Vineno vidogo vya Kiingereza vinavyosumbua baadhi ya wazungumzaji

Vineno vidogo vya Kiingereza vinavyosumbua baadhi ya wazungumzaji

Steal, still, steel usiombe ukakutana na hayo maneno ktk ripoti (report) kama umesimama utaanguka
 
kwenye vijiwe vya football, liko neno ambalo hata watu linawasumbua. Defence and defend.Mfano: Timu ya Costa Rica inaji 'defence' zaidi.
Jitu lingine atasikia commentator anasema ''ten minutes to go'' ye anakuambia ''ten minutes ago'' akimaanisha zimebaki dk 10 gemu liishe
 
means standard of professional or group of professional
 
Namshukuru sana mzee wangu,nikiwa darasa la kwanza aliniambia penda kusoma magazeti ya kiingereza,tv angalia habari za kiingereza.leo hii pamoja na kuanza na kumalizia kayumba naburuza sana,na mpaka leo bado naendelea kusoma na kufanya mazoezi.namshukuru sana babaangu
 
Kiswahili msaada kati ya Mda/muda, Asubui/asubuhi, taarifa ya habari/taaarifa/habari, mwisho wa siku/hatimaye,...........
 
Kuna watu Tanzania hii hata lugha yao ya Taifa hawajuwi wapi waweke R na wapi waweke L, wewe unaona ajabu hiyo lugha ya kigeni?

Mkuu hujakosea hilo nalo janga maana kwenye h na a, gh na g mfano (hapendi anaandika apendi, magharibi anandika magaribi, mangaribi) akipatia spelling matamshi tabu.
 
Kila lugha ina maneno fulani yanayosumbua wanaojifunza hiyo lugha. Nimegundua katika Kiingereza yapo haya maneno yanayotumiwa vibaya na baadhi ya watu kama ifuatavyo:their, there, they are: Maneno haya mawili yanawachanganya sana baadhi ya watu.Nimeshakutana na matumizi yafuatayo ya maneno hayo kama:1.The guests have come. Show them there rooms 2.Where are the cats? I see, they are their.3. conflict: Baadhi huandika comflict wanapoitumia kwenye sentensi. Ugonjwa wa hili neno lenye herufi n pia upo kwenye neno convert ambayo huandikwa comvert. Hata hapa JF, kuna mdau kwenye jukwaa fulani ametangazia ufundi wake wa kubadili frdge kuwa incubator, ameandika: I comvert fridge into incubator Chanzo cha tatizo: Nionavyo,matatizo ya matumizi ya haya maneno yanatokana na matamshi yake.Suluhisho:1. Tutumie muda kuyapambanua hayo maneno kwa kuyakariri vizuri 2. Kila tunapoyatumia kwenye maandishi tuhariri maandishi hayo kuhakikisha tumeyatumia vizuri.Nina uhakika yapo mengine kadhaa ambayo nimeyasahau. Mdau mmoja kwenye jukwaa hili kazungumzia loose na lose.

Hivi huwa ni bangeee, ushamba au ni nini?
Wabongo kwa presentation si mchezo waambie watekeleze, mweee!
 
Mkuu hujakosea hilo nalo janga maana kwenye h na a, gh na g mfano (hapendi anaandika apendi, magharibi anandika magaribi, mangaribi) akipatia spelling matamshi tabu.

Ni kweli hata fridge wanaandika "frdge", mpaka maneno mengine hayasomeki!
 
kumbe kitu cha msingi ni angalau kusoma mara kwa mara zile kwa kiswahili tunaita NAFSI na kuzielewa maana hizo ndio tatizo kubwa....utakuta pahala pa kuwekanafsi ya kwanza umoja mtu anaweka nafsi ya tatu uwingi.... hili ni tatizo... na kama kuna walimu basi wawakazanie watoto haya mambo vizuri
Tatizo hata walimu wengi wa somo la kiingereza nao ni tatizo..
 
Haswaa! Wawe wanaanza sentensi japo kwa herufi kubwa na waachage nafasi kati ya neno na neno!
 
Back
Top Bottom