Viongozi wa dini waliokutana Rais Samia Wamemshauri kuifuta kesi ya Mbowe

Viongozi wa dini waliokutana Rais Samia Wamemshauri kuifuta kesi ya Mbowe

Hawa Viongozi Macho Yao Wameiona Kesi moja tu Mahakamani? Mbona ipo mikesi mingi tu Wameifumbia Macho..!
Wajikite Kumtangaza Mungu , haya mambo Sijui futa Kesi Ya Sabaya ,Sijui futa Kesi Ya Mbowe Waachane nayo...!
Kama umekerwa kalia mkuki
 
Mnaacha kazi mliyonayo ya kuhubiri neno la Mungu na kuvuna wafanya dhambi na mnaingilia siasa.

Mnataka kulazimisha ionekane Mbowe alikuwa na hatia na ameonewa huruma?

Mahakama ni chombo huru, msilazimishe mkuu wa nchi kuingilia maamuzi yake.

Fanyeni kazi ya Mungu acheni siasa .
 
Kwa vile kesi za mashehe wa uamsho zimeshafutwa, ni busara na hiyo ya Mbowe ikafutwa kwa sababu hadi sasa, hakuna ushahidi wowote uliotolewa mahakamani unaoonyesha Mbowe alihusika kwa namna yoyote na mipango ya ugaidi.

Kusema Rais hawezi kuifuta hiyo kesi sio sawa maana atakayeifuta sio yeye bali ni DPP ambaye sheria inamruhusu afute kesi yoyote anapoona ushahidi uliopo hautoshelezi na kuendelea na kesi ni kupoteza tu fedha za wananchi.

Lazima nyie mnaotoa maoni ya kubeza na wengine mnaoropoka kwamba eti viongozi wa dini hawatakiwi kuingilia hiyo kesi mwelewe kwamba hiyo kesi ya Mbowe "imeichafua" sana Tanzania kimataifa. Mataifa mengi ya nje yamekuwa yanaifuatilia na kuona jinsi ushahidi unaotolewa ni wazi ni wa KUTUNGA TU.

Kuna baadhi yenu "mtaropoka" na kusema mataifa ya nje "wasituingilie" Mnapoenda kuwaomba misaada mbona hamuwaambii "msituingilie"?
 
Kichwa cha Habari WAMEMSHAURI

Habari halisi WAMEMWOMBA

Kwani ukisema Rais Ameombwa unaona kama utampa credit Rais?

mwisho: Mh Rais Alishasema; suala hili kwa kuwa lipo Mahakamani si busara kulisemea.

Tuwe na imani na Mahakama yetu na itatenda haki.
Wakuu naomba kuuliza kwenye picha ya kwanza nimeona Laigwanani mgongoni kushoto kwa Malasusa je anawakilisha dini gani
 
Kichwa cha Habari WAMEMSHAURI

Habari halisi WAMEMWOMBA...
Ni Rais huyohuyo aliyeufahamisha ulimwengu kupitia BBC kuhusu uhalifu na kukimbia nchi alioufanya Mbowe huku wenzake wakifikishwa mahakamani na kufungwa!

Sasa tushike lipi maana tulipotangaziwa kesi tayari ilikuwa mahakamani naye aliingilia mahakama kwa kusema Mbowe ni mhalifu.
 
Yule Sheikh aliyewasilisha hoja anaonekana ana uwezo mdogo sana wa fikra, la sivyo ni mchumia tumbo
 
Taarifa rasmi ya ikulu imesema hivyo. Kuna yafiatayo;
1. Samia amekosa jinsi ya kumuachia Mbowe kaona awatumie viongozi wa dini baada ya ile ya KIBARAKA (ZUBERI) ku backfire.
2. Mbinyo umekuwa mkubwa lakini Samia anaona aibu baada ya kuropoka BBC.
Crap…
 
Kwa vile kesi za mashehe wa uamsho zimeshafutwa, ni busara na hiyo ya Mbowe ikafutwa kwa sababu hadi sasa, hakuna ushahidi wowote uliotolewa mahakamani unaoonyesha Mbowe alihusika kwa namna yoyote na mipango ya ugaidi...
Mkuu uhamsho hakuna aliyepelekwa mahakamani, Mbowe yupo mahakamani kila siku na wenyewe wana "mashahidi" kibao.

Embu tutulie aanze kujitetea tujue ukweli uko wapi
 
Back
Top Bottom