Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Binti mwaka 1.6 wimbo wa darasa maisha na muziki hata kama amelala lazima ataamka na kuucheza mwanzo mwisho
 
Wazazi wakongwe hayo mambo ni kawaida.

Wazazi wapya kila muda wanataka tusikilize stori zinazohusu watoto wao.
Ukongwe wako hautuhusu na hakuna aliyekuita uje kusoma huu uzi.
Ukisema ukongwe kila mtu ni mkongwe kwa mwenzake.
Usilete stress zako za maisha mkuu kama unaona uzi hauna maana tembelea jukwaa la ufugaji, siasa n.k
 
Tatizo unabana Sana. Huwezi pata HIV hiv
 
Nimecheka saaana. Mwanao km wangu ana miaka mitatu na miezi mitatu... Anapenda mikate ila anaitengeneza iwe muundo wa bunduki ndogo ndio ale. Kingine ukitaka umpw raja mnunulie gari na bunduki( kuna zile zinazorusha maji) atalitega gari na kuanza kulilipilia mabunduki yaaani..
Being a mother is a wonderful experience.
 
Mwanangu alipokuwa ba miaka 1-2.5 hivi yaani alikuwa akisikia baba yake anaonngea kwa nguvu alafu ananiangalia anaenda kumpiga.. Nikienda nae salon km msusi anavuta nywele nikikunja sura anaenda kumpiga... Alikuwa ananilinda sana. I love him kwa kweli.
 
akilala dizain analala kama mbuzi kagoma ..hahahaha bas burudani kwel kwel..
ilo poz ndo lazma aanze kutafutia usingiz...
 

hahaha mkuu pole tafuta ata chogo la 21 inch mkuu ...litamfaa mfungieni ka corner kake...mum limit tu distance na mda
 
Mwanangu (5yrs) yeye bwana computer... Ameanza kuijua kila kona ya computer akiwa na miaka kama 2 hivi.. Saiz hashikiki kwa kuitumia iwe ni games zile za mission au kuset tu vitu mbalimbali.. Kuna vitu vingine nimemfundisha ila vingi amejifunza mwenyewe.. Kipindi cha nyuma ilikuwa kila wiki na weka Windows upya ikabidi nimtaftie tu computer yake saiz mzee kuna siku siku nikamkuta kashika bisibisi kashafungua laptop nati mbili nyingine zimemgomea kisa iligoma kuwaka.. Kuna siku nikasahau external hdd kutoka kazini kikakuta pc yake imejaa ka install kila game na software iliyopo ndani yake..
 
Yani naona kila mwenye mtoto utaskia nimtundu mala anaakili sana mala mjanja mjamja mala nini naona sifatu inamaana nyie wenye watoto wote hakuna mwenye mtoto zoba anae lialia nakulamba kamasi mdawote anae pigwa nakila mtoto humu hakuna du!!! Ebu ongeeni ukweli wenu msifate mkumbo
 
Haya mambo ya wazazi kutopata muda wa kukaa na watoto wao, kuna dogo aliharibu ndoa ya wazazi wake, bila baba wala mama kujua kwamba dogo miaka 4 ameshajua kusoma vizuri alichukua simu ya baba yake, sasa bahati mbaya sijui ilikuwaje wakashtuka anasoma meseji ya mchepuko kwa kwa sauti mpaka akaimaliza, ma mama alikuwa hana tabia ya kugusa simu ya mume wake.

Kilichoendelea hapo ni mtafaruku.
 
Wangu ni vijana wa Mwenye Enzi Mungu Mwenyewe, anawafundisha na kuwa Linda na kuwabariki Mwenyewe! Mimi wala baba yao hatuna cha kujisifia juu yao, sifa zote ziende kwa Muumbaji wa vitu vyote kwa kweli!
 
Usije ukaanza kumlazimisha asome awe daktari au mwanasheria hicho ni kipaji tayari anacho kitamtoa aongezewe tu elimu kiasi sio madegree ili mzazi ujisifie.

Hongera sana Mkuu
Asante mkuu.

Yes, sina mpango wa kuwalazimisha watoto wangu chochote.

Kwanza nawalea kisela. Tunaenda kishkaji mpaka.sometime huwa najishuku mwenyewe.

Am I wrong.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…