Viongozi wa Afrika ambao bado wanaishi hata baada ya kufa

Viongozi wa Afrika ambao bado wanaishi hata baada ya kufa

IKUNGURU IJIRU CHUKU

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2021
Posts
484
Reaction score
545
1:Patrice Lumumba,
Julai 2, 1925 katika ardhi ya Congo alizaliwa mtoto wa kiume katika viuno vya Mzee François Tolenga Otetshima na tumbo la Bi Julienne Wamato Lomendja, akaitwa jina lake Elias Okit’ Asombo yaani Mrithi wa Aliyelaaniwa.

2: Kwame Nkrumah,
Aliye ifanya Ghana ikawa nchi ya chama kimoja, yeye akawa life president, jeshi likampindua,
akakimbilia Guinea, Ayi Kwei Armah akaandika, THE BEUTYFUL ONES ARE NOT YET BORN kuitangazia Dunia serikali ya Kwame ilikuwa corrupt, kitabu kikafundishw sekondari na vyuoni, ndoto za Kwame zikakwama, shetani wa Afrika akazaliwa upya, sasa mabeberu wanakula sisi
tunaondoa vyombo!.

3-Julius Nyerere
April, 13, 1922, alizaliwa Julius Kambarage Nyerere katika familia ya kichifu, akasoma mpaka Ulaya, akapata ajira yenye mshahara mnono, akaiacha na kwenda kupigania Uhuru, Tanganyika tukawa huru, lakini akasema, "Uhuru wetu hauwezi kuwa na maana kama wenzetu bado wanatawaliwa",

4:-Nelson Mandela,
Makaburu walimtenga Mandela na upendo wa familia yake kwa miaka 27, akazikosa zile sauti nzuri za watoto wake zikiita baba, dada mchokozi, akaimis ile sauti ya mke wake Winnie ikiita,"chakula tayari honey." Alipotoka jela aliwasamehe wote isipokuwa mke wake kwa sababu vitu vya kusamehe si mapenzi! Eti, alichepuka.Loh! Mandelaaaa!

5:-Samora Machel,
Ukitaja jina la Samora Machel wazelendo wote tunagonga cheers, washenzi wananuna kwa sababu wanajua alivyowakaba, wakaishia kumtungua kwenye ndege na kumuua, mkewe akaomboleza kwa kuvaa nguo nyeusi kwa miaka mitano mfululizo. Ndoa zilikuwa zamani bwaba, siku hizi kama siti ya daladala, ukishuka wenzako wanakaa. Loh!

6: Muammar Gaddafi,
"Vya bure huondoa akili," ni methali ya waha wa Kigoma inayoelezea yaliyomkuta Muammari Gaddafi wa Libya na watu wake aliowapa kila kitu, halafu wakamuua kama kibaka na kumzika kusikojulikana, wafrika tukalia kumpoteza masiah wa Afrika, mabeberu wakashangilia kumpoteza mfadhili wa magaidi duniani. Walimuita "mad dog" kwa sababu ya gwaride alilowachezesha kwa miaka arobaini ya utawala wake. Aliapa kuwatafuna popote walikojificha akaja kutafunwa na wale aliowalisha na kusaza.

7:-Robert Mugabe
Ukisikia watu wanasema tuko nyuma yako 'be careful' maana ukigeuka unaweza usiwakute. Hii nimeiona 'live' kwa Robert Mugabe pale alipojitoa muhanga kuwakwida mabeberu kwa maslahi ya Afrika, wakaumia wananchi wake kwa vikwazo vya uchumi na diplomasia, viongozi wa Afrika wakamtelekeza, leo hii amekufa viongozi wanashindana kumsifia Mugabe kwa mbwembwe na mikogo kwa sababu marehemu hatukanwi. Haya ndiyo maajabu makuu ya viongozi wa Afrika!

8:-Jomo Kenyatta
Jomo Kenyatta alizaliwa, akakua, akapiga kazi kwa bidii na maarifa akaacha historia ndefu iliyotukuka, leo uzao wake unatafuna vya wenye meno. Hakuuacha historia fupi kama ya wale wazee waliozaliwa, wakakua, wakazura kwa bidii, wakafa na kuacha historia ndefu ya ufukara, leo uzao wao ndo hao wanaopiga mbizi kwenda kuzengea maishaa huko Ulaya na Marekani. Hawa ukiwaambia maisha yako Afrika ni sawa na kumwambia mbwa asali ni tamu kuliko mifupa wakakuelewa!

9:-Abeid Karume
Mwaka alfu mia kenda na tano, alizaliwa Abeid Amani Karume kuwakomboa wanyonge kutoka kwenye mikono katili ya Sultan aliyewatumikisha kwa jasho na damu tangu enzi na enzi, kwa jina la Karume wanyonge wakavua unyonge wao na kukavaa Uzanzibar, wakatibiwa pamoja, wakasoma pamoja, wakaishi pamoja, wakaabudu pamoja, wakaoana pamoja, wakajenga uchumi wao pamoja, Zanzibar maisha yakapata maana, dunia ikashuhudia ukarimu wa Karume kwa watu wake, halafu wale aliokula na kunywa nao wakachagua kumuua Karume kwa risasi nane za moto sawa na miaka nane ya utawala wake, damu ya Rais ikamwagika ardhini, Zanzibar ikaingia kwenye rekodi chafu Dunia, wahenga wakasema, ‘Ama kweli, kikulacho ki nguoni mwako!’

10:-Gamal Nasser
Gamal Abdel Nasser aliongoza mapinduzi ya 1952 yaliyomng'oa madarakani Mfalme Faruk I na kumuweka Jenerali Mohamed Naguib, wakapishana kiitikadi akampindua na kukalia kiti mwenyewe kupambana na Israel badala ya kuijenga Misri na Afrika kama alivyotuamisha kipindi cha mapinduzi, mwaka 70 akafa kifo cha ghafla na kuicha Misri njia panda, wa biblia wakasema alijichanganya kuligusa taifa teule la Mungu maana imeandikwa ukiwagusa utaangamia, ukiwabariki utabarikiwa ameeenii!

11:-Thomas Sankara
Disemba 12, 1949 Mzee Joseph Sankara na Bi Marguerite Kinda wa Bukina Faso, walibarikiwa mtoto wa kiume, wakamuita jina lake Isidore Noel Thomas yaani Zawadi ya Krismas, Thomas akawa zawadi ya Waafrika wote, tukamuita Che Guevara wa Afrika, Thomas akatawala Bukina Faso kwa fikra za “Mtegemea vya Nduguye Hufa Maskini,” watu wakaachana na fikra tegemezi, wakaingia shambani, jembe likapigwa, ardhi ikaitika, maskini wakavuna chakula, wakala na kusaza na kingine wakauza nje, maskini wakajifunza kitu,
 
7: Shetani Umemsahau anaeweza kumpa wasifu kiongozi huyu ,aafu huyu kanisani msikitini huwepo ,ukiamka tu anakupa mikakati.
 
Acha uwongo...wa kwetu je huyu wa juzi?
 
6:-Robert Mugabe
Ukisikia watu wanasema tuko nyuma yako 'be careful' maana ukigeuka unaweza usiwakute. Hii nimeiona 'live' kwa Robert Mugabe pale alipojitoa muhanga kuwakwida mabeberu kwa maslahi ya Afrika, wakaumia wananchi wake kwa vikwazo vya uchumi na diplomasia, viongozi wa Afrika
wakamtelekeza, leo hii amekufa viongozi wanashindana kumsifia Mugabe kwa mbwembwe na mikogo kwa sababu marehemu hatukanwi. Haya ndiyo maajabu makuu ya viongozi wa Afrika!

7:-Jomo Kenyatta
Jomo Kenyatta alizaliwa, akakua, akapiga kazi kwa bidii na maarifa akaacha historia ndefu iliyotukuka, leo uzao wake unatafuna vya wenye meno. Hakuuacha historia fupi kama ya
wale wazee waliozaliwa, wakakua, wakazura kwa bidii, wakafa na kuacha historia ndefu ya ufukara, leo uzao wao ndo hao wanaopiga mbizi kwenda kuzengea maishaa huko Ulaya na Marekani. Hawa ukiwaambia maisha yako Afrika ni sawa na kumwambia mbwa asali ni tamu kuliko mifupa
wakakuelewa!

8:-Abeid Karume
Mwaka alfu mia kenda na tano, alizaliwa Abeid Amani Karume kuwakomboa wanyonge kutoka kwenye mikono katili ya Sultan aliyewatumikisha kwa jasho na damu tangu enzi na enzi, kwa jina la Karume wanyonge wakavua unyonge wao na kukavaa Uzanzibar, wakatibiwa pamoja, wakasoma
pamoja, wakaishi pamoja, wakaabudu pamoja, wakaoana pamoja, wakajenga uchumi wao pamoja, Zanzibar maisha yakapata maana, dunia ikashuhudia ukarimu wa Karume kwa watu wake, halafu wale aliokula na kunywa nao wakachagua kumuua Karume kwa risasi nane za moto sawa na miaka nane ya utawala wake, damu ya Rais ikamwagika ardhini, Zanzibar ikaingia kwenye rekodi chafu Dunia, wahenga wakasema, ‘Ama kweli, kikulacho ki nguoni mwako!’

8:-Gamal Nasser
Gamal Abdel Nasser aliongoza mapinduzi ya 1952 yaliyomng'oa madarakani Mfalme Faruk I na kumuweka Jenerali Mohamed Naguib, wakapishana kiitikadi akampindua na kukalia kiti mwenyewe kupambana na Israel badala ya kuijenga Misri na Afrika kama alivyotuamisha kipindi cha mapinduzi, mwaka 70 akafa kifo cha ghafla na kuicha Misri njia panda, wa biblia wakasema alijichanganya kuligusa taifa teule la Mungu maana imeandikwa ukiwagusa utaangamia, ukiwabariki utabarikiwa ameeenii!

9:-Thomas Sankara
Disemba 12, 1949 Mzee Joseph Sankara na Bi Marguerite Kinda wa Bukina Faso, walibarikiwa mtoto wa kiume, wakamuita jina lake Isidore Noel Thomas yaani Zawadi ya Krismas, Thomas akawa zawadi ya Waafrika wote, tukamuita Che Guevara wa Afrika, Thomas akatawala Bukina Faso kwa
fikra za “Mtegemea vya Nduguye Hufa Maskini,” watu wakaachana na fikra tegemezi, wakaingia shambani, jembe likapigwa, ardhi ikaitika, maskini wakavuna chakula, wakala na kusaza na kingine wakauza nje, maskini wakajifunza kitu.
 
Back
Top Bottom