Mtanzania akiambiwa ukweli huwa anaishia kumtukana mleta ujumbe badala ya kuupima ujumbe kama unafaida maishani mwake. Umasikini wetu kwa kiasi kikubwa sana unasababishwa na sisi wenyewe. Ukitaka kuipima akili yetu jinsi ilivyo mbovu, tazama timu moja ya kigeni inapokuja kucheza na Yanga, jinsi ambavyo mashabiki wa simba watakavyofanya kila liwezekanalo kuihujumu Yanga. Na wakati mwingine Simba inapojiandaa kucheza na timu ya nje, wale watu wa Yanga wanafanya kila liwezekanalo ili mradi tu Simba ifungwe.
Uchukue mfano huo huo kwani unafaa kutumika hata kwenye masuala ya siasa. Mtu anaihujumu nchi yake pekee aliyopewa na Mungu. Zipo habari za chini ya kapeti kuwa hata mgao wa umeme ni hujuma ya baadhi ya watanzania. Mtu anauhujumu uchumi wa nchi yake mwenyewe, anayahujumu maisha ya ndugu zake wa damu!!. Paul Kagame aliposema apewe bandari yetu na fedha itakayopatikana itailisha Tanzania na Rwanda, alikuwa sahihi kabisa. Aliuona uzembe wetu, aliuona ukosefu wetu wa uzalendo.
Lakini mtanzania ukimwambia ukweli anaishia kukuita mtutsi, badala ya kupima uzito wa hoja anaishia kumshambulia mtoa hoja. Tanzania ikiwa kama mgonjwa ni lazima ipewe dozi sahihi ya dawa ili iweze kupona.