya habari vya serikali ya Syria vinasema watu 18 waliuawa siku ya Jumatatu katika uvamizi huo karibu na mji wa Masyaf nchini Syria - karibu maili 25 (kilomita 40) kaskazini mwa mpaka wa Lebanon - na wenginekadhaa walijeruhiwa.
Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, vikosi maalum vya Israel vilishuka kutoka kwa helikopta, kuweka vilipuzi ndani ya kituo kilichojengwa na Iran na kuondoka na stakabadhi zenye taarifa nyeti.
Maafisa wa Marekani na wengine walionukuliwa kwenye gazeti hilo wanachora taswira ya operesheni ya kijasiri, iliyoundwa kuharibu kituo cha kijeshi cha chinichini.
Mashambulizi ya anga yalitumika kupunguza ulinzi wa Syria na kuzuia uimarishaji kufikia eneo hilo.
Kwingineko, ripoti ya tovuti ya habari ya Axios - ikinukuu vyanzo vitatu vinavyosemekana kufahamu operesheni hiyo - inasema kitengo maalum cha Shaldag cha Jeshi la Wanahewa la Israel kilifanya uvamizi huo.
Axios pia inaripoti kuwa Israel iliiarifu Marekani kabla ya operesheni hiyo kupangwa na kufanyika, na haikukabiliwa na upinzani wowote kutoka Ikulu ya Marekani.
BBC bado haijaweza kuthibitisha ripoti hizi kwa njia uhuru.
Serikali ya Israel haijatoa maoni yoyote, lakini uvamizi huo unaonekana kuwa umeundwa ili kuzuia Iran kusambaza makombora ya usahihi kwa Hezbollah, mshirika wake wa Lebanon na wakala.
Israel ilishambulia kituo hicho miaka sita iliyopita na imetekeleza makumi ya mashambulizi ya anga dhidi ya Syria tangu vita vya Gaza kuanza karibu mwaka mmoja uliopita.
Lakini, kuweka wanajeshi wa Israel ndani ya Syria ni jambo lisilo la kawaida.
Hii itakuwa moja ya operesheni ya kisasa zaidi ya aina yake katika miaka.
Source.
NY. Times
BBc