TAMKO TAKATIFU NA TUKUKA
Waambieni hakuna Mchezaji mkubwa kuliko Simba SC yetu, Wameikuta na Wataiacha / Watatuachia. Huu Mtindo wa Kucheza Mpira kwa Kudekadeka, Kuringa na kama Wanalazimishwa uwe mwanzo na mwisho. Kama kuna Mchezaji anaona Simba SC siyo mahala pake aombe avunjiwe Mkataba wake upesi sana na atupishe. Kuanzia Mchezo weru wa Ligi Kuu ya NBC ya Jumatano au Alhamisi dhidi ya Coastal Union FC Uhuru Stadium ( Shamba la Bibi ) Saa 10 Kamili Jioni tunataka kuona mabadiliko makubwa kwa Wachezaji kujitoa kweli huku wakivuja Jasho na ikiwezekana watokwe hata na Damu kwa ajili ya Kuipambania Simba SC yetu. Wasipobadilika na wakiendelea na huu Upuuzi wao kiukweli Watatusamehe kwani wale ambao tunawamudu Kiubavu tutawapiga mno tu Viwanjani na hata Mitaani / Maskani tunakokaa na kukutana nao Kutwa na kwa wale ambao kutokana na Kukomaa Kwao na kuwa na Nguvu nyingi na Ubavu hatutoweza Kuwapiga tutakachofanya ni Kuwapopoa tu kwa Mawe au hata Kuvunja Vioo vya Magari yao ya Kifahari. Tumechoka kwakweli.
Wenu Mtoa Tamko Mkuu GENTAMYCINE.