Sitaki kukubaliana wala kupingana na wewe, Watanzania inatupasa tujitathmini sana kwanza tusiamini sana kama Chama cha siasa ndiyo mkombozi wa matatizo yetu, bado tupo kwenye utumwa wa kuamini Samaki mmoja akioza basi wote wameoza. vyama vyote vya Siasa havina tofauti maana viongozi wake ni wanaadam wenye miili na fikra zinazolingana. sitaki kuamini kwamba CCM ni mbaya moja kwa moja ila kuna watu ndani ya CCM ambao wanaitia doa ionekane ni mbaya, hivyohivyo kwa Chadema, ATC Nk. Wanasiasa hawa usione wanalumbana na kutoleana maneno mabaya mengine hata tukadhani ni kutishiana maisha, hawa wanatuzubaisha tu, wakiwa chemba wote wanaongea lugha moja matokeo yake Wananchi ndiyo tunayumbishwa tunakosa msimamo wakati wao maisha yanaendelea kuwanyookea (Tukumbuke kwamba Vyama na wanasiasa, sisi Wananchi ndiyo Mtaji wao na ndiyo tumewaweka hapo walipo).
Kwahiyo katika hivi vyama tariban vyote vinakuwa na sera na mitizamo mizuri sana lakini ndani ya hivyo vyama ndiyo kuna vivuruge! Unaweza kuta ndani ya CCM watu wanaoifanya ionekane ni ya ovyo hawazidi 20 lakini humo humo kuna wazalendo waliopitiliza! hivyo ushauri wangu ni Wananchi kujitafakari. kutafuta njia ya kudeal na hawa wachumia tumbo kuliko kutoa hizo lawama na kuonesha moja kwa moja kukata tamaa kwa kulalamikia chama moja kwa moja wakati hivi vyama ni sisi Wananchi ndiyo tumeviweka.