Hawa vijana wadogo wanachofanya ni upuuzi. Wazazi wao wasiwachekee. Mtoto wa kiongozi wa umma kupost kabeba maburungutu ya pesa nyumbani sio sawa. Inaleta maswali mengi sana hasa nyakati hizi za uchaguzi. Tunajua viongozi sio maskini ila hili la watoto wao kupost mali na pesa hovyohovyo lina athari kubwa kwa serikali iliyoko madarakani. Ni kama kuwapa agenda ya bure wapinzani ambao tayari walishapoteza mwelekeo.
Kuna mtu hata ugali dagaa hajapata siku nzima mara anaonyeshwa na shetani Mange toto la Kigogo limebeba maburungutu na kuambiwa ni za kulia bata. Kwa vyovyote vile itamletea msongo wa mawazo na kukata tamaa. Pongezi kwa watoto wote wa viongozi wanaojiheshimu wasiopost mali za wazazi wao kijinga.
Kwani hatimaye na wewe umetambua wanalamba mno hadi nje ya urefu wa kamba zao?