Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Halafu wangu haniiti baba, yeye ni mwendo wa kuniita baba Grace, vile anavyoniita mama yake.
Wakati wa kulala, nikimuambia sali, anagonga ile sala ya kuombea chakula, nadhani RCs wenzangu wanaipata hiyo.
The Same na wakwangu ananiita baba malu Kama anavyoniita mama ake, kenyewe kanaitwa Marcus sasa kitaani wakalitohoa jina na kumuita malu kwa kifupi
 
Jembe langu lina maswali flan ya kichunguzi sana halafu ana kumbukumbu ukimwambia kitu inabidi uwe makini kuna siku atakuumbua,mbaya zaidi au nzuri anapenda sana ishu za kijeshi jeshi, kuna siku tunaangalia maadhimisho ya Muungano gwaride linapigwa ye katulia tuuuliiiii duuh baadae nmkuta nje kashika gongo kaweka begani anapiga kwata na sauti za kikakamavu "mbeeeleeee tembeeeaaaa.....nyumaaaaa geeeukaaaaa"....

Moja ya maswali aliyowahi kuniuliza nilienda nae benk ATM kutoa hela akaangalia mchakato ulivyo baadae akaniuliza "hivi baba zile hela kuna mtu ndani anazitoa au zinatokaje?" hahahahaaa

Siku nyingine Aliuliza hivi mvua inatoka wapi? au Mungu anamwaga maji? daah

Kubwa kuliko alikua anacheza na wenzake wakamtania "mwangalie kichwa chake" duuh karudi amekasirika analia anasema "baba hiki kichwa sikitaki niletee kingine" Ilibidi niuvae ubaba kumtuliza.

kua na mtoto au watoto ni faraja sana....
Hahahhahahahahhahaha
 
Mwanangu 4 years old tunalingana matonge... [HASHTAG]#natafta[/HASHTAG] shamba
 
Wangu ana Mwaka na Nusu the funny thing is akisikia naongea na mama yake kuwa naenda sehemu fulani au akaona nimeshika funguo ya gari utaona mtu yupo bize atatafuta viatu vya na vyangu anaanza kutaka kuvalishwa viatu ili safari ianze [emoji23] [emoji23]
 
ha ha ha nina wa kwangu now ni 2.1 years na ni wa kike, ila tabia na vituko vyake unaweza sema ni wa kiume
1) Akinikuta nimekaa na mama yake karibu labda nimemshika/kumuwekea mkono ni mawili either aje aning'ate au achukue kitu chochote na kunipiga nacho, hajui kama yule ni mkewangu.

2) Simu yangu ikiita hata kama niko chooni unaweza katisha shughuli maana atakusumbua mpaka uichukue...

3) Sikumbuki mara ya mwisho ameniita baba ni lini.....mara zote kama si kuniita kwa jina langu (kwa lugha ya kitoto) au baba xxxx (xxx ni jina lake). Ni mama yake tu ndio anaweza muita mama au wakati mwingine anamuita mama xxxx (xxx ni jina lake).

4) Ana uwezo mkubwa wa kujua saa hii baba au mama anataka kutoka basi utamkuta mlangoni na viatu mkononi...kumkimbia hapo ni shughuli kubwa.

5) Tabu ipo kwenye TV...mnaweza kua mnatizama kitu muhimu labda na marafiki (let say habari/movie) then yeye atatafuta remote ilipo na kutaka mumuwekee katuni...neno lake ni moja tu "toto", hapo hatulii mpaka muwekee. Katuni zake ni channel ya BBC inaitwa ceebees tofauti na hapo hakieleweki.

6) Ukimvalisha pampasi na akishikwa na mkojo atakulazimisha mpaka umvue akojoe. Mara nyingi hua tunamvua ili hata siku akivaa kawaida asijikojolee.

7) Poda za mama yake zinapata tabu sanaaa.....! Mama yake akijisahau tu...imekula kwake maana atajipaka vyote.

8) Tukiwepo nyumbani, hakubali hata kidogo kuvalishwa/kuogeshwa/kulishwa na dada. (Napenda sana hii part).

9) Asikuone unampa mtu hela......atataka ampe yeye. Tukiwa out/dukani malipo yote anafanya yeye....yeye ndio anataka kushika hela.

10) Jana alifanya kituko cha mwaka....mara nyingi hua akiwa na homa or flue hivi tunalala nae kwa ajili ya uangalizi wa karibu, sasa nimeshtuka saa kumi usiku tunakuta hakuna mtu kitandani tukajua ameanguka chini kumbe ameteremka na kwenda kulala kwa dada yake....anauwezo wa kufikia vitasa vya milango yote (isipokua jikoni na chooni) na sisi hatuna tabia ya kujifungia kwa ndani milango ya vyumbani.

11) Kua na mtoto ni raha sana...ila Omba Mungu sana asipatwe kila mara na yale magonjwa ya kitoto. Mtoto akiumwa the whole family imeumwa.
 
Mtu akijamba hata Kama si yeye bali ni wewe baba kwanza anastuka afu anacheka ukimuuliza unacheka nini anamuangalia mamayake alafu alafu anasema mama kajamba, maskini mama wa watu pengine hata c yeye, tabia hii huwa anamuuzi sana mama mtu yaani hata apumue yeye atasema mama yake ndo kapumua, pia kuna kale katabia anaingia chumbani we uko seblen, alafu unakuta kimya kimepita, kupo kimyaaaaaaa kumbe yeye huko unaweza mkuta labda analamba sukari au maziwa ya kopo au kashika simu yaani lazma kuna jambo utakuta kisha zingua, jambo jingine kwa mtoto wangu wa miezi minne huyu yeye ndio nimegundua juzi kwamba akilala hajikojolei, akiamka pia hakojoi ila anakojoa ukimbeba tuu anamwaga kojo huku anatabasamu, tabia ingine ambayo inanikera ni pale jioni nikitoka kazini akiniona hata kama alikuwa ananyonya ataacha atanishangilia kwa vicheko na tabasamu huku akiinua mikono umchukue sasa ukimchukua ndio kama umejipalia mkaa utafunga nae ndoa, hataki umweke chini yaaani umbebe mpaka sa tano usiku au mpaka upate hasira na majuto kwa nini umembeba...vinginevyo atalia hadi sauti ikauke...tena analia huku anakohoa basi unamuonea huruma unakuta unambeba tena huku masaa yanaenda hakupi nafasi ya kula wala hupati nafasi ya kuoga na wala halali, hali inaenda hivi mpaka mamayake akuonee huruma ni nusu ya usiku, maana hata yeye hunipa mashtaka kwamba dogo anamnema mchana, so mchana kazi na usiku ulezi,
 
Kuna Mtoto Wa Mshkaj Wangu Ana Miaka 2, Kuna Cku Nmemtembelea, Alibebwa Na Bnt Wa Kaz Akaanza Kumshika Ziwa Akasema " Dada Nyonyo Yako NJuli" Babaake Akamkemea Na Kuamuru Asiwe Anambeba Beba Km Ndo Mchezo Wake. Ki Ukweli Kale Kabint Ziwa Lilikua Limesimama Af Limejaa. Me Nkamtania2 Mshkaj Nkamwambia Like Father Like Son
 
Mpwa wangu alikuwa anaonjeshwa bangi na baba yake toka akiwa mchanga kisa baba yake anajifanya Rastafarah. Sasa dogo ana miaka 12 shule hataki anataka aende Tarime akalime bangi na kuwa mjasiliamali kupitia bangi.
bangi.jpg

Hapa akiwa na baba yake miaka hiyooo
lighter.jpg

Hapa akiwa ndiyo hataki kabisa shule...(wa kwanza toka kushoto)...anataka kuwa mjasiliamali wa bangi huko Tarime. Yaani shida kweli kweli nyumbani kwa dada yangu.
 
Nadhani kilicho bora ni kusubiri wakue. Mana hata nami nilikuwa na mpango wa kupaka rangi hivi karibuni. Kumbe itakuwa kazi bure.
Mie nimeipaka juzi juzi tu hapo. Nayo ishachorwa zamani. Patterns na days na dates.
Suluhisho ni kupaka rangi washable. Silk au water guard. Wakichora unaweza kufuta.
 
Back
Top Bottom