Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Mwanangu wa 3 ana umri wa miaka 6 hivi....,,week iliyopita nilimnunulia FIRIMBI,,,aisee hatukulala siku hyo....hadi Tisa za usiku ANAPIGA FILIMBI TU...hatukulala siku hiyo ni KELELE ZA FIRIMBI USIKU MZIMA,,,ikabidi niichukuwe nikaiweka chumbani kwangu,,,ALFAJIRI SAA KUMI NA MBILI,,,,,nasikia MTU anagonga mlango,,kufunguwa ni yeye,,,anataka FILIMBI YAKE,,,aisee ZILIPIGWA FILIMBI MFULULIZO HADI NIKAJUTA KUMNUNULIA FIRIMBI,,...duu...tuliendelea KUPATA ADHA YA KELELE ZA FILIMBI hadi tulipoamua KUPANGA MATOKEO YA KUIFICHA,,,,hapa ninapokwambiya KANUNA HATAKI CHOCHOTE inatakiwa FILIMBI IRUDI...sijuwi itakuwaje,,,watoto aisee...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie sina mtoto lakini nikikumbuka vyenye nilimpa stress mama na baba.. huwa nawafata nawapa pole..tena kuna nengine nawakumbusha wanachekaaaa... inshaAllah nitapata wangu tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe hii mbaya sana. Emu fanyeni ustaarabu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi wa kwangu ni Anamika 2 Sasa huyu mtoto amejua kuhesabu 1..10 kwa kiswahili na kingereza tangu akiwa na mwaka 1.2 na hakuna day care Wala shule yoyote alio enda zaidi ya mama take.

Huyu mtoto mkifika ugenini Basi akitulia zake anaanza kuhesabu ile serious na kwa sauti Hadi watu wanashangaa kwa umri wake imewezekanaje Hadi Kuna siku babu yake akajisifia eti mtoto kachukua akili zake na katika wajukuu ametokea kumpenda haswa.

Alafu pia ni mtoto mwenye maneno ya hekima na kufariji Sana ukimpatia kitu hachoki kusema nashukuru sana,ubarikiwe na Mungu akutunze Sasa kwa umri wake amejizolea umaarufu mtaani atu wanaamini ni malaika maneno yake yanabaraka za kweli hivyo basi wanamnunulia vitu na anapendwa sana.

Kuna siku alilia tumpigie simu Babu yake basi mama yake akafanya hivyo aliishia tu kumuambia Babu yake asalimia Babu , Ashante Babu, Mungu atunze Babu haya maneno Kama umemfanyia vibaya ni maneno yanayo choma Sana.

Kwenye vioja kunasiku badala atumie pot lake kujisaidia yeye akaenda kujisaidia kwenye hotpot Tena hotpot icon ambalo ndio linategemewa kwenye kupamba kabati [emoji1][emoji1][emoji1] hili hotpot lilioshwa lkn Hadi leo halitumiki tunaliogopa .

Akiwa na hasira ni mkali Sana na haijalishi ni Nani atakunyoishea kidole na kukufokea ukitaka aache ni wewe kuondoka Ila ukisema sijui umchape aisee utaua tu bure . Maana anaujasiri mkubwa Sana na misimamo mikali Sana na hayumbishwi kwenye kile anachokiamini .

Pia akiwa katulia anafanya kitu kikiwa hakileti matokeo yale anayo yataka atapandwa na hasira na kuanza kuharibu hicho kitu Kama ni nguo anavaa haivaliki ataibeba kwa hasira na kwenda kuitupa nje [emoji38][emoji38]


NB
Jaman tuwatunze watoto na tuhakikishe ni wasafi wanavutia Sana, mwanao akiwa msafi atapendwa na kila mtu .

Mimi wa kwangu ni star wa mtaa si watu wazima si watoto wenzie wote wanampenda imefika kipindi amewashika masikio Hadi watoto wenzie walio mzidi umri
 
Mwanangu ana miaka miwli kasoro miezi 3
Ni wa kike, anapenda sana kushka simu ya mama hasa ninapokuwa mbali nae

Lengo mama anipigie ili niongee nae

Abi mambo- pwafi,,unacheza- eee,,Sasa muulze kitu ambacho hafanyi mfano
"Unakula mwangu"? Anajbu kwa kutingisha kichwa akimaanisha hapna , kuongea bado taabu kidogo

Juzi nimeingia bandani nikatoa mayai ya kuku mabovu yote,,nikaweka ndani ili mama yake akiamka ayatupe.Nikaenda zangu kazini,saa nne nakuta message ya mama ake mwanao kapasua mayai yote bandani na yale mabovu nyumba nzima inatoa harufu ata hatupiki leo [emoji2][emoji2]

Mama yake anasema huyo mtoto namdekeza sana ngoja anionyeshe yaan ukiamka tu naye yupo tayari daah.
 
Muombee ulinzi wa Mungu
 
Dogo janja anaendeleaje sasa
 
That's a very smart kid.
 
Kama siyo waumini wa dini, huyu wa kukaa macho usiku na kulala mchana mnatakiwa mumubadilishe jina. Anatakiwa kupewa jina la mtu mwingine, especially kama amechukua jina kutoka ukoo wa mama, mnatakiwa mmbadilishe mmpe jina kutoka ukoo wa Baba.

Vinginevyo solution rahisi kabisa kuliko zote, mpelekeni kwa Baba Paroko au kwa Baba Mchungaji
 
[emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787]
 
Huyo ana dalili za wivu kama mwanangu , hata akiwa anacheza bize kiasi gani ukimkumbatia mama yake dogo anakuja mbio mbio anataka mama yake ambebe[emoji23] [emoji23]
Hasa watoto wa kiume[emoji16][emoji16][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…