Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Kuna watu wanajifanya wanaipenda Simba lakini hadi hawajachangia hata sumni halafu wao ndio wanajiona mastaa wa kuisemea Simba, ukiwaona mitaani ama uwanjani wanajifanya wao ndio Simba kweli kweli lakini kwenye kuchangia timu wako mbaali.
Timu yetu imewasilisha hoja ya kuchangia adhabu iliyotolewa na Caf kwa madai tulishiriki kufanya fujo kwenye mchezo vs Csxfien ya Tunisia na tumetakiwa kulipa dola efu 40,000, hoja hii imetokana naa mashabiki wengi kuomba tulipe wenyewe kwa sababu sisi ndio tumekosa, yaani kimsingi sisi washabiki ndio tumeigharimu timu yetu hivyo lazima tulipe deni hilo sisi wenyewe, kumbuka hii ni adhabu ya pili kwa sababu adhabu ya kwanza tulikwishabebeshwa na serikali.
Sasa ombi langu kwa viongozi wa Simba, wekeni mkeka wa watu wote waliochangia ili tuangalie majina yetu huku kwenye matawi tujue nani katuchangia na nani hajachanga ili tuanze msako wa nyani na kuwajua wasaliti wa timu yetu ni nani, maana tutawauliza wenzetu ambao hawajachanga kwanini hawajachanga, kwanini hiyo hela ambayo walipanga kukatia tiketi jumapili wasichangie klabu yetu?
Wekeni mkeka huo viongozi.