Viongozi wa Tume ya Marekebisho ya BAKWATA wajiuzulu. Mufti Abubakar Zubeir adaiwa kuiendesha kama genge

Viongozi wa Tume ya Marekebisho ya BAKWATA wajiuzulu. Mufti Abubakar Zubeir adaiwa kuiendesha kama genge

Ex Spy

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2007
Posts
222
Reaction score
1,827
Mufti Abubakar Zubeir amedaiwa kuwa hajui namna ya kuendesha BAKWATA kiutawala na kwa hivyo tokea ameingia madarakani amekuwa akiendesha ofisi yake na BAKWATA kama duka lake au genge.

Endapo mamlaka ikiamua kufanya uchunguzi wa kina itaona kuwa hiyo ndio hali ilivyo ndani ya BAKWATA.

Kiuhalisia ukiangalia mifumo ya Bakwata japokuwa ni ya kizamani na haiendani na hali ilivyo sasa katika jamii ya waislamu lakini kama ingekuwa pia inafuatwa ipasavyo ingeweza kwa kiasi fulani kuleta mabadiliko mazuri ndani ya Bakwata.

Bakwata imekuwa inaendeshwa kwa matukio (Baraza la Eid, Msimu wa Hijja, Maulidi n.k), ili fedha zikusamywe kwa matumizi ya tukio,lakini zinaishia mifukoni mwa wachache.

MATATIZO YA BAKWATA

Tatizo kubwa la Bakwata, ni uongozi dhaifu wa Sheikh Abubakar Zubeir-Mufti wa Tanzania na Sheikh Mkuu.Amepoteza mwelekeo,na kujikuta yupo nje ya Madhumuni halisi ya Bakwata.

Viongozi waandamiziwa wa Bakwata kama vile Katibu Mkuu,Mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Bakwata Taifa,Mhasibu Mkuu,Mkurugenzi wa Hija, Mkurugenzi wa Elimu,na kadhalika; wanaujua vizuri udhaifu wa Mufti Abubakar Zubeir Kwani wamekuwa wakitumika kwa Mufti kumtafutia au kumkusanyia hela toka wa wafadhili mbalimbali. Pia wanajua jinsi ya kumfikisha Mufti Abubakar Zubeir afanye jambo lao.

Mambo haya, yamepelekea Tume kujiuzulu:


a12dd2fd-7f26-49de-970e-fc0c91d04d96.jpeg

3ac14122-3de4-4b38-9120-31f2867d2971.jpeg

df3719bc-6da6-4ff5-9a87-dd30122d308c.jpeg
 
Matatizo yote yatamalizwa iwapo WaIslam watakubali kuongozwa na Askofu Mkuu toka Catholic au Lutheran.

Jambo hili wala haliweza kuathiri Iman,bali kuongeza ufanisi na maadili ktk utendaji kazi.

Najua wapo watakaoshangaa na kuhoji uwezekano wa kuongozwa na Mgalatia lakini leo hii UK inaongozwa na Waziri Mkuu from India !.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Maboresho Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Issa Issa pamoja na wajumbe wanne wameng’atuka katika nyadhifa zao kutokana na kile walichoeleza ni ugumu wa kutekeleza majukumu yao.

Waliong’atuka ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Sheikh Issa Issa, wajumbe Mohamed Nyegi, Daudi Nasib, Idi Kamazima pamoja na Omari Igge.

Ikumbukwe tume hii ilizinduliwa Februari mwaka huu na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Ibn Zubeir kwa lengo la kufanyia kazi mambo sita ndani ya Bakwata, ikiwemo kuhakiki madeni na kushauri namna ya kulipwa.

Taarifa za kuachia ngazi kwa viongozi hao zimetolewa leo Jumapili April 30,2023 kupitia barua ya Mwenyekiti wa Tume hiyo Sheikh Issa kwenda kwa Mufti Sheikh Zubeir ikieleza kwamba kutokana na ugumu wanaoupitia katika kutekeleza majukumu yake ameamua kuachia nafasi hiyo.

“Dhumuni la barua hii ni kukufahamisha kuwa kutokana na haya yaliyojitokeza ndani ya Bakwata ya ugumu wa kutekeleza na kuifanya kazi ya maboresho kwa ufanisi ambayo naamini unayatarajia wewe binafsi na waislamu kwa ujumla, baada ya kutafakari kwa kina juu ya hali hii ambayo kwa hakika unaifahamu vizuri leo April 30, nimeamua kujiuzulu nafasi ya uenyekiti,”imeandikwa barua hiyo.

Mwenyekiti huyo aliambatanisha majina manne ya wajumbe wengine, ambao walimuarifu kwamba nao hawapo tayari kuendelea kutekeleza majukumu yao sababu kubwa ugumu wa kutekeleza majukumu waliyopewa.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Katibu wa Tume hiyo Omar Igge alithibitisha kuachia nafasi hiyo pamoja na viongozi wenzake.

Amesema katika hadidu za rejea, kazi waliyopewa kuifanya ni pamoja na uhakiki wa madeni, kufanyia uchunguzi mali za Bakwata zinazomilikiwa na watu wengine kinyume cha utaratibu na kuchukua hatua za kutatua,

“Pia kufanya tathmini ya changamoto za mifumo ya utawala inayoikabili Bakwata na kusahauri namna ya kufanya maboresho pamoja na kuibua na kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa Bakwata,”alisema.

Jambo la sita ambalo Tume hiyo ilipaswa kutekeleza ni pamoja na mambo mengine itakayoyaona yanafaa kufanyiwa kazi.

Kufuatia hatua ya viongozi hao kuachia nyadhifa zao, tume hiyo sasa itabakiwa na wajumbe wawili ambao ni Al haj Nuhu Mruma na Sheikh Qaasim Jeizan.

Fu-SQ4fWIAE5ugG.jpg

Fu-SRqHWAAAkmVo.jpg

Chanzo: Mwananchi
 
Nilishangaa walipomuomba rais mwanamke awasaidie kutatua wakati dini yao haitambu uongozi wa mwanamke
Tanzania sio Islamic State Kwa hiyo kuna vitu hata kama dini yako haitambui hauna budi kukubaliana navyo, sababu huna any other alternative.
 
Rais alisema matatizo ya Mali za bakwata yanaanzia bakwata.

Hiyo kazi ni ngumu sana sana, walitakiwa kuombewa Dua kwanza kwa mwaka mzima mfululizo.

Kulikuwa na issue ya nyumba za wakfu sehemu fulani, wazee wa kiislamu walijimilikisha nyumba hizo. Uongozi mpya ukaingia. Mpambano ukawa jinsi gani wawaondoe katika hizo nyumba. Wale wazee waliwapukutisha vijana kwa kuwauwa mmoja baada ya mwingine, walikuwa wanakufa vifo visivyoeleweka.

Sasa ndio upewe kazi hiyo kwa nchi nzima, utaiweza? Watu wenyewe kwa asili ni wabishi wabishi tu.

Hapo hujagusa visehemu ambavyo Alhad Mussa alikodisha na ndio vinamuweka mjini kwa wakati huu anatembelea rim
 
Hao wajumbe wawili waliobaki wanasubiri nini kuachia ngazi, au ni magwiji ngoma hiyo wataiweza? All in all dini gani hiyo inajiingiza kwenye migogoro ya mali yenyewe kwa yenyewe? Kama vipi wawaachie tu hao wazee hizo mali na wakatafute na kuanzisha zingine. Wafanye kama wametoa sadka na shukrani kwa hao wazee wao wa dini
 
Kazi ngumu sana mali na madeni yanatlrudi kwa uongozi ukiopita na wengine wapo kwenye uongozi mbali mbali ....Mali wameuziana wenyewe kwa wenyewe na matajiri ...wadhamini wakuu
 
Wameohopa kurongwa,mana waislamu kwa kuroga na kutupiana majini ndio kazi yao,nashauri bakwata iendelee kujikita zaidi kwenye kuuza vyeti vya ndoa na talaka,mana ndio kazi wanayoiweza vyema.
 
Walitakiwa wawajumishe baadhi ya wajumbe waislamu kutoka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama na wanasheria kwenye hiyo tume.
 
Sheikh Ponda atabaki kuwa mkweli daima kuhusu mali za umma wa waislam wa Tanzania.

Wanaumizwa sana na serikali haiwasaidii zaidi ya kuwatumia kisiasa
 
Walitakiwa wawajumishe baadhi ya wajumbe waislamu kutoka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama na wanasheria kwenye hiyo tume.

Labda wawaweke waganga, wachawi na wauguzi wa kimashetani, hiyo vita sio ya bunduki, ni ya ulonzj
 
Matatizo yote yatamalizwa iwapo WaIslam watakubali kuongozwa na Askofu Mkuu toka Catholic au Lutheran.

Jambo hili wala haliweza kuathiri Iman,bali kuongeza ufanisi na maadili ktk utendaji kazi.

Najua wapo watakaoshangaa na kuhoji uwezekano wa kuongozwa na Mgalatia lakini leo hii UK inaongozwa na Waziri Mkuu from India !.
Rekebisha waziri mkuu kutoka Tanzania sio India.Ungesema waziri mkuu Mtanzania mwenye asili ya Asia.
Hata wewe ni raia wa Tanzania mwenye asili ya Dodoma kwa Wagogoo
 
Back
Top Bottom