Viongozi wa Yanga Feitoto ameshageuka adui yenu, achacheni naye

Yanga wana roho mbaya sana kama wachawi
 
Kama mkataba unamruhusu wamwache aende,Kama sio lazima auzwe mpira Ni biashara.
Kucheka kwa dharau au kwa mashaka hakujalishi .viongozi mwacheni Kama mkataba.muuzeni Kama mkataba uko upande wa Yanga.Na tena mwacheni na milioni 112 zake Kama mkataba uko upande wake msilazimishe mkashindwa kwa aibu
 
Sheria za FIFA zipo wazi mchezaji mwenye mkataba hawezi vunja mkataba kati kati ya msimu bila kuzungumza na club yake
 
Sheria za FIFA zipo wazi mchezaji mwenye mkataba hawezi vunja mkataba kati kati ya msimu bila kuzungumza na club yake
Acha uongo hakuna sheria kama hiyo alafu unacho takiwa kujua ni kuwa mikataba huwa haifanani ww usidhani vipengere vya mkataba wa chama ni sawa na vipengere vya mkataba wa kanouti au kibu.
 
Yanga ipi unayoizungumzia?
Hii ambayo kila kesi yenyewe huwa ni kunyukwa tu?
Au kuna Yanga nyingine?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Aziz Ki ameshamfunika Feikubwa sababu jamaa anafunga, ni play maker na anatoa assists
Aziz k ni mchezaji mkubwa huwezi kumfananisha na Fei, mechi za kimataifa sina wasiwasi kabisa na Aziz ki. Fei ni mchezaji wa mechi za ndani tu.
 
Nani asiyejua uhuni wa Yanga kwa wachezaji?
Kwa morisson ilikuwaje? Nyimbo si zilikuwa kama hizihizi kwamba afuate utaratibu kumbe wao ndo wako kinyume na utaratibu.
Yanga ina wanasheria vilaza Sana tusidanganyane.
Hii kesi mapema tu kabla jogoo hajameza punje ya matama Fei anawapiga kichwa utopolo

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Umeandika kishabiki mno....na kama unaongelea mashuti muulize aishi habari ya ki aziz
 
Wapo sawa hata kama hasipocheza still timu inayomtaka itafuata taratibu za soka na Yanga anaweza tengeneza hela nzuri kama ilivyokuwa kwa Vipers na Manzoki,kwa kumuuza kwa timu itakayo fuata taratibu.

Na si hii ya kujiamulia kununua mkataba kabla hujafuata taratibu za usajili.
 
Mnajitahidi kupotosha hoja zilizopo mezani kuhusu yanga na feisal, Yanga aiwezi kumzuia feisal kwenda anakokutaka isipokuwa Feisal na wanaomrubuni ndio wanaofanya mambo yawe magumu, Feisal alisaini mkataba mpaka 2024 kwaiyo mnataka yanga imwachie tu feisal kihuni huni ? Wanaomtaka kwa nini wasiende mezani kuongea biashara wauziwe feisal bali wanataka wampate kwa njia haramu! Akuna timu ya kiboya inayoweza kumuachia mchezaji kirahisi rahisi namna iyo kama mnavyofikiria nyie, Rejea kesi ya onyango na simba alipotaka kuvunja mkataba wake akidai apewi nafasi ya kucheza kamati iliamua abaki simba kwakuwa bado ana mkataba halali awezi kuuvunja kwa stahili ile, Sasa feisal awaambie wanaomtaka waende wakatajiwe dau lake walipe aondoke kiroho safi na sio kienyeji kama anavyofikiria kila jambo lina utaratibu
Tatizo lenu mnaangalia kipengele kimoja tu ndo mnatuletea hapa, kwenye huo mkataba wake kuna kipengele kimoja tu basi? Unajua mpaka mchezaji mwenye mkataba aamue kuuvunja anatakiwa kuwe kumetokea nini kwenye mkataba wake na waajiri wake? Kwanza vipengele vya mkataba viwe vimekiukwa ikiwa ni kutolipwa mshahara wake miezi 3 mfululizo, pili kukosa nafasi ya kucheza, tatu kutotimiziwa makubaliano yaliyopo ndani ya mkataba husika, Sasa katika ivyo akuna ata kimoja ambacho ajatekelezewa anavunjaje mkataba kihuni namna iyo? Kama ingekuwa ivyo basi vilabu vyote visingekuwa na wachezaji ina maana mchezaji yoyote angekuwa na uwezo wa kuvunja mkataba muda wowote na kusepa anakoona kunafaa
 
Tunashusha vifaa vingine huko!
 

Attachments

  • Screenshot_20230106_225035_Instagram.jpg
    173.7 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…