Viongozi wa vyama vya siasa, Serikali na Bunge acheni unafiki shule zote za Serikali ziwe English medium watoto wenu mbona wanasoma English Medium?

Dah apo sasa ndo pagumu maana kweli Walimu wetu wengi Lugha shida, ila m binafsi natamani watoto wasome ngeli toka primary masomo yote.
Kiswahili Liwe somo kama la kujitegemea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimu wengi wanajua kutamka maneno ya kingereza lakin kuongea kifasaha shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimu wengi wanajua kutamka maneno ya kingereza lakin kuongea kifasaha shida

Sent using Jamii Forums mobile app
English medium ndio hao hao wanaofundisha waliosoma vyuo vyetu vya ualimu mbona watoto wanatoka wako fit tu.Shule zote za English medium walimu ni watanzania Tena visichana na vivulana vidogo tu vilivyomaliza vyuo vyetu ualimu vya Tanzania.English medium schools Wala hazifundishwi na vibibi na vibabu visivyosaidia enzi za ukoloni wa mwingereza au vilivyomaliza middle school au darasa la kumi la mkoloni mwingereza
 
Walimu wengi wanajua kutamka maneno ya kingereza lakin kuongea kifasaha shida

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenikumbusha Kuna babu mmoja nduguye na mwenye shule alimleyta huyo babu msstaafu atufundishe kiingereza yeye kutwa alikuwa akidai hatujui kiingereza eti kimejaa many common mistakes akatuletea kitabu chake Cha kizamani kimepauka hicho eti kila mtu ampe hela akatutolee photocopy wakati anatumia photocopy ya shule tukagoma.Kitabu chake hicho kilichozeeka na kupauka kilikuwa kinaitwa common mistakes in English mwandishi simkumbuki Lakini alikuwa na Jina la kigiriki Sijui fitikides sikumbuki vizuri
 
Wote vyama vya siasa kuanzia CCM na upinzani hakuna hata anayeongelea hili iwe bungeni au popote .Sababu watoto wao Wako English medium hawajali hao Wengine Loooooh!. Roho mbaya kabisaaa
Ungesema watanzania waliona uwezo wa kifedha kuwatujumu wanasiasa pekee hakutoshi.
 
Ukisema Mwalimu ndio rais mbovu kuwahi kutokea nchi hii watakutukana balaaa


Licha ya kuwa Mwalimu ndio nguzo kuu ya Umaskini na Ujinga Tanzania ana wafuasi ambao hawaelewi kitu kabisa. Sijui hata walilishwa nini na wazee wao.
 
Ulicho eleza ndicho alicho eleza sijui umekwama wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni upumbavu ulio kufikisha hapo hao ulio wataja wanapigana vikumbo kusomesha watoto wao kwenye shule za kiingereza. Ni kuulize swali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moja ya baraka ambayo watz hatujaitumia ni kiswahili. Tunang'ang'ania kiingereza sababu tuna mawazo kikoloni kwenda kumfanyia kazi mzungu na bado tunawaza kuwa kujua kiingereza ndiyo usomi, hili bado halijatutoka.
 
mkombozi wa elimu yetu ni kutumia kiswahili hadi chuo kikuu. Tunajifunza sayansi na sanaa kwakiingereza ili iweje? Kiingereza kibaki kama lugha. Mtu mweusi hajisomi kabisa, Msumbiji wanaona kireno ndiyo safi, Congo wanaona kifaransa ndiyo safi, ila kiswahili hakifai.
 
Nafikiri miundoombinu, ratio ya wanafunzi kwa mwalimu na uzuri mwingine wa hizo shule unaujua. Fikiria hiyo shule iwe inafundisha kwa kiswahili! kungekuwa hamna wanaopata B, wote A. Ufaulu ungezidi mbali hao wanaosoma kwa kiingereza.
 
Katika maisha kuna vitu unatakiwa uvifanye ukiwa kijana au mtoto huo kumri ukipita ndo basi tena, sasa kama taifa tulishachelewa kwa sasa haiwezekani ilitakiwa ifanyike wakati ule ambapo mtu alipokuwa akisimama kwenye ukumbi wa Nkrumah akiongea kuswahili anachekwa au kunyanganywa mike lkn leo hii ukiongea kizungu unanyanganywa mike au kama kuna tv inarusha live inakatisha matangazo, kwa hali hiyo unadhani inawezekana.
 
Wewe utakuwa mpiga dili mlizoea kupeleka watoto nje kusoma kwa kuwaibia Wanyonge.. Sasa Jemedari Dr JPM anawanyoosha mnalia lia hapa..
 
Mwenzako ameamua kuukacha upumbavu na kuamua kubaki tu kuwa mjinga wa lumumba,wewe bado umeamua kuukumbatia upumbavu,shenzy kabisa,yaani ma ccm hata mwenzao akitoa hoja ya maana yanahisi amekuwa chadema!! Maana haya ma KARLO MWILAPWA yanajijua kuwa hayanaga akili.
Akili kama hii ikiingia 2020 inabidi tulie kilio Cha kusaga meno kwa sababu tutaangamiza taifa letu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenena vyema. Serikali inajichanganya yenyewe. Kwanza kama mfumo wetu wa elimu ni kiswahili basi ilipaswa kuwa hivyo kuanzia chekechea hadi chuo kikuu. Kusiwepo na shule yoyote english medium Tz isipokuwa international schools ambazo zinakuwa highly regulated na wanasoma foregners tu sio wazawa na lazima wawe na pasipoti za kigeni.

Shule za binafsi ziendelee kuruhusiwa lkn lugha ya kufundishia ibaki kiswahili na english libaki kuwa somo. Hapo nina hakika elimu itasimamiwa ipasavyo.

Kwa mfumo wa sasa, watoto wa viongozi wote, watoto wa wafanyabiashara wenye pesa, watoto wa wafanyakazi wenye kipato kikubwa wanasoma english medium schools lkn watoto wa watanzania masikini wanasoma shule za kiswahili, tunajenga tabaka baina ya wananchi walionacho na wasionacho. Hali hii ni mbaya sana kwa umoja wa kitaifa, tunasema sisi ni wamoja lkn ukweli ni kuwa sio wamoja. Kwa sasa nina hakika hakuna kiongozi hata mmoja ambaye wanaye wanasoma st kayumba! Hawa ndio wanatuongoza,unategemea nini?

Iwapo serikali haiwezi kusimamia mfumo nilioutaja hapo juu basi suluhisho ni moja tu, shule zote Tanzania tubadili lugha ya kufundishia kuwa kiingereza kuanzia shule ya msingi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…