Viongozi wa kiislamu wanaturudisha nyuma sana kwenye No reform No election



Nasaha zangu kwako ndugu yangu najua wewe ni Muislam na kwa Waislam wote watakaosoma hapa nikiwemo mimi, haifai kufanya uasi dhidi ya mtawala hata kama atakuwa dhalimu.

Tusijitoe kwenye twaa ya mtawala. Na tunatakiwa kumsikiliza na kumtii (katika yasiyo haramu) hata kama atakuwa ni dhalimu, muovu.

Na hata kama mtawala akiwa ni kafiri, ima kafiri wa asili au ;

karitadi (tunajikinga kwa Allah kutokana na ukafiri na ridda) na mtawala akawa ameonyesha kufru ya wazi kabisa yenye kumtoa katika Uislam na kukatimia masharti ya kumkufurisha (yapo kwa mujibu wa Shari'ah) na kukawa hakuna kizuizi chenye kuzuia asikufurishwe (kuna mambo akiwa nayo Muislam aliyefanya jambo la ukafiri wenye kumtoa katika Uislam hayo mambo akiwa nayo mtu huyo yanazuia asikufurishwe), hata masharti yakitimia na kukawa hakuna vizuizi na mtawala huyo akakufurishwa (na Wanachuoni wa Kiislam). Bado haitofaa kumtoa kwenye uongozi kama Waislam hawana nguvu au hata kama wana nguvu ila kufanya hivyo kutaleta madhara makubwa. Hivyo Waislam watapaswa kuwasikiliza Wanachuoni wao waliosimama katika Qur-aan na Sunnah juu ya Ufahamu wa Wema waliotangulia.

Huu ni Msingi madhubuti mno kwetu. Sio kwa sababu sisi ni machawa, au sisi tunajipendekeza kwa watawala, hapana, hivi ndivyo tulivyofundishwa na Mtume wetu (Swala na Salamu ziwe juu yake) na ndivyo walivyoelewa Salafus-Swaalih (Wema waliopita yaani Maswahaba (Radhi za Allah ziwe juu yao) Wanafunzi wao na Wanafunzi wa Wanafunzi wa Maswahaba (Allah Awarehemu wote)) na wote waliofuata njia yao hao Salaf wamesimama na hili.



Haifai kumsema mtawala mbele za watu. Ukitaka kumnasihi mtawala mnasihi kwa siri, mfano umekutana naye uso kwa uso mshike mkono kama ukipata nafasi hiyo umnasihi, au muandikie kwa siri, sio kumsema kwenye mitandao au majukwaa. Hili limekatazwa. Mnasihi kwa siri, akisikia basi ni kheri, asiposikia basi utakuwa umeutua mzigo wako na unapaswa kuwa na subra na unatakiwa kumsikiliza na kumtii

Na watawala Waislam wanaombewa Dua nzuri.

Mwisho, maandamano hayana nafasi katika Uislam.

Na kama mtawala ni dhalimu basi ni juu yetu kuwa na subra.

Hii haimaanishi tunaunga mkono dhulma ya mtawala au tunapenda maovu yake, la hasha. Tunachukia maovu na dhulma yafanywe na mtawala au raia, ila tunafuata Muongozo wa Mtume wetu (Swala na Salamu ziwe juu yake) wa kuwa na Subra kunako dhulma ya mtawala, na kutofanya uasi dhidi yake na kutomsema mtawala hadharani, pamoja na kumnasihi mtawala kwa siri ikipatikana fursa hiyo.

Kuna Hikma kubwa mno kwenye hili na huu ni Uzuri wa Uislam, Uislam sio Dini ya kujifanyia mambo hovyo hovyo, ni Dini ina Utaratibu wa hali ya juu kwenye kila kipengele cha maisha ya kila siku. Basi tu Waislam tuna mapungufu yetu, ila Dini yetu Imekamilika. Namshukuru Allah kwa Neema ya Uislam na Sunnah. Tukiishika hii Dini bila kuzua na tukaikamata vilivyo mambo yetu yatanyooka mno kwa Idhini ya Allah.


Tunamuomba Allah Atuongoze katika njia iliyonyooka, Aamiin.



Kazakh destroyer naomba uje utie neno kwenye huu uzi ndugu yangu.
 
Ibn Abbas reported: The Messenger of Allah, peace and blessings be upon him, said, β€œWhoever sees something from his ruler that he hates, let him be patient. Whoever secedes from the community by as much as a handspan and dies will have died a death of ignorance.”

Source: SΜ£ahΜ£iΜ„hΜ£ al-BukhaΜ„riΜ„ 7054, SΜ£ahΜ£iΜ„hΜ£ Muslim 1849
 
Hudhayfah ibn al-Yaman reported: I asked, β€œO Messenger of Allah, we were living in an evil time and Allah brought us good in which we live now. Will there be evil after this good?” The Messenger of Allah, peace and blessings be upon him, said, β€œYes.” I said, β€œAnd any good after this evil?” The Prophet said, β€œYes.” I said, β€œAnd any evil after this good?” The Prophet said, β€œYes.” I said, β€œHow will it be?” The Prophet said, β€œAfter me, leaders will come who do not follow my guidance or my Sunnah. Some of their men will have the hearts of devils in a human body.” I said, β€œO Messenger of Allah, what should I do if I live to see that time?” The Prophet said, β€œYou should listen and obey the ruler, even if he strikes your back and takes your wealth, even still listen and obey.”

Source: SΜ£ahΜ£iΜ„hΜ£ Muslim 1847
 
The Messenger of Allah, peace and blessings be upon him, said, β€œWhoever intends to advise one with authority, he should not do so publicly. Rather, he should take him by the hand and advise him in private. If he accepts the advice, all is well. If he does not accept it, he has fulfilled his duty.” Source: Musnad AαΈ₯mad 14909 Grade: Sahih (authentic) according to Al-Albani
 
Umm Salama (wife of the Holy Prophet) that he said: Leaders will be appointed over you, and you will find them doing good as well as bad deeds. One who hates their bad deeds is absolved from blame. One who disapproves of their bad deeds is (also) safe (so far as Divine wrath is concerned). But one who approves of their bad deeds and imitates them (is doomed). People asked: Messenger of Allah, shouldn't we FIGHT against them? He replied: No, as long as they say their prayer. "Hating and disapproving" refers to liking and disliking from the heart - Sahih Muslim 1854.
 
Simak who said: Ash'ath b. Qais pulled him (Salama b. Yazid) when the Messenger of Allah (ο·Ί) said: "Listen to them (leaders) and obey them, for on them shall be the burden of what they do and on you shall be the burden of what you do." - Sahih Muslim 1846
 
Abu Dharr who said: "My friend (i. e. the Holy Prophet) advised me to listen (to the man in position of authority) and obey (him) even if he were a slave maimed (and disabled)." - Sahih Muslim 1837
 
Messenger of Allah (ο·Ί) said: "It is obligatory for you to listen to the ruler and obey him in adversity and prosperity, in pleasure and displeasure, and even when another person is given preference over you.” - Sahih Muslim 1836
 
It has been narrated on the authority of Abu Huraira that the Holy prophet (ο·Ί) said: "Whoso obeys me obeys God, and whoso disobeys me disobeys God. Whoso obeys the leader obeys me, and whoso disobeys the leader disobeys me." - Sahih Muslim 1835
 
Messenger of Allah (ο·Ί) said: The best of your rulers are those whom you love and who love you, who invoke God's blessings upon you and you invoke His blessings upon them. And the worst of your rulers are those whom you hate and who hate you and whom you curse and who curse you. It was asked (by those present): Shouldn't we overthrow them with the help of the sword? He said: No, as long as they establish prayer among you. If you then find anything detestable in them. You should hate their administration, but do not withdraw yourselves from their obedience. - Sahih Muslim 1855
 
Naomba elimu huru kuhusu mahakama ya Qadhw
 
Nashukuru kwa kuniita ustadh, japo umetosheleza ila niseme tu kuwa itikadi ya kiislamu na itikadi ya utatu mtakatifu ni vitu mbali mbingu na ardhi, na ndio maana tunasisitizana kusoma kila siku, sisi waislamu ni haramu kwetu kuhamasishana uasi na kufanya maandamano na fujo, kwani kwenye hilo kuna madhara makubwa sana na madhara yenyewe yanarudi kwa watu wengi sio wale waliofanya uasi peke yao.

Hivyo hao viongozi wa kanisa waendelee kuhubiri no reforms no election kwani wao hawana muongozo kutoka kwa allah unaowaongoza kwenye kila kitu hata mambo ya siasa na utawala, allah ndiye mjuzi zaidi.

Allah akubariki ndugu yangu na akuzidishie elimu na maarifa Baljurashi
 


Allahumma Aamiin, na wewe pia ndugu yangu, Allah Akubariki na Akuzidishie Elimu na Maarifa
 
Chai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…