Viongozi wa kanisa Katoliki na kanisa la kristo nchini DRC wamekutana na kufanya mazungumzo na waasi wanamgambo wa AFC-M23

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
VIONGOZI wa Makanisa Katoliki Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (CENCO) pamoja na Kanisa la Kristo nchini humo (ECC), mapema leo Februari 12, 2025 wamekutana na kufanya mazungumzo na waasi wanamgambo wa AFC-M23 lengo likiwa ni kujadili udumishaji amani nchini humo.

Viongozi hao wamekutana na sehemu ya uongozi wa M23 katika Hoteli ya Serena mjini Goma ambako pamoja na mambo mengine wamewashukuru wanamgambo hao kwa kuendelea kudumisha amani katika mji huo walioutwaa hivi karibuni.

Wamesema kwa mara ya kwanza, Goma inafanya kazi saa 24 kwa siku, bila matukio ya wizi wa kutumia silaha au vurugu za aina yoyote tofauti na ilivyotarajiwa.

Vilevile kabla ya kikao hicho viongozi hao wanaelezwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa DRC Felix Tshisekedi.

Katika mwendelezo wa mzozo huo ambako serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inaishutumu Rwanda kufadhili moja kwa moja mashambuli hayo mapema leo imefunga anga yake kwa ndege zote za kiraia na za serikali zilizosajiliwa au kutoka Rwanda.
 
Yesi ni jambo zuri wao wenyewe kama wakongomani kukaa na kutafakari hatma ya nchi yao.Hapo ndiyo nafasi ya viongozi wa dini inapoonekana.hata hivyo jambo la kuwashukuru waasi kuleta amani goma si jambo jema kwa serikali. maana yake serikali imepuuzwa na kukubalika kwa jambo ambalo waasi wamelifanya.Isije ikawa ni mbinu nyingine ya kuwapa nguvu waasi hao kuendelea kuchukua na miji mingine
 
Hiyo dini Avenue huwa ina shida zake
 
Hakuna namna ya kuwapuuza M23, lazima wapewe heshima yao ya kiuongozi na kiutawala kwakuwa mamlaka zilizopo Kinshasa zimeshindwa kuleta utawala bora, utawala wa haki na maendeleo ya watu
 
M23 ndio suluhisho la hayo matatizo?
 
M23 ndio suluhisho la hayo matatizo?

Lt. Col Willy Ngoma - M23 tayari wameonesha uwezo wa kutawala
1739383603127.jpeg
 
Huu mgogoro hauleweki ni wao wakongo ndio wanaoujua ukweli
 
VIONGOZI wa Makanisa Katoliki Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (CENCO) pamoja na Kanisa la Kristo nchini humo (ECC), mapema leo Februari 12, 2025 wamekutana na kufanya mazungumzo na waasi wanamgambo wa AFC-M23 lengo likiwa ni kujadili udumishaji amani nchini humo.

Viongozi hao wamekutana na sehemu ya uongozi wa M23 katika Hoteli ya Serena mjini Goma ambako pamoja na mambo mengine wamewashukuru wanamgambo hao kwa kuendelea kudumisha amani katika mji huo walioutwaa hivi karibuni.

Wamesema kwa mara ya kwanza, Goma inafanya kazi saa 24 kwa siku, bila matukio ya wizi wa kutumia silaha au vurugu za aina yoyote tofauti na ilivyotarajiwa.

Vilevile kabla ya kikao hicho viongozi hao wanaelezwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa DRC Felix Tshisekedi.

Katika mwendelezo wa mzozo huo ambako serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inaishutumu Rwanda kufadhili moja kwa moja mashambuli hayo mapema leo imefunga anga yake kwa ndege zote za kiraia na za serikali zilizosajiliwa au kutoka Rwanda.
Wafanye yooote ila Congo ibaki moja hakuna taifa jipya.
 
Mstari wa mbele katika mapambano ya kijeshi ushindi kwa M23, Diplomasia ya Maridhiano SADC / EAC tarehe 08 February 2025 Dar es Salaam ushindi kwa M23, Upande wa Kiroho M23 wanakubalika mbele ya Maaskofu tarehe 12 February 2025 Goma Kivu Nord, Mahakamani (Mahakama ya Afrika) Arusha ushindi kwa M23 ...

View: https://m.youtube.com/watch?v=ODenv6_qMnE
 
Hapo kwenye kuutwaa mji wa goma sijaelewa vzr, uongozi wa mji wa Goma sasahivi uko kwenye mikono ya serikali ya Congo au m23?
 
Kwa jinsi M23 walivyoonyesha kuwa na nidhamu, wengi tulitegemea Goma itakuwa na amani, na hata itastawi chini ya M23. Nikistaafu nitaenda kuishi North Kivu, huko Masisi.
 
Kivu ipewe mamlaka ya kujitawala lakini uendelee kuwa chini ya DRC, kama ilivyo Zanzibar Kwa Tanzania, Hong Kong Kwa China au Scotland Kwa Uingereza.
 
Back
Top Bottom