Mnajitahidi kupotosha hoja zilizopo mezani kuhusu yanga na feisal, Yanga aiwezi kumzuia feisal kwenda anakokutaka isipokuwa Feisal na wanaomrubuni ndio wanaofanya mambo yawe magumu, Feisal alisaini mkataba mpaka 2024 kwaiyo mnataka yanga imwachie tu feisal kihuni huni ? Wanaomtaka kwa nini wasiende mezani kuongea biashara wauziwe feisal bali wanataka wampate kwa njia haramu! Akuna timu ya kiboya inayoweza kumuachia mchezaji kirahisi rahisi namna iyo kama mnavyofikiria nyie, Rejea kesi ya onyango na simba alipotaka kuvunja mkataba wake akidai apewi nafasi ya kucheza kamati iliamua abaki simba kwakuwa bado ana mkataba halali awezi kuuvunja kwa stahili ile, Sasa feisal awaambie wanaomtaka waende wakatajiwe dau lake walipe aondoke kiroho safi na sio kienyeji kama anavyofikiria kila jambo lina utaratibu
Tatizo lenu mnaangalia kipengele kimoja tu ndo mnatuletea hapa, kwenye huo mkataba wake kuna kipengele kimoja tu basi? Unajua mpaka mchezaji mwenye mkataba aamue kuuvunja anatakiwa kuwe kumetokea nini kwenye mkataba wake na waajiri wake? Kwanza vipengele vya mkataba viwe vimekiukwa ikiwa ni kutolipwa mshahara wake miezi 3 mfululizo, pili kukosa nafasi ya kucheza, tatu kutotimiziwa makubaliano yaliyopo ndani ya mkataba husika, Sasa katika ivyo akuna ata kimoja ambacho ajatekelezewa anavunjaje mkataba kihuni namna iyo? Kama ingekuwa ivyo basi vilabu vyote visingekuwa na wachezaji ina maana mchezaji yoyote angekuwa na uwezo wa kuvunja mkataba muda wowote na kusepa anakoona kunafaa