Viongozi wa dini waliokutana Rais Samia Wamemshauri kuifuta kesi ya Mbowe

Viongozi wa dini waliokutana Rais Samia Wamemshauri kuifuta kesi ya Mbowe

Nawasiwasi lisu atakataa viongozi wa
Hivi ndivyo Mwananchi walivyoeleza kwenye tovuti yao jioni hii .

View attachment 2136460

=======

VIONGOZI WA DINI: BUSARA ITUMIKE KUMALIZA KESI YA MBOWE

Viongozi hao wameomba Mamlaka husika kutumia busara na kuangalia namna ya kumaliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na wenzake

Wametoa rai hiyo leo Machi 2, 2022 walipokutana na Rais wa Tanzania, Samia Suhulu Hassan Ikulu Dar es Salaam. Katika Mkutano huo, Viongozi hao wa Dini mbalimbali pia wamependekeza kuwe na Mjadala mpana kuhusu Mfumo mpya wa Elimu utakaokidhi mahitaji ya sasa

View attachment 2136462
 
Hawa Viongozi Macho Yao Wameiona Kesi moja tu Mahakamani? Mbona ipo mikesi mingi tu Wameifumbia Macho..!
Wajikite Kumtangaza Mungu , haya mambo Sijui futa Kesi Ya Sabaya ,Sijui futa Kesi Ya Mbowe Waachane nayo...!
Sabaya hawezi kufutiwa kesi. Yule ni jambazi na tulipiga kelele sana humu ila mlimuona ni shujaa wa taifa, sasa atanyea ndoo kwa miaka 30
 
Kichwa cha Habari WAMEMSHAURI

Habari halisi WAMEMWOMBA

Kwani ukisema Rais Ameombwa unaona kama utampa credit Rais?

mwisho: Mh Rais Alishasema; suala hili kwa kuwa lipo Mahakamani si busara kulisemea.

Tuwe na imani na Mahakama yetu na itatenda haki.
Mahakama Kutenda kazi inashirikiana DPP kwa hiyo hata DPP atatenda kazi
 
Hawa Viongozi Macho Yao Wameiona Kesi moja tu Mahakamani? Mbona ipo mikesi mingi tu Wameifumbia Macho..!
Wajikite Kumtangaza Mungu , haya mambo Sijui futa Kesi Ya Sabaya ,Sijui futa Kesi Ya Mbowe Waachane nayo...!
KESI za kuku ndio wahangaike nazo tumia Akili hata za jirani zako
 
Hawa Viongozi Macho Yao Wameiona Kesi moja tu Mahakamani? Mbona ipo mikesi mingi tu Wameifumbia Macho..!
Wajikite Kumtangaza Mungu , haya mambo Sijui futa Kesi Ya Sabaya ,Sijui futa Kesi Ya Mbowe Waachane nayo...!
Usiwapangie......
 
Mahakama ina kazi gani sasa kwa mujibu wa katiba ya JMT?

Hao viongozi wa dini wamelewa mvinyo!
Hapana hawajalewa mvinyo....

Bali ni namna nyingine ya wao kusema "MBOWE SI GAIDI" maana hata Rais Samia mwenyewe anajua hilo kuwa huyu bwana siyo gaidi...

Rais Samia alilikoroga mwenyewe na sasa anatumia njia ya mzunguko kulimaliza hili kwa kuwatumia hawa the called "vingozi wa dini" akidhani watu wazima wenye akili timamu hatuwezi kuelewa kilicho nyuma ya pazia....
 
Tuliyajua haya maana jaji ameshajichanganya kesi yenye kurasa zaidi ya elfu naaa aliitolea hukumu ndani ya dakika 5 tu
 
viongozi wa michongo hao hakuna lolote hapo
 
Unaonesha kuwa ujinga ni kipaji! Nikukumbushe kuwa Mahakama sio huru kama unavotaka kujiaminisha! Rais huteua Jaji Mkuu, Msajiri Mkuu, majaji WOTE wa mahakama ya Rufaa na Kuu! Rais anaweza hata kumsamehe mfungwa anayatumikia kifungo kilichoamriwa na mahakama!

Swali: Je zile kesi za mashehe wa uamsho na 147 za uhujumu uchumi zilizofutwa wa maelekezo ya mahakama alikuwa ameingilia uhuru muhimili mwingine??

Ujinga wako uko hapa: Mahakama sio inayomshitaki Mbowe na wenzie na wengine wowote. Kesi huwa ni au za jamhuri au watu binafsi dhidi ya wengine na hupelekwa kwa third party - mahakama!! Uamuzi alioombwa kuchukua Rais sio wa kumwambia Jaji aseme Mbowe hajatenda kosa. Rais amwambie mteule wake mwingine DPP “kutoendelea na shauri”!!! Rais anaombwa achukue maamuzi ndani wa mhimili wake - DPP yuko katika mhimili wa serikali.

Nchi hii itasonga siku kiwango cha ufikiri kitakuwa bora kuliko chako!!!
Ukinielewesha bila kutumia kebehi unapungukiwa nini pu.mbavu wewe au hujaona kuwa nimeuliza swali?
 
Back
Top Bottom