kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Muda wa maandamano ya vyama vya siasa Bado kabisa, ukifika hakutakuwa na chombo kitakachoweza kuyazuia kufanyika. Hakuna nguvu itakayoweza kuzuia nguvu ya umma muda ukitimia. Sasa hivi mnachofanya ni vurugu TU (nuisance), wananchi hawawaelewi mnachomaanisha, ndiyo maana maandamano yenu yanadhibitiwa kirahisi TU.
Jengeni vyama kwanza hadi kwenye ngazi ya mioyo ya watu kule mashinani. Waelezeni watu njia mbadala za kuboresha maisha yao wanakoishi ili waelewe. Ishini nao, kuleni, vaeni, laleni na somesheni watoto wenu kama wao.
Haiwezekani mwenyekiti wa chama amekamatwa lakini nchi yote imetulia tulii kama vile hakuna kilichotokea, mko peke yenu TU na wapendwa wenu TU.