Viongozi kumi (10) Bora Tanzania

Baadhi yaliyokuwemo katika utawala wa Mwinyi

1. Azimio la Arusha la mwaka 1967 la ujamaa na kujitegemea liliwekwa kando na Azimio la Zanzibar la 1992 la soko huria (Ruksaa)

2. Mfumo wa chama kimoja (1965/1977) uliondolewa na kuwekwa mfumo wa vyama vingi (1992). Wanachi 20%, wakiongozwa na Baba wa Taifa Mwl Nyerere, wakiukubali huku 80% wakiukataa.

3. Kiliundwa cheo kisicho cha kikatiba cha naibu waziri mkuu na wakati huo alikuwa Lyatonga Mrema.

4. Viongozi na familia zao, wakageuka kuwa wafanya biashara wakubwa na wasiolipa kodi. Rasilimali za nchi zikaanza kutoroshwa nje kama dhahabu iliyokamatwa airpoti ya JNIA.
"Ikulu isigeuzwe pango la wanyanganyi"(NYERERE).

5. Muungano ulipata msukosuko mkubwa haswa kwa kitendo cha Zanzibar kutaka kujiunga na umoja wa nchi za kiislam (OIC) na vuguvugu la kutaka kujitenga la G55.

6. Sarafu ya shilingi ikashushwa thamani kufuatia maelekezo ya IMF na tukaanza kuona noti mpya za shilingi 200, 500, 2000, 5000 na 10000 zinazodunda hadi leo.

7. Pesa ikawa rahisi kupatikana, biashara kedekede, watu wakawa na fedha kuliko serikali yao. Wakati huo serikali ilikuwa inakusanya Shilingi bilioni 25 kwa mwezi.

8. Wanyama mwalimu aliocha Ikulu kama Swala, Mbuni na Tausi wakaanza kupungua kwa kasi.

9. Wafanya biashara wakubwa kina Bakhresa, Mengi na Raza wakaibuka kipindi hiki.

10. Vyombo huru vya habari, TV, Radio Fm na Magazeti vikashamiri.

11. Mwalimu Nyerere akawa raisi mstaafu mwenye nguvu na ushawishi mkubwa, huku akisimama na kukemea mambo mbalimbali aliyoyaona hayapo sawa

12. Shule za Sekondari za serikali zilikuwa zinafungwa mara wa mara kwa kukosa chakula.
13. Ada ya shule za Sekondari ya Serikali ilipanda kutoka elfu nne hadi nane kwa mwaka.
14. Michael Jackson alitembelea Tanzania huku kajifunika puani kuzuia harufu mbaya na vumbi la Dar es salaam na alifika hadi Ikulu wakati huo Ikulu hakuna masofa [emoji3]
15. Nyerere alimuita Rais Mwinyi ni dhaifu ukiangalia kwenye kitabu cha Mwl Nyerere cha Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania cha Mwaka 1994 ukurasa wa 66 Mwl aliandika hivi Nanukuu "Rais Mwinyi ni mtu mwema na mpole lakini ni kiongozi dhaifu; na upole wake na udhaifu wake unatumiwa na watu ambao sio wema"

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Kwani kuwa kiongozi ni lazima uwe mwanasiasa?

Mbona list haina CEO, Labour Union leader, religious leader, military leader, business magnate, social movement leader, etc.
 
Kilichomfanya mleta mada asimuweke salim ktk list yake nafikiri (1) dini yake (2) uzanzibar wake. Angekuwa dini moja na mleta mada basi tungemuona akishika hata nafasi aliyompachika Chifu Mkwawa
 
1) azimio la Arusha ndio iliyokuwa sababu ya watanzania kutoka katika maisha ya kawaida na kuanza kuishi maisha ya umasikini wa kutupwa. 2) Mfumo wa vyama vingi uliondolewa na huyo huyo Nyerere unaesema aliongoza 20% ya watanzania kudai demokrasia, lengo la Nyerere kuondoa demokrasia ilikuwa ni kutaka kuiongoza Tanzania kwa mawazo yake yeye, inamaana hata akikosea kama binadam asiwepo mtu mungine wa kumkosoa. 3) sipingani na ww. 4) Hata wakati wa Nyerere walanguzi wengi walineema kwa kuiibia serikali na kuja kuwauzia watu mitaani ilikuwa hauwezi kula milo mitatu bila kujigusa mfukoni, kwahiyo wenye pesa zao hawakwenda kupanga folen bali waliletewa majumban na walanguzi, Mwinyi alipoingia madarakan alianza kwanza kukomesha hawa walanguzi kwa kuanzisha "fagio la chuma" ambapo walanguzi wengi walikamatwa, walifungwa na wengine kutoroka nchi. 5) Muungano huwa unapata misuko suko awamu zote hata wakati wa Nyerere, uliza kuhusu mzee Jumbe utaambiwa. 6) Sarafu kushushwa thaman huku wananchi wakipata mahitaji yao ya msingi kama chakula, madawa, nguo nk sioni tatizo, hauwezi kuacha mtoto wako afe na njaa au magonjwa eti kwa kuogopa kushushiwa hela yako thamani. 7) Unasema pesa ikawa rahisi kupatikana, biashara kedekede, watu wakawa na fedha kuliko serikali yao, wakati huo serikali ilikuwa inakusanya sh bilion 25 kwa mwezi.. lkn umeshindwa kujua kwamb kabla ya Mwinyi hela haikupatikana kirahisi, biashara haikuwepo kedekede, na watu hawakuwa na fedha kuliko serikali. Lkn bado Mwinyi alipoingia alikuta hazina nyeupee yan serikali haina pesa hata kidogo na ndio sababu ilisababisha Nyerere akoswe koswe kupinduliwa (au haulijui hili la kupinduliwa?) 8) Hili sina uhakika nalo huenda ni kweli au ni propaganda tu zile zile za kumchafua Mwinyi. 9) Hapa kuna ukweli. 10) Kweli. 11) Mi nafikiri kwa kiasi kikubwa aliheshimika tu kama baba wa taifa lkn angekuwa na nguvu kama hii unayoisema hapa sidhani kama Mwinyi angeweza kuyafanya yale aliyoyakataa Nyerere. 12) Chakula kilianza kuingia kwa wingi wakati wa utawala wa Mwinyi, afu useme eti shule zilifungwa tu kipindi chake kwa kukosa chakula!! Hii bila shaka ni zile zile propaganda za kuchukua mabaya ya Nyerere kumtwisha Mwinyi na kuchukua mazuri ya Mwinyi kupewa Mkapa. 13) Vitu hupanda kutokana na wakati, hata ww hapo ulipo bei ya kiatu au kitanda uyonunulia leo haiwezi kuwa sawa na bei ya kiatu au kitanda uliyonunulia mwaka 2005 uliyonunulia mwaka, pia bei ya ada ya sekondari wakati wa utawala wa Mwinyi au Mkapa haiwezi kuwa sawa na hii ya leo ya utawala wa raisi Samia. 14) Haya ni maneno ya mitaani yasikupe shida kijana. 15) Hizi ni propaganda tu.. Nyerere aliona Mwinyi ashafanya mambo mengi ya kiubinadam na kiutu ktk kuinua nchi kwahiyo akahofia asije akapoteza heshima kwa kuonekana yeye(Nyerere) hajafanya chochote cha maana kwa wananchi wake. Ndo akaja na propaganda za kumchafua chafua kwa kila baya au zuri alilolifanya ilimradi watu wasione mema ya Mwinyi, na kweli kwa 90% kafanikiwa.
 
Kwani kuwa kiongozi ni lazima uwe mwanasiasa?

Mbona list haina CEO, Labour Union leader, religious leader, military leader, business magnate, social movement leader, etc.
Mtaje hata CEO mmoja ambaye amekuwa na Influence/Ushawishi mkubwa na kuacha alama katika Jamii ya watanzania iliyobadilisha fikra na mitazamo na kuweka misingi ya jamii/nchi ya Tanzania katika historia. Shida ya Business magnate na hao CEO's ni kwamba wapo hapo kimaslahi ya biashara zaidi.They are not there to serve society ndio maana Legacy zao huwa zinatoweka mapema katika jamii.Mfano Bwana Abushiri, Tajiri na mfanyabiashara mashuhuri kama asingeshirikiana na Mkwawa katika mapambano ya kudai uhuru wa watanganyika huenda leo hii tusingemkumbuka pamoja na utajiri wake.Mara nyingi Legacy ya mtu huachwa kwa kujitoa kwake katika mambo yanayowagusa wanajamii moja kwa moja.
 
Kilichomfanya mleta mada asimuweke salim ktk list yake nafikiri (1) dini yake (2) uzanzibar wake. Angekuwa dini moja na mleta mada basi tungemuona akishika hata nafasi aliyompachika Chifu Mkwawa
Sidhani kama hoja yako ina mashiko mkuu, Mkwawa alikuwa dini gani? Alikuwa Mzanzibari au Mtanganyika? Mwinyi pia alikuwa dini gani?
 
Nitarejea kwako mkuu
 
Sidhani kama hoja yako ina mashiko mkuu, Mkwawa alikuwa dini gani? Alikuwa Mzanzibari au Mtanganyika? Mwinyi pia alikuwa dini gani?
Ni kwa vile mwanzo wa uzi wako ulikuwa haujamuweka kiongozi hata mmoja wa dini ile, japo wapo waliofanya mazuri zaidi ya baadhi ya uliyowaweka hapa (mmoja wao ni Mwinyi) ndio maana ikaonekana kama huu uzi umekaa kidini. Wengi tulishangaa uzi kujaa hadi machifu wa makabila kama Mkwawac, huku ukiacha viongozi wa kitaifa na waliolifanyia makubwa taifa hili kama vile mzee Mwinyi. Hata Mkapa uliemuweka humu alikuta kila kitu kishasetiwa na Mwinyi alichofanya yeye ni kutelezea mle mle alipoishia Mwinyi, lkn kwa vile ni dini yetu ulimuweka yeye (Mkapa) na kumuacha mzee Mwinyi mpk pale tulipokusahihisha
Sidhani kama hoja yako ina mashiko mkuu, Mkwawa alikuwa dini gani? Alikuwa Mzanzibari au Mtanganyika? Mwinyi pia alikuwa dini gani?
 
Huyo namba 3 mtoe hapo , hastahili , kumuacha hapo ni kumkufuru Mungu , jiangalie
Kwann mkuu mbn nilikuona unapiga picha juu ya daraja la ubungo? Au ndo umefata ule msemo wa "baniani mbaya, kiatu chake kizuri"!
 

Kwa #3, #4 na #7 nakukatalia mapema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…