Viongozi wangu wa CCM inatosha sasa, TEC hawatatuelewa hadi tueleweke!

Viongozi kuwa na madhehebu Yao ni sawa ila msimamo wa madhehebu Yao haupaswi kuwa msimamo wa Nchi.

Ukiwa na madaraka kwenye Nchi hipaswi kuleta mambo ya madhehebu yenu.

Upuuzi wa hivi ukome maana unaweza kuja kuleta shida baadae
Kesho Karatu, mara njombe mara Kigoma.....mtamaliza majimbo yoote ya Katoliki?

Pambaneni na ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Hizo bla bla kila mtu anazijua.
 
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
Sema yote lakini usipingane na ukweli aliouandika VUTA-NKUVUTE. Inaweza isiwe kwa uwazi unaoutaka wewe, lakini uhalisia ndo upo hivyo. Hivi unajuwa matamko mangapi yametoka kuhusu suala la bandari na DPW? Tamko la TEC ndo limeonekana kushika hatamu..!! Yaani kila mtu aliibuka toka alikokuwa..!! Hiyo pekee inatosha kukuambia kuwa TEC wapo very powerful.
 
Mkizingua mkumbukeee Biden ni mkatoliki tutampigia simu soon akiwasheeeeeeee soon, putin mkatoliki atakiwashaa soon
Be care..ccm
 
Kujipendekeza hakusaidii Ccm kurudi madarakani.....tayari mna tume isiyo huru na organs zote za kusaidia 2025 mshinde.

Hizo sarakasi mnapoteza muda na fedha tu
Ndio maana nimeungana na mtoa mada na Mimi hii tabia inanikera,kwani lazima watu wafabane maoni? Kwamba Waumini wa RC ni wapuuzi kiasi kwamba Kila wanachoambiwa na TEC lazima.wafuate?

Acha TEC wawe na msimamo wao na Serikali iwe na msimamo wao,kujipendekeza kwao ni wanatukosea sana ,itakuja kuleta shida baadae
 
Hakuna hatamu iliyoshika,aliyepambana vyema na DP World ni Mwambukusi tuu
 
Hahahaaa
 
Issue ya bandari wananchi woote waliipinga ispokuwa nyie viongozi wachache wa ccm n serikali mnainufaika nayo

Ndio maana tamko la Tec liliungwa mkono na makundi yoote.
 
Hii mada inazidi uwezo wako, subiri uchangie zile zenu machawa
 
Hata sisi waumini maaskofu wetu wasijaribu kutuburuza tufuate misimamo ya kisiasa wanataka nini, watuache tuwe hurua kufanya maamuzi yetu ya kisiasa kwa utashi wetu. Hata sisi tuna Mungu anayetusikiliza haja zetu. Wao walainike tu huko na chama tawala ila sisi tunajua tunachokitaka wasituletee kampeni zao
 
Isimamie na Wala hakuna mtu amekataza wao kusimamia na nakereka na kujipendekeza Kwa viongozi wa Serikali.

Serikali nayo inatakiwa kusimamia na inachokiamini,hii Nchi haiongizwi na TEC
Kiongozi,
Nchi hii haiongozwi na Rais peke yake ,ndio maana unaona utulivu. Hao TEC unaodhani hawaiongozi nchi Leo hii wakijitokeza wakasema hatuna imani na Serikali iliyoko madarakani unadhani Rais atakalia kiti Kwa utulivu??
 
Kiongozi,
Nchi hii haiongozwi na Rais peke yake ,ndio maana unaona utulivu. Hao TEC unaodhani hawaiongozi nchi Leo hii wakijitokeza wakasema hatuna imani na Serikali iliyoko madarakani unadhani Rais atakalia kiti Kwa utulivu??
Kwanza mikaa yote viongozi Wakiwa Waislamu hao TEC Huwa wanaosumbua hivyo hivyo ila akiwa mtu wa dhehebu lao pamoja na madudu wanakausha.

Kwani saiiz Wana Imani nae? Wao wasiookuwa na Imani wengine watakuwa na Imani ,TEC haiongozi Nchi bwana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…