Viongozi imarisheni vyama, maandamano Bado muda wake

Ni mpumbavu pekee anayeweza kulinganisha vitu visivyofanana!
Unataka kuchora picha kubwa kuwa Tanzania kuna tabu nyingi kuliko nchi nyingine. Yaani unatembea na wake za watu wenyewe wakikuchukulia hatua unaita watu waandamane. Unawadhulumu wafanyabiashara wenzako, wakikuadhibu unatuita tukaandamane. Unamtukana Rais ukiadhibiwa unaita watu waandamane.
 
Waunga juhudi watekwe na Mungu kama akikosekana wa kuwateka. Ni wasaliti na adhabu ya msaliti kiapo chake hata Mungu hamtaki. Mtu kaenda kuwaficha watoto wake nje ya nchi wako salama halafu yeye anataka watoto wa wenzake wakaandamane wasiende shule. Wakati wengine wakikimbilia kujificha kwenye balozi za wazungu nchini amani ikitoweka, sisi wengine hatuna hata passport.
Ulisukuma magari au walikusukuma mkundu?
 
Ningekujibu ila ninakuonea huruma, asante.
 
Ningekujibu ila ninakuonea huruma, asante.
Nimemsikia jamaa anataka kukamata ndege zetu (kodi zetu) sisi wakulima wa Nanjilinji kwa manufaa yake binafsi, anafaa kuwa Rais wa wote huyu?. Saa ya maandamano bado kabisa, ikifika kila mtu atajua kuwa imefika, hakutakuwa na kuhamasishana wala hakutakuwa na nguvu ya kuyazuia isitokee. Endeleeni kuwaombea CCM wafanye makosa tu kwa wananchi wake. sasa hivi bado hawajakosea kwa kiasi hicho.
 
Ulisukuma magari au walikusukuma mkundu?
Whatever, lakini ninachokuambia ni kwamba sasa hivi nchi haiko tayari kuandamana kwa kishindo kama unanvyotaka. Utakamatwa wewe na hakuna nguvu ya umma yoyote itayolazimisha wewe uachiliwe, maana nguvu hiyo haipo na haijatayarishwa kufanya hivyo. Mmewachuuza wananchi kwa miaka mingi kuanzia kulee kwa akina Lamwai, Marando, Lyatonga, "Tumbili", Dr. Slaa, Mdee, Nasari, Mtoleya, Prof. Lipumba, Mch. Msigwa, na wengine wooote ambao walienda na kura na nguvu zetu kwenda kuunga juhudi na hakuna kiongozi yeyote aliyejitokeza kuomba msamaha kwa niaba yao waliokwenda kuunga juhudi. Watu hawana imani na vyama vya upinzani any more. Kila mtu ameamua kwenda mwenyewe kuunga juhudi za mama 2025.
 
Nani kakutuma utusaidie kudai haki?
m
 
Sera haziundi vyama, vyama/vikundi vinaundwa na watu/wananchi ndio wanachama/ wafuasi. hayo unayotaka ni uongo unaoenezwa na CCM.

Maandamano ni hisia kupinga wasiyoyataka, hayahitaji sera wala katiba ya vyama.
 
Unataka waimarishe vyama halafu hakuna maandamano? Sasa watahamasisha watu vipi? Traditionally kuhamasisha watu lazima uwakusanye ili uwahutubie, labda ungebadirisha msemo useme vyama vijijenge kwa kuwasiliana na watu wao kimtandao, lakini hapo utwaacha nyuma wale wa vijijini.
 
Umeweka bandiko je ulijitafakari kabla au Ni Uchawa wako umekutuma!
Je unaishi Tanzania hii kweli.
Au Kuna alikutuma na kukupa posho ya buku 7!!!
WaTanzania wanaumia na kupotewa na kuuliwa ndugu na watoto zao wewe unaleta upuuzi FK uu.
 
Kuna tofauti kati ya maandano na mikutano, kwani wamezuiwa kufanya mikutano ya kuwaambia watu njia bora ya kutawaliwa?

Kama utavaa miwani yako ya kuonea utagundua kuwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanataka Tanzani ifungiwe mahusiano na nchi nyingine kama njia mojawapo ya wao kwenda Ikulu. Wanakasirika kusia Mtanzania ni Rais wa Mabunge ya dunia, mtanzania ameteuliwa WHO, Tanzania inapewa misaada, watalii wanakuja Tanzania na mambo mema yanatokea Tanzania. Ukweli ni kwamba siasa za aina hiyo hazilisaidii taifa na watu wake, na wananchi sio mbumbumbu kama wanavyofikiria wao. Watanzania wa leo wanajua totauti yao na nchi yao na mataifa mengine yanayowazuunga na hata mataifa ya ulaya na Asia. Huwezi kusema mtanzania wa leo hajui kuwa Marekani kuna watu hawana pakulala (homeless) wanaolala kwenye baraza za nyumba, magari mabovu, na kando ya barabara na reli. Anataka kusema pale Marekani hakuna watu wanauliwa kila siku?.

Mbona Marekani na Ulaya zinashindwa kusaidia kuleta amani DRC, Somalia, Sudani, Ukraine, Ethiopia, Iraq, Libya, Haiti, Palestine, Israel, Syria, nk. Namuunga mkono Mama Samia kuwaambia wazungu wasitufundishe namna ya kuendesha nchi yetu, maana hawatakuwa na masaada wowote pia kurudisha utulivu kama utulivu wetu utapotea pia. Wacha tuendelee hivihivi na utulivu tulionao hata kama amani sio kubwa sana. Maana nchi yenye vita hakuna maandamano wala mikutano ya hadhara.
 
Umeweka bandiko je ulijitafakari kabla au Ni Uchawa wako umekutuma!
Je unaishi Tanzania hii kweli.
Au Kuna alikutuma na kukupa posho ya buku 7!!!
WaTanzania wanaumia na kupotewa na kuuliwa ndugu na watoto zao wewe unaleta upuuzi FK uu.
Tanzania tuna watu wanapotea na kufa kuliko nchi gani? au huna exposure?

Kwahiyo Tanzania ina watu wengi wanaokufa na kupotea kuliko Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, DR Congo, Sudani, Ethiopia, Malawi, South Africa, Burkina Faso, Nigeria, Mali, Niger, au Marekani? acha puuzi na uroho wa madaraka kwa njia ya mkato.
 
Absolutely correct. Lakini na wabongo sisi pia tuna matatizo sana kwenye hilo eneo la ufahamu, kuhamasika, kuelewa haki zako, kuelewa nini cha kufanya na proactiveness kwenye kudai haki. Sishangai kabisa kuona kilichofanyika watu wanaendelea na bussiness as usual. Ni kweli setting na social cultural context za wabongo, akili zetu , culture zetu za kiswahili na umbeya wetu,it will take a century to reach awakeness level hiyo unayoongea. Labda Kizazi hiki kitakuwakimekwisha potea.
 
Mtu anaweza kuona kama vile watz ni waoga na hawajui haki zao, inaweza kuwa ni kweli lakini kila kitu kina natural history yake. Tanzania ni nchi ambayo imekuwa ikopokea wakimbizi wengi kutoka nchi mbalimbali tangu tulipopata uhuru. Tumekuwa na makambi ya wakimbizi kutoka Burundi, Rwanda, Uganda, DR Congo, Msumbiji, Angola, Zimbabwe, Afrika kusini, Somali na Comoro katika sehemu mbalimbali za nchi yetu. Tanzania imehusika sana katika kusuluhisha nchi zinazopigana na wanaopigana wenyewe kwa wenyewe' tunazo mahakama zao hapa. Tunajua kuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe hailetwi na wageni, bali inaletwa na wenyeji wanaowaleta wageni wa kushirikiana nao kwa makubaliano/malipo fulani.

Hivyo, kutokana na uzoefu wa kupokea na kuishi na wakimbizi watanzania wanafahamu thamani ya amani na utulivu, wanajiona wana haki nyingi kuliko nchi zinazotuzunguuka, wanafahamu madhara ya kupoteza amani na utulivu. Hivyo ni wepesi sana kumpuuza mpuuzi mmoja anaetaka kuwatumbukiza kwenye kuwa wakimbizi, na hawajui watakimbilia nchi gani kama amani yetu ikitoweka. Ukweli kila mtanzania anaona ni heri kumtosa abiria mmoja anaetaka kulitoboa jahazi lizame ili wengi wapone.
 
Nchi masikini kama hii ya kwetu inayotegemea misaada na mikopo kujenga madarasa na kununua madawati unataka taifa litumie fedha nyingi kusimamia maandamano nchi nzima kila siku miaka 5 baada ya uchaguzi kumalizika? ni nchi gani inafanya hivyo? Waliachiwa wafanye maandamano nchi nzima, hayakutosha? Hata ulaya hawafanyi hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…