KERO Vilio vya Wamiliki wa Vituo vya Afya Binafsi Wilaya ya Tarime Mjini - Mara

KERO Vilio vya Wamiliki wa Vituo vya Afya Binafsi Wilaya ya Tarime Mjini - Mara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari,hongereni Kwan kazi nzuri ya kufichua maovu,Mimi ni mdau wa Vituo afya wilaya tarime

Napenda kuziomba mamlaka za juu zifuatilie kwa makini mwenendo wa usimamizi wa vituo binafsi vya afya katika Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara.

Katika kipindi cha takribani miaka miwili , zaidi ya vituo 11 vya afya binafsi vimefungwa katika nyakati tofauti kupitia hatua zinazochukuliwa na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Halmashauri. Hali hii imekuwa na athari kwa wananchi wanaotegemea huduma hizo, wafanyakazi wanaopata ajira kupitia vituo hivyo, pamoja na wawekezaji waliofuata taratibu za usajili na uendeshaji.

Kinachozua maswali kwa wadau wengi ni kwamba wakati hatua kali zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya vituo binafsi, bado wananchi wanaendelea kulalamikia changamoto za ubora wa huduma katika Hospitali ya Wilaya. Endapo malalamiko hayo ni ya kweli, basi ni muhimu usimamizi na ukaguzi ufanyike kwa viwango sawa katika vituo vya umma na binafsi, ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora bila upendeleo.

Hatupingi utekelezaji wa sheria wala ukaguzi wa vituo vya afya. Tunachoomba ni uwazi, haki, usawa, na matumizi ya viwango vinavyofanana kwa kila mtoa huduma. Tunaziomba Wizara ya Afya, TAMISEMI,PHAB na mamlaka nyingine husika kulifanyia uchunguzi suala hili na kuchukua hatua stahiki pale itakapobainika kuwa kuna mapungufu katika usimamizi.

Lengo letu ni kuona mfumo wa afya wa Wilaya ya Tarime ukiimarika kwa manufaa ya wananchi wote sio tu mtu akiamka akijiskia kufunga kituo Fulani anafunga bila kujali ajira za watu wengine kumbuka sekta binafsi ni muhimu katika ukuaji wa uchumi nchini.Asante
 
Back
Top Bottom