Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Hata mimi nimegundua wengi wamekuwa waongo sana humu
Wengine watoto wao wazembe Ila wanashindwa kusema tu
 
Siku moja nilirudi home toka mihangaikoni nikakuta kabinti kangu kanaogeshwa chumbani kwakuwa kulikuwa na baridi kali, ile nazama tu chumbani kakanirudishia mlangoni "baba rudi chebuleni uchinchungukie" nikasema asante Mungu kameanza kujitambua bado kadogo, nikatulia sebuleni, mamake alivyokachomoa ktk beseni la maji akakapaka mafuta huku amekaandalia nguo za kuvaa, ila mamake amejipindua tu, mara hako kakaja na nguo mkononi katupu kama kalivyozaliwa kakisema "baba nivalishe nguo nimechaoga".
Sijasahau hadi leo, nitamkumbusha siku ya harusi yake Mungu akipenda nikisimamishwa na MC kutoa neno kama Mzazi.
 
Hata mimi nimegundua wengi wamekuwa waongo sana humu
Wengine watoto wao wazembe Ila wanashindwa kusema tu
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hata kama wewe ulikua kilaza shuleni bado huwezi kumwambia ukweli mwanao.
Sasa kama mwanao kilaza utaanzaje kusema hapa wakati wataalamu wanajua akili za mtoto ni suala la kurithi inamaana ukisema mwanao ni kilaza simply unamaanisha wewe ndo kilaza au mkeo[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Je uko tayari kusema wewe ni kilaza??
 
Mm mwanangu anamsumbua sna babaake, muda wa usiku akitaka kulala babaake anamvalisha pampers sasa hataki kuvaa anaangusha kilio anataka na babaake avae
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] wafanane
 
Good lkn tuwe makini mwanga huo na macho cyo salama
 
Huyo atakuja kuwa kiongozi wa migomo mingi huko mashuleni
 
Ukongwe wako hautuhusu na hakuna aliyekuita uje kusoma huu uzi.
Ukisema ukongwe kila mtu ni mkongwe kwa mwenzake.
Usilete stress zako za maisha mkuu kama unaona uzi hauna maana tembelea jukwaa la ufugaji, siasa n.k
Hahahaaaaa bora umempa vyake asitukate stimu buana[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Amen
 
Mwanangu one year now...ameonyesha kupenda sana mziki akisikia wimbo wa jux hapalaliki....anaimba na kupiga kelele ....na akiwa amelala akisikia tangazo LA airtel money lzm aamke acheze kwanza ndio alale tena....yan nafurah sana kuona vituko vyake
 
Mungu wangu...!! yani watoto niliowatupa bafuni nadhan wangekua wananipa furaha sasa hivi daah...anyway tusubir labda next day inshalah nitapata furaha na watoto wangu wajao...
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] huo ugali sasa
 
Mwanangu is so sweet kwa kweli,hadi huwa natamani muda uende haraka nitoke kazini nimuwai kabla hajalala

Akinisikia tu nje ya geti ananikimbilia huku anashangilia mama mama utasema hajaniona mwezi mzima

Atataka nimpe pochi,tukiingia ndani,anataka kunitoa viatu,ananiingizia pochi na viatu ndani

NB: huwa anachukua remote ya TV anaweka sikioni alafu anaongea eti ndio simu

Au akifanya kosa,ukamuita,akifika tu anaanza Ku count numbers/alphabets au kuimba nyimbo zake za shule,nabadilisha mawazo ya kumgombeza

Next month anatimiza 4 years
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…