Ndugu Commanche kwanza kabisa ujue kuwa mie sina maslahi na wahutu sana sana naweza kusema mie sijawahi kufahamiana na mhutu hata mmoja ile ktk maisha yangu nina marafiki zangu wawili ambao ni watutsi. Lakini hilo halinifanyi mie sasa nisiongee ninachoamini. Na pia sijisikii vibaya kuambiwa natumiwa na FDLR kwasababu mbili kwanza hiyo ndio propaganda ya Kagame dhidi ya Kikwete na by implication Rwanda dhidi ya Tanzania na binafsi ni mtanzania. Pili mie siwachukulii FDLR kama watu wabaya kama ambavyo serikali ya Rwanda inawabrand. Kwahiyo uko huru kusema natumiwa na FDLR.
Halafu ni kweli mie naongea kwa hisia tu lakini hisia zangu zinatokana na kulinganisha hoja za FDLR na zile za Serikali ya Rwanda; Serikali ya Rwanda inasema wale jamaa hawakubaliki kwasababu wana itikadi ya kuwauwa watusi yaani wao mpaka leo wanajipanga kuhakikisha wanawamaliza watutsi (kitu ambacho ni kibaya). Upande wa pili wao FDLR wanasema hawana itikadi ya aina hiyo wao wanataka haki na usawa Rwanda na wapo tayari kurudi Rwanda kama chama cha siasa waachane na mapigano. Tunakuja kwenye uhalisia hawa watu kimahesabu sio watu walioshiriki mauaji maana umri wao waliowengi ni labda kuanzia miaka 16 mpaka 35 (makisio) hawa haiwezekani ndio waliokuwa wanawauwa watu mwaka 1994, lakini hata kama wamo baadhi FDLR wapo tayari mtu aliyeshiriki mauaji awajibike binafsi kwa utaratibu uliopo. Kitu kingine wale waliouwa watu walijiita interahamwe sasa wahutu kuanzisha FDLR na interahamwe kuwa wahutu haitoshi kuwafanya FDLR ni interahamwe kwasababu wakati wa mauwaji kulikuwa na jeshi la serikali lilikuwa linapambana na waasi RPF na kulikuwa na interahamwe vikundi vya mauwaji vya wahutu, baada ya waasi kushinda jeshi la serikali na interahamwe wakakimbilia DRC. Sasa baada ya kuona wameondolewa madarakani jeshi la serikali wakaamua kuunda Chama cha ukombozi (FDLR) kama ilivyokuwa RPF ili wajipange kurudi madarakani halafu interahamwe kwasababu walikuwa hawana sera yoyote wakaanza kujiunga na FDLR sasa RPF kwa kujua mchezo waliokuwa wanacheza wao wanaona kitu pekee kitakachohalalisha wao kuhumiliate FDLR na hata nchi ya DRC ni kuibrand FDLR kama interahamwe.
Hivi karibuni propaganda imeanza kukosa nguvu maana kagame kasema watu kama Rudasingwa, Karegeya na Nyamwasa nao wanashirikiana na FDLR sasa hebu jiulizeni inawezekanaje hao watu washirikiane na kikundi chenye itikadi ya kuwauwa hata wao wenyewe? Halafu FDLR si ingekataa au kuwavizia na kuwauwa?
Kuhusu RPF kuwa mkombozi; hiyo ni propaganda inayoweza kuwaingia watu wasiofuatilia RPF imetoka wapi. Vyama vya ukombozi huanzishwa baada ya tatizo kuwapo. Muda RPF ilipoanzishwa kulikuwa hakuna mauaji ya halaiki sasa RPF ilikuwa inapigana kumkomboa nani? Watutsi?.
Mwisho wanyarwanda wanatakiwa wajue kuwa duniani kote hakuna mahali demokrasia ikichukua mkondo wake mtu aliyetoka kwenye minority group akapindua utawala wa majority group halafu ashinde uchaguzi. Na Rwanda haijafikia mahali pa kuwa na jeshi lililo na watutsi wengi kwahiyo kuna viashiria vingi tu kuwa Rwanda bado hali haijatengamaa. Wewe fikiria uvumi tu kuwa kagame kafariki watu wanashangilia.
mkuu umechambua vizuri sana, nakukaribisha kwenye chama chetu cha "wahutu", Hahaha, kwa kuwa mimi mwenyewe tayari nilishapachikwa kila kitu kuanzia uhutu, FDLR, interahamwe, genocidaire...etc. Hawa watutsi wa humu JF (sio wote, bali extremists ones) huwa hawana hoja zozote za msingi, huko Rwanda (kama umefika), mkiwa mnajadili kitu ,ukiitwa tu mhutu tayari unatakiwa kukaa kimya, ukiendelea na mjadala utajikuta uko ndani kwa makosa ya "divisionism", "revisionism", "genocide denying" na mengineo mengi. Ndio maana hawa jamaa wao wanaona uhutu ni tusi kubwa sana,
Kuna mambo mengi ambayo hawawezi kujibu mfano:
1. Hao interahamwe wenyewe walikuwa wanaongozwa na mtutsi aitwaye Robert kajuga ambaye alikuwa anatumia kitambulisho cha kihutu, akijifanya ni mhutu. Huyu mtutsi ndio aliyeongoza chinja chinja ya watutsi wenzie na kumpa kisingizio kagame aingie na kujifanya kaja "kustopisha genocide". Interahamwe originally ilikuwa kama green guard au red brigade ya chama tawala kwa wakati huo. Bila "genocide" kagame angeshiriki uchaguzi huru na asingepata chochote, haiwezekani kwa muasi, tena muasi aliyetokea uganda ambaye hata kinyarwanda hajui, aliyeshambulia nchi kwa miaka minne akiua watu ashinde kwa kura nyingi.
Cha ajabu huyu robert kajuga alimficha kaka yake kwenye ile hoteli maarufu kama "hotel Rwanda" ili alindwe na mhutu Paul rusesabagina. Mhutu huyu sasa hivi naye ni adui wa Rwanda/kagame, kama walivyo wahutu wote influential. Kagame anamtuhumu kushirikiana na FDLR, sasa sijui inaingiaje akilini kuwa kama jamaa ana chuki na wahutu kwa nini asingewaita hao interahamwe wawauwe pale hotelini 1994, aje kushirikiana na interahamwe leo wakati watutsi wanaendesha nchi...vitu vya ajabu kweli.
2. Muanzilishi wa hiyo FDLR alihongwa fedha na vyeo na serikali ya kagame, leo hii Gen Paul Rwakarabije ni MKUU WA MAGEREZA Rwanda. Huyu
Commanche nikimuuliza inawezekanaje kwa muanzilishi wa boko haram kupewa cheo serikali ya Nigeria hawezi kujibu. Ukweli ni kuwa FDLR ni chama tishio kwa kagame, hata members wa kawaida tayari wameanzishiwa program ya kupewa mashamba na fedha za kuanzia maisha anytime watakapoamua kurudi Rwanda. Sasa kama ndio hivyo kwa nini FDLR wakitaka mazungumzo wanaitwa genocidaires, wakikubali matakwa ya kagame wanapewa mpaka post za serikali? Hao kweli ni wauaji au chama cha siasa tishio?
3. RPF haijawahi kuwa chama cha ukombozi, ndio maana unakuta kuna watu kama Laurent Nkunda ambaye ni mtutsi raia wa DRC naye alikuwa mpiganaji wa RPF, Sultani makenga wa M23 naye alikuwa mpiganaji wa RPF. Kama swala lilikuwa ni ukombozi mbona RPF haikusaidiwa na nchi zingine kama vile Tanzania iliposaidia ukombozi wa nchi za SADC? Ni watutsi tu walijikusanya kuja kuteka Rwanda, baada ya hapo kagame naye kaenda kusaidia watutsi wenzie wateke DRC kwa mgongo wa M23 na waasi wengine.
Hawa kina
Commanche wasichojua ni kuwa wanatengeneza chuki dhidi ya watutsi hata hapa bongo kutokana na misimamo yao ya ajabu. Hata DRC ilikuwa hivi hivi mpaka watutsi wa kawaida wakaacha kujiita watutsi wakaanza kujiita Banyamulenge.