Viongozi mtatuua kwa sonona

Umetoka kula Mbuni na Swala.
Umeshiba sasa.
 
Mchele kilo 3500? C yule jamaa alisema amezunguka nchi nzima hakuna bei ya punje 3500 kwa kilo?
 
Angalizo:

Serikali ya CCM wanapoongelea VIJANA,

Wanamaanisha vijana wa UVCCM.

Kama wewe ni kijana na haupo UVCCM, wewe ni Mzee😃😃😃
 
Mchele kilo 3500? C yule jamaa alisema amezunguka nchi nzima hakuna bei ya punje 3500 kwa kilo?
CHADEMA walioko Mwanza wanaripoti soko la mirongo Mchele ni 3000 Kwa kilo,

Kama Bei ni hiyo Leo mza, dar baada ya wiki Bei itakuwa 4000 Kwa kilo.
 
Mawazo kama haya ndio yanawaponza,tuma maombi Kupitia Halmashauri Yako.

Hata Vijana wa CCM wakipata ni sawa pia.
Nimewahi tuma Halmashauri vijana wangu kadhaa, wakaambiwa wajiunge ktk makundi na wote wawe na card za CCM!!!

Ikabidi warudi tu mtaani kuendelea kuhangaika,

Maana waliseema kuliko kujiunga CCM ya sasa Bora wasubiri Mkombozi mwingine aje.
 
Ni wapumbavu, watoto wa mama na wale wanaoishi kwa shemeji zao ndiyo watakukejeli! Ila kiukweli hali mtaani ni mbaya.

Binafsi sijawahi kushuhudia bei ya chakula kupaa kiasi hiki, huku thamani ya lesa ikizidi kushuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…