Viongozi wa dini waliokutana Rais Samia Wamemshauri kuifuta kesi ya Mbowe

Viongozi wa dini waliokutana Rais Samia Wamemshauri kuifuta kesi ya Mbowe

Viongozi walitakiwa kuongea mwanzo kabisa wa kesi.

Kwa sasa wananchi wana kiu ya kumsikiliza Freeman Mbowe akijitetea!

Huu ndio wakati Yesu alijaribiwa na shetani pale juu ya mlima.
Ni rahisi wao kutwambia Yesu atarudi lini kuliko kumshauri rais kuingilia mahakama
 
Nusrat Hanje aliachiwa kwa sheria gani ili. aje kukamilisha 'covid 19' ya genge la Halima Mdee na Ndugai.

Bwashee punguza mbege wakati wa kwaresma
Kesi ya Mbowe Kama ya Yesu. HERODE: Sioni kosa namwachia. WAYAHUDI: Ukimwachia wewe siyo RAFIKI yake Kaizari. Jaji anayesikiliza kesi ya Mbowe ana shinikizo tu la CCM ( Wayahudi).
 
Hivi ndivyo Mwananchi walivyoeleza kwenye tovuti yao jioni hii .

Hoja hiyo iliwasilishwa mbele ya Rais na Shehe Mkuu (BAKWATA) Mufti Aboubakar Zuberi
=======

VIONGOZI WA DINI: BUSARA ITUMIKE KUMALIZA KESI YA MBOWE

Viongozi hao wameomba Mamlaka husika kutumia busara na kuangalia namna ya kumaliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na wenzake

Wametoa rai hiyo leo Machi 2, 2022 walipokutana na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Ikulu Dar es Salaam. Katika Mkutano huo, Viongozi hao wa Dini mbalimbali pia wamependekeza kuwe na Mjadala mpana kuhusu Mfumo mpya wa Elimu utakaokidhi mahitaji ya sasa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbalimbali wa Dini mara baada ya Kikao chao kilichofanyika leo tarehe 02 Machi, 2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Hiyo picha wasiione watu wa mambo ya "gender"
 
Nasikia moja ya kilelezo cha utetezi wa mh. Mbowe ni mkataba wa yeye kukopeshwa shs 1,000,000/= na Urio = kumbe zile hela alizomtumia Urio alikuwa anapunguza deni
Umeambiwa na nani?Epuka kuandika upuuzi mbele ya watu waliostaarabika!
 
Viongozi walitakiwa kuongea mwanzo kabisa wa kesi.

Kwa sasa wananchi wana kiu ya kumsikiliza Freeman Mbowe akijitetea!

Huu ndio wakati Yesu alijaribiwa na shetani pale juu ya mlima.
Kma ni hivyo, basi ujue serikali imewatumia viongozi wa dini ili Mbowe akiachiwa ipate pa kusemea kwamba iliombwa na viongozi wa dini. Hapa Kuna ka mchezo kanachezwa kuiondolea aibu serikali.
 
Bibi ushungi anataka amfunge Mbowe basi
Anaweza akanawa mikono Kama Herode....Mchukueni ninyi mkamhukumu kwa Sheria yenu(Sheria ya Wayahudi/CCM ni kusulubu kwenye msalaba), Mbowe anaweza kusulubiwa kwa Sheria ya Kiyahudi (au CCM) Yaani uonevu bila ushahidi.
 
Mahakama ina kazi gani sasa kwa mujibu wa katiba ya JMT?

Hao viongozi wa dini wamelewa mvinyo!

Tofautisha viongozi wa dini na Zuberi:

IMG_20220303_122227_245.jpg
 
Ni utapiamlo wa akili kuamini kuwa Tanzania ina viongozi wa dini.

Huyu hapa ni hao unaodai kuwa ni viongozi wa dini akidai kuwa Magufuli ni mkubwa kuliko Mungu,Yesu na mtume Mohamad enzi za uhai wa Magufuli.
View attachment 2136477

Mkuu be fair, weka video yote inayoonyesha mwanzo hadi mwisho wa kauli hiyo ya huyo sheikh.

Hakuna shaka kuwa huyo sheikh ni chawa mkubwa wa viongozi wa serikali. Lakini hiyo kauli ni zaidi ya wendawazimu. Ni muhimu na lazima ithibitike mwanzo hadi mwisho wake.
 
Kichwa cha Habari WAMEMSHAURI

Habari halisi WAMEMWOMBA

Kwani ukisema Rais Ameombwa unaona kama utampa credit Rais?

mwisho: Mh Rais Alishasema; suala hili kwa kuwa lipo Mahakamani si busara kulisemea.

Tuwe na imani na Mahakama yetu na itatenda haki.

Kuombwa ni kama vile Mbowe ana makosa.
Kushauri Mbowe hana kosa ila Rais kwa kutumia mamlaka yake anaweza kutumia busara kuachana na kesi ya michongo,majaji wa michongo,waendesha mashtaka wa michongo,mashahidi wa michongo na hukumu za michongo.
 
03 March 2022

GUMZO KUBWA BAADA YA MBOWE KUTAJWA KTK MKUTANO BAINA YA RAIS NA VIONGOZI WA DINI

Askofu Bagonza afafanua mkutano wao na Rais Samia Hassan, nini walizungumza viongozi wa dini kuhusu kesi ya Mbowe:


 
Back
Top Bottom