Viongozi wa vyama vya siasa, Serikali na Bunge acheni unafiki shule zote za Serikali ziwe English medium watoto wenu mbona wanasoma English Medium?

Viongozi wa vyama vya siasa, Serikali na Bunge acheni unafiki shule zote za Serikali ziwe English medium watoto wenu mbona wanasoma English Medium?

Hii itakua ngumu mno! watoto wetu watafeli mpaka basi

English medium ni mfumo mzuri sana nami pia niseme wazi mwanangu yupo huko anapiga zake ngeli

hii haitewezekana kwa sababu ya walimu wengi wanaofundisha kayumba English ni tatizo kubwa kwao, labda useme wote watimuliwe waajiriwe wengine nchi nzima wataofit na mfumo wa english media

Vyuo vya walimu pia hasa hivi vya certificate vibadilisho

Elimu bure hii ya kiswahili serikali inashindwa, itaweza vipi elimu kwa english media?

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah apo sasa ndo pagumu maana kweli Walimu wetu wengi Lugha shida, ila m binafsi natamani watoto wasome ngeli toka primary masomo yote.
Kiswahili Liwe somo kama la kujitegemea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani Serikali ilipoamua kuhama toka English.medium kuja swahili.medium walimu walitimuliwa wote? Na iliwezekanaje wakati vitabu vyote vya kufundishia vilikuwa English na vyuo vya walimu vilikuwa English?

Kwa Nini isiwezekane Sasa kubadili kutoka Swahili medium kuwa English medium wakati walimu wote wa diploma wa shule za msingi husoma diploma zao na digrii za elimu ya ualimu wa shule ya msingi kwa kiingereza?

Mbona shule za English medium walimu wanaofundisha Ni watanzania hao hao waliosoma vyuo hivi hivi vya ualimu vya Tanzania? Hazifundishwi na watu wa nje mbona?
Walimu wengi wanajua kutamka maneno ya kingereza lakin kuongea kifasaha shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimu wengi wanajua kutamka maneno ya kingereza lakin kuongea kifasaha shida

Sent using Jamii Forums mobile app
English medium ndio hao hao wanaofundisha waliosoma vyuo vyetu vya ualimu mbona watoto wanatoka wako fit tu.Shule zote za English medium walimu ni watanzania Tena visichana na vivulana vidogo tu vilivyomaliza vyuo vyetu ualimu vya Tanzania.English medium schools Wala hazifundishwi na vibibi na vibabu visivyosaidia enzi za ukoloni wa mwingereza au vilivyomaliza middle school au darasa la kumi la mkoloni mwingereza
 
Walimu wengi wanajua kutamka maneno ya kingereza lakin kuongea kifasaha shida

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenikumbusha Kuna babu mmoja nduguye na mwenye shule alimleyta huyo babu msstaafu atufundishe kiingereza yeye kutwa alikuwa akidai hatujui kiingereza eti kimejaa many common mistakes akatuletea kitabu chake Cha kizamani kimepauka hicho eti kila mtu ampe hela akatutolee photocopy wakati anatumia photocopy ya shule tukagoma.Kitabu chake hicho kilichozeeka na kupauka kilikuwa kinaitwa common mistakes in English mwandishi simkumbuki Lakini alikuwa na Jina la kigiriki Sijui fitikides sikumbuki vizuri
 
Wote vyama vya siasa kuanzia CCM na upinzani hakuna hata anayeongelea hili iwe bungeni au popote .Sababu watoto wao Wako English medium hawajali hao Wengine Loooooh!. Roho mbaya kabisaaa
Ungesema watanzania waliona uwezo wa kifedha kuwatujumu wanasiasa pekee hakutoshi.
 
Ukisema Mwalimu ndio rais mbovu kuwahi kutokea nchi hii watakutukana balaaa

Mijadala kama hii ni bora ungekuwa unapitia coments ili ujifunze kitu, kuliko kuandika usichokijua!

Historia usiyoijua ni 1964, kulitolea jeribio LA mapinduzi na walimpindua Mwalimu, kati ya makundi yaliyosemekana kushiriki, ni Wasomi, Wafanya biashara na Wanajeshi weusi.

Baada ya kuzima mapinduzi, mwalimu alishauriwa na makachero ya uingereza adhibiti hayo makundi, kwanza akabadili gia, alikuwa bepari akawa mjamaa toka 1966 baada ya kwenda China, mbili akabadiri lugha ya kufundishia 1967, kutoka english to Swahili ili kupunguza wanaojielewa a.k.a wasomi, tatu akatangaza azimio la Arusha ili kudhibiti wafanya biashara na kuwapora Mali zao etc!

Kaa pembeni ujue mambo sio unatumia usichokijua

Licha ya kuwa Mwalimu ndio nguzo kuu ya Umaskini na Ujinga Tanzania ana wafuasi ambao hawaelewi kitu kabisa. Sijui hata walilishwa nini na wazee wao.
 
Mijadala kama hii ni bora ungekuwa unapitia coments ili ujifunze kitu, kuliko kuandika usichokijua!

Historia usiyoijua ni 1964, kulitolea jeribio LA mapinduzi na walimpindua Mwalimu, kati ya makundi yaliyosemekana kushiriki, ni Wasomi, Wafanya biashara na Wanajeshi weusi.

Baada ya kuzima mapinduzi, mwalimu alishauriwa na makachero ya uingereza adhibiti hayo makundi, kwanza akabadili gia, alikuwa bepari akawa mjamaa toka 1966 baada ya kwenda China, mbili akabadiri lugha ya kufundishia 1967, kutoka english to Swahili ili kupunguza wanaojielewa a.k.a wasomi, tatu akatangaza azimio la Arusha ili kudhibiti wafanya biashara na kuwapora Mali zao etc!

Kaa pembeni ujue mambo sio unatumia usichokijua
Ulicho eleza ndicho alicho eleza sijui umekwama wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe Shwain Rudi kwenye hoja ya msingi. Issue ilikuwa ni english na exposure huko duniani. Ndio Mana nikauliza what is the role of english wakati Kuna inchi Zina exposure kubwa na English sio kipaumbele. Nimekutajia warusi na wachina Kama mfano tu. Not mentioning france, Germany etc.
Hapo issue ni uvivu wa fikra na vitendo hata mngejua lugha zote duniani. Shwain wewe [emoji1787][emoji23]
Ni upumbavu ulio kufikisha hapo hao ulio wataja wanapigana vikumbo kusomesha watoto wao kwenye shule za kiingereza. Ni kuulize swali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mala ya kwanza umeongea hoja zenye mashiko! Ungekuwa rafiki yangu wa kuaminika ningekupa chronological flow! Na ushahidi kuwa kwa upande mmoja kiswahili kimeliunganisha taifa lakini lengo la awali halikuwa zuri?!

Kama lengo la awali halikuwa jema, kiswahili ni moja ya 'laana' especially kwenye mfumo wa elimu!

Reference kama wewe ni mchunguzi, jua je ni lini Mwalimu alibadiri gia kutoka kuwa bepari mpaka mjamaa, 1966 while mapinduzi yalikuwa 1964, and Azimio 1967!

Curses kwa nchi hii ni 1. Azimio la Arusha, (kudhurumu Mali za watu) 2. Kiswahili 1967 ili kuudhoofisha mfumo wa elimu etc.

Yote hayo yalipangwa baada ya jaribio la mapinduzi 1964.
Moja ya baraka ambayo watz hatujaitumia ni kiswahili. Tunang'ang'ania kiingereza sababu tuna mawazo kikoloni kwenda kumfanyia kazi mzungu na bado tunawaza kuwa kujua kiingereza ndiyo usomi, hili bado halijatutoka.
 
mkombozi wa elimu yetu ni kutumia kiswahili hadi chuo kikuu. Tunajifunza sayansi na sanaa kwakiingereza ili iweje? Kiingereza kibaki kama lugha. Mtu mweusi hajisomi kabisa, Msumbiji wanaona kireno ndiyo safi, Congo wanaona kifaransa ndiyo safi, ila kiswahili hakifai.
 
English medium ndio hao hao wanaofundisha waliosoma vyuo vyetu vya ualimu mbona watoto wanatoka wako fit tu.Shule zote za English medium walimu ni watanzania Tena visichana na vivulana vidogo tu vilivyomaliza vyuo vyetu ualimu vya Tanzania.English medium schools Wala hazifundishwi na vibibi na vibabu visivyosaidia enzi za ukoloni wa mwingereza au vilivyomaliza middle school au darasa la kumi la mkoloni mwingereza
Nafikiri miundoombinu, ratio ya wanafunzi kwa mwalimu na uzuri mwingine wa hizo shule unaujua. Fikiria hiyo shule iwe inafundisha kwa kiswahili! kungekuwa hamna wanaopata B, wote A. Ufaulu ungezidi mbali hao wanaosoma kwa kiingereza.
 
Katika maisha kuna vitu unatakiwa uvifanye ukiwa kijana au mtoto huo kumri ukipita ndo basi tena, sasa kama taifa tulishachelewa kwa sasa haiwezekani ilitakiwa ifanyike wakati ule ambapo mtu alipokuwa akisimama kwenye ukumbi wa Nkrumah akiongea kuswahili anachekwa au kunyanganywa mike lkn leo hii ukiongea kizungu unanyanganywa mike au kama kuna tv inarusha live inakatisha matangazo, kwa hali hiyo unadhani inawezekana.
 
Wewe utakuwa mpiga dili mlizoea kupeleka watoto nje kusoma kwa kuwaibia Wanyonge.. Sasa Jemedari Dr JPM anawanyoosha mnalia lia hapa..
 
Mwenzako ameamua kuukacha upumbavu na kuamua kubaki tu kuwa mjinga wa lumumba,wewe bado umeamua kuukumbatia upumbavu,shenzy kabisa,yaani ma ccm hata mwenzao akitoa hoja ya maana yanahisi amekuwa chadema!! Maana haya ma KARLO MWILAPWA yanajijua kuwa hayanaga akili.
Akili kama hii ikiingia 2020 inabidi tulie kilio Cha kusaga meno kwa sababu tutaangamiza taifa letu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenena vyema. Serikali inajichanganya yenyewe. Kwanza kama mfumo wetu wa elimu ni kiswahili basi ilipaswa kuwa hivyo kuanzia chekechea hadi chuo kikuu. Kusiwepo na shule yoyote english medium Tz isipokuwa international schools ambazo zinakuwa highly regulated na wanasoma foregners tu sio wazawa na lazima wawe na pasipoti za kigeni.

Shule za binafsi ziendelee kuruhusiwa lkn lugha ya kufundishia ibaki kiswahili na english libaki kuwa somo. Hapo nina hakika elimu itasimamiwa ipasavyo.

Kwa mfumo wa sasa, watoto wa viongozi wote, watoto wa wafanyabiashara wenye pesa, watoto wa wafanyakazi wenye kipato kikubwa wanasoma english medium schools lkn watoto wa watanzania masikini wanasoma shule za kiswahili, tunajenga tabaka baina ya wananchi walionacho na wasionacho. Hali hii ni mbaya sana kwa umoja wa kitaifa, tunasema sisi ni wamoja lkn ukweli ni kuwa sio wamoja. Kwa sasa nina hakika hakuna kiongozi hata mmoja ambaye wanaye wanasoma st kayumba! Hawa ndio wanatuongoza,unategemea nini?

Iwapo serikali haiwezi kusimamia mfumo nilioutaja hapo juu basi suluhisho ni moja tu, shule zote Tanzania tubadili lugha ya kufundishia kuwa kiingereza kuanzia shule ya msingi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom