Viongozi wetu wa Afrika wanakaa kimya juu ya vita ya Urusi na Ukraine kwasababu wanaogopa watanyimwa misaada

Wapi wamesema wanataka kutawala dunia yote? Mpaka sasa wametawala nchi ngapi na ngapi zimesalia? Ku share ideals haina maana unakuwa puppet.
Unajua kitu kinaitwa 'New world order' maana yake ni nini?
 
Tusibishane mkuu katika hili! Nisamehe kama nitakuwa nimekukwaza, ila Urusi mpaka sasa ivi tunavyoochatika JF ina msaada mkubwa sana kwa TZ ni hivyo si mambo yote hua yanawekwa hadharani but ni rafiki mzuri tu.
Kuuliza swali sio kubisha. Swali linahitaji jibu
 
Ugomvi wa watu wengine hauwezi kusababisha nawewe umchukie mojawapo.......na hao hao unataka kuwatetea na wajinga wengi tu huku Africa Kila siku wanatwiti na kuleta hashtags kibao,eti pray for yukreiniani.....jinga kabisa.... inamaana wale ndiyo binadamu Bora pekee? Africa kuna vita Kila kona,wachochezi ndiyo haohao
 
Kama ulifuatilia, mkutano wa UN kuhusu vita hii utatambua nchi za Afrika nyingi msimamo wao ulikuwaje. Wacha kudhalilisha viongozi wa Afrika.
 
Reactions: Tui
Wapi wamesema wanataka kutawala dunia yote? Mpaka sasa wametawala nchi ngapi na ngapi zimesalia? Ku share ideals haina maana unakuwa puppet.
Inaonesha hujui political economy ya ulimwengu. Si rahisi mtu kukuelewesha kwenye jf
 
Kama ulifuatilia, mkutano wa UN kuhusu vita hii utatambua nchi za Afrika nyingi msimamo wao ulikuwaje. Wacha kudhalilisha viongozi wa Afrika.
Wewe utakua ni kiongozi, ile video inakuhusu. Kaisikilize taratibu utaelewa uzi umelinga nini. Hapa hatuoneani huruma tunaambiana ukweli.
 
Pole sana ndg Urusi kwetu amekuwa msaada mkubwa sana na si kwetu tu hata kwa baadhi ya nchi za Afrika katika harakati za ukombozi kusini mwa afrika
Tuambie hiyo misaada hayo ya ukombozi tuyaache
 
Hivi unajua kwamba ukraine ilishakuwa na kinu cha nuclear na ilikuwa na silaha za nuclear??
 
Tusibishane mkuu katika hili! Nisamehe kama nitakuwa nimekukwaza, ila Urusi mpaka sasa ivi tunavyoochatika JF ina msaada mkubwa sana kwa TZ ni hivyo si mambo yote hua yanawekwa hadharani but ni rafiki mzuri tu.
Upi huo? China walijenga Reli, Scandinavian countries wametupa misaada mingi sana kwenye Elimu, VETA, Maliasili, Afya etc, Marekani nao halikadhalika wanetusaidia sana mfano MCC funds kwenye umeme, miundombinu etc... Sasa huyo Mrusi hebu tusaidie
 
Viongozi wetu wa Afrika wanakaa kimya juu ya vita ya Urusi na Ukraine kwasababu wanaogopa watanyimwa misaada.
Hata wakiongea maneno matupu hayavunji mfupa
Hata wakiamua kuisaidia nchi moja kati ya hizo teknolojia yetu ni very old, fikiria mpaka leo tunatumia "singe choma" kupambana na adui
 
Tusaidie link mkuu tuishushe toka ilipo
 
Sasa uliona wapi mwenye njaa akamkemea mwenye chakula..miafrika mingi imejaa unafiki tu..hapo inasubiri vita iishe ipereke bakuli.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…