Viongozi wa CHADEMA walioko gerezani waachiwe mara moja bila masharti

Mkuu ulichosema ni kweli. Lakini mbona Lissu katolea mifano ya kina Mandela?

Hapa pia nadhani kuna shida kwasababu siyo wao waliomuuwa Akwilina. Pia wengine wengi wamekuwa wakiteseka humo ndani kabla hata kina Mbowe hawajitiwa hatiani. Hata yeye mwenyewe alipokaa huko wakati ule alipofungwa alizungumzia hilo. Tundu Lissu amezungumzia hilo.
 
Jela tofauti na mahabusu kwanza kuingia ni kunyolewa kipara kisha kupangiwa gereza la kukaa na kufanyishwa kazi tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakiendelea kukaa gerezani, ni aibu kwa Taifa letu. Kesi yenyewe tayari washasema ni ya kisiasa! Hivyo wanaamini kuwa kina Mbowe ni wafungwa wa kisiasa.
 
Wakae tu kwani wao ni malaika ? Wangapi wapo gerezani wanatumikia vigungo vyao.....wafanye ujinga halafu watazamwe tu wao ni akina nani?

sent from toyota Allex
 

Utawala huu wa Yohana unaonekana dhulma nje nje na watu wanaendelea kuumia sasa kama kutakuwa na fursa yeyote ya kupunguzia watu machungu itumike haraka iwezekanavyo. Watawala wao hawaoni shida kuumiza mtu na hao viongozi wa chadema mwaka huu wataumizwa zaidi japo wamekuwa wakiumizwa toka 2015 na mamluki waliopokea ndio wanawaumiza zaidi, ukimuona Polepole manake ndio maamuzi ya chama chao na furaha wanayoonesha ndio mioyo yao inataka kuona wengine wanateseka.

Ebu chukulia kesi ya Mbowe kama yeye binafsi ni hasara ngapi wamempa hata kama ni tajiri basi watoto wake wameandaliwa kupata tabu, wamemfungia biashara na wanamtoza faini kubwa kinachofuatia amini nakwambia watamtoa roho. Usawa huu faini ya 70 Milioni laiti kama ningekuwa mimi ningechagua kubaki jela manake hela hiyo ni zaidi ya ndoto.
 
Wakae tu kwani wao ni malaika ? Wangapi wapo gerezani wanatumikia vigungo vyao.....wafanye ujinga halafu watazamwe tu wao ni akina nani?

sent from toyota Allex
Walifanya ujinga gani? Unafahamu nani aliyemuuwa Akwilina? Unafahamu kuwepo kwao gerezani ni doa zaidi kwa serikali hii?
 
Kwa maoni yangu, kadri viongozi wa chadema wnavyozidi kukaa gerezani, ndivyo ambavyo umaarufu wa ccm ndani na nje ya nchi unadidimia.
Kwa mtaji huu, kwanini basi wasingeendelea kubaki gerezani ili umaarufu wa CCM udidimie hadi kumalizika kabisa?.
Ushauri wangu kwa ccm, muwaachie huru viongozi wa chadema waendelee kutoa hoja zao kwa wananchi kwa uhuru kama katiba inavyosema. Na tume huru ni LAZIMA.
Naunga mkono hoja, katazo la mikutano ya siasa liondolewe, japo aliyezuia mikutano sio CCM ni rais wa JMT.

Hili la Tume, kuifanya iwe Shirikishi ni jambo linalohitaji lobbying, tusitumie maneno makali kama LAZIMA, blaza wangu yule hapendi kabisa kupangiwa, hivyo kulazimishwa ndio kabisa!.

Kama ni yeye aliyesema hasomeshi mtoto wa kike atakayepata ujauzito, lakini juzi kamtuma tarishi kupeleka barua ya kuibadili hiyo kauli kwa kubwa la mabeberu, hivyo hata mikutano ya siasa ataruhusu na Tume kuifanya Shirikishi.
P
 
Nashauri waendelee kukaa gerezani hadi pale watakapotolewa bila masharti yoyote kwasababu ni wafungwa wa kisiasa(Polisi ndo walimuuwa Akwilina)R.I.P

Katazo la mikutano ya kisiasa limewekwa na rais wa JMT ambaye pia mwenyekiti wa ccm(Kumbuka ccm wao wameendelea kubebwa mpaka na dola)

Tunahitaji tume huru. Kuwa shirikishi ni tokeo la kuwa huru.

Kuhusu tarishi aliyepelekwa, wamarekani wameshangazwa na matokeo ya kesi hii huku wakijiuliza “huyu tarishi si alikuwepo huku juzi tu”, wakashangazwa pengine aliyoyatamka tarishi kule ni tofauti kabisa na haya yanayoendelea huku.

Nyie ndiyo mnaochagua ni uhuru upi wa kutoa(mmechagua watoto waliopata mimba)

Akili nyingine bhana mnazijua nyie wenyewe.🤦🏾‍♂️
 
Nyie ndiyo mnaochagua ni uhuru upi wa kutoa(mmechagua watoto waliopata mimba)

Akili nyingine bhana mnazijua nyie wenyewe.🤦🏾‍♂️
Kwa vile fedha za WB zimezuiliwa kwa hoja ya mimba za mtoto wa kike, kuruhusiwa kuendelea na masomo baada ya kujifungua, hiyo ni sababu tosha ya serikali ku take action.

WB wakiweka shurti la mikutano iruhusiwe, tutaruhusu.
P
 
Kwa vile fedha za WB zimezuiliwa kwa hoja ya mimba za mtoto wa kike, kuruhusiwa kuendelea na masomo baada ya kujifungua, hiyo ni sababu tosha ya serikali ku take action.

WB wakiweka shurti la mikutano iruhusiwe, tutaruhusu.
P
Kumbe WB siyo mabeberu bali ni marekani tu “wanaoingilia sovereignty yetu”?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…