Mtu akijamba hata Kama si yeye bali ni wewe baba kwanza anastuka afu anacheka ukimuuliza unacheka nini anamuangalia mamayake alafu alafu anasema mama kajamba, maskini mama wa watu pengine hata c yeye, tabia hii huwa anamuuzi sana mama mtu yaani hata apumue yeye atasema mama yake ndo kapumua, pia kuna kale katabia anaingia chumbani we uko seblen, alafu unakuta kimya kimepita, kupo kimyaaaaaaa kumbe yeye huko unaweza mkuta labda analamba sukari au maziwa ya kopo au kashika simu yaani lazma kuna jambo utakuta kisha zingua, jambo jingine kwa mtoto wangu wa miezi minne huyu yeye ndio nimegundua juzi kwamba akilala hajikojolei, akiamka pia hakojoi ila anakojoa ukimbeba tuu anamwaga kojo huku anatabasamu, tabia ingine ambayo inanikera ni pale jioni nikitoka kazini akiniona hata kama alikuwa ananyonya ataacha atanishangilia kwa vicheko na tabasamu huku akiinua mikono umchukue sasa ukimchukua ndio kama umejipalia mkaa utafunga nae ndoa, hataki umweke chini yaaani umbebe mpaka sa tano usiku au mpaka upate hasira na majuto kwa nini umembeba...vinginevyo atalia hadi sauti ikauke...tena analia huku anakohoa basi unamuonea huruma unakuta unambeba tena huku masaa yanaenda hakupi nafasi ya kula wala hupati nafasi ya kuoga na wala halali, hali inaenda hivi mpaka mamayake akuonee huruma ni nusu ya usiku, maana hata yeye hunipa mashtaka kwamba dogo anamnema mchana, so mchana kazi na usiku ulezi,