Vipindi vya dini katika shule za msingi na Sekondari za Serikali vifutwe

Vipindi vya dini katika shule za msingi na Sekondari za Serikali vifutwe

Muda wa kuendeleza vipaji vya mtu ni wakati akiwa bado mtoto, huo muda ukishapita sio rahisi tena kuviendeleza. Taifa letu linazalisha watu wengi wasio na ujuzi/ufundi/ubunifu wowote wa ziada zaidi ya masomo waliyokariri darasani.

Badala ya kuwajazia watoto mambo ya dini shuleni ungewekwa mpango wa kuwapa ujuzi wa nje ya masomo.
Yoda toka uache skul ambapo vipindi vya dini vilikuwepo umekuwa huru na muda mwingi tuu umegundua nn cha maana ambacho wasoma bible na quruan hawajakigundua??
 

Wale waliofanikiwa kupata elimu ya darasani angalau ya darasa la saba na kuendelea watakumbuka vipindi vya dini ambavyo vilitengwa rasmi kulingana na madhehebu mbalimbali na wanafunzi wote ni lazima kuhudhuria katika vipindi hivyo.

Mara nyingi vipindi hivi huwa Ijumaa kuanzia muda wa saa nne ili kuwapa fursa waislamu kwenda msikitini kwa sababu mara nyingi wao huwa hawatumii madarasa kuswali katika vipindi vya dini kama wenzao Wakristo.

Wakati mjadala wa tija elimu yetu ukiwa mkali bungeni na mtaani ipo haja ya kuliangazia pia jambo hili na kuona kama kuna tija yeyote kuwa na hivi vipindi.

Ukiangalia kwa makini utagundua vipindi hivi vya dini havina tija yoyote kwa wanafunzi zaidi ya kuwachukulia muda wao ambao ungweza kutumika katika mambo mengine muhimu kama sanaa za uchoraji, uchongaji, kuimba, kuogelea, ushonaji n.k

Ni wakati sasa mamlaka zinazohusika na elimu zitoe muongozo wa vipindi hivi kufutwa na kuongeza mambo mengine secular au kupunguza muda wa wanafunzi kukaa darasani.
Katika maisha kila jambo lina muda wake na maana yake hata likiwa dogo kiasi gani so relax
 
Mashahidi wa YEHOVA hawashiriki vipindi vya dini shuleni,wamepata hasara gani? Lakini wao ndio wanaongoza kwa heshima kwa kila mtu.

Serikali haina dini basi swala la dini ziachiwe taasisi za dini. Kwani mashahidi watoto wao heshima na biblia wanajifunzia wapi?
 
Kila mtu na mtazamo wake ila kwa upande wangu hivi vipindi vya dini kuanzia O level,A level na mpaka chuo vimenisaidia sana,kwanza vilinijenga kiimani zaidi nikazidi kumwomba Mungu na nguvu za giza zilizonifatilia mda sana mpaka kutaka kukatisha uhai wangu nilizishinda
Pia kupitia vipindi hivo nilisoma kwa bidiii na kuzingatia mda wangu(haya yote tuliyapata kwenye mafundisho ya mkamate sana elimu na God can not help in empty vacuum )
Kupitia vipindi hivo nilikuwa muoga wa dhambi hasa uzinzi sikutaka kumuudhi Mungu hyo ilinisaidia kufanya kazi moja ya kusoma na kumwomba Mungu kwa hyo mkuu sikubaliani na wazo lako
 
Mwanao akiwa shoga ndio utajua umuhimu wa hofu ya Mungu.

Kumbuka kumcha Bwana/Mungu ni chanzo cha maarifa.

Maarifa yote chanzo chake ni Mungu.
Wee nae una mawazo mfu na duni, kwahiyo dini ndo inazuia mtu kuwa shoga?
Mbona sasa kwenye hizo shule zilizoshika dini, na zenye kulenga San dini hasa za bweni, ndo mashoga na wasagaji wapo wengi?

Unapotoa hoja, kuwa makini ktk uwasilishwaji wake, sio una hemkwa tyuuh.
 
Kuna wengine wengi walikuwa na tabia mbovu sana, tena wakiwa viongozi wa dini shuleni.
Shule inaendeshwa kwa sheria na taratibu kama mwanafunzi hazifuati kuna adhabu zake zimeainishwa, sio kazi ya vipindi vya dini kudumisha amani, utulivu na utaratibu shuleni.
Naungana na wee, uko sahihi sana.
 
Watu badala ya kujibu hii mada kwa hoja wanaanza kuleta nonsense na personal attacks.

Alafu hawa wanaopiga promo hapa tabia zao na dini ni tofauti trust me asilimia 90 ya wote waliocomment kuhusu vipindi vya dini vimewasaidia na blahblah wapo kwenye ule uzi wa kula tunda kimasihara.
Na wao ndio walikuwa wakitongozana na kufanya ngono hukohuko shule baada ya kutoka kwenye hivyo vipindi vya dini.

Wewe unayesoma hapa na mfuasi wa dini nafsi yako yenyewe inakwambia ukweli.

Haya ndio mazao ya dini Unafiki na Uvivu wa kufikiri hata uwe na PhD.

hivi vipindi havina faida wala impact yoyote kwa wanafunzi tabia chafu, uhuni, ngono zembe, mimba za utotoni, uvutaji bangi na ujeuri uko palepale.
Hakika umenena na ndio ukweli wenyewe, ubarikiwe sana.
 
Mojawapo wa faida za vipindi vya dini katika shule za msingi na sekondari ni kuwajengea utamaduni wa kutambua na kuvumilia itikadi za dini/imani zingine. Ndiyo maana tunaweza kuwa na staha dhidi ya imani ya mwingine.
Ni kazi ya nyumba za dini, shule za dini, na kwingineko sio shule za serikali.
 
Shule zote nilizosoma ilikuwa ni lazima kuhudhuria vipindi vya dini, na viranja walikuwa wanawawinda wanafunzi waliokuwa hawaendi kwenye hivyo vipindi. Pia walimu walikuwa wanacharaza sana bakora wakikuta nje ya kipindi wakati wenzako wakiwa wanaendelea na kipindi.

Kwa wanafunzi wasiotaka kwenda kwenye hivyo vipindi waachwe wajisomee au wakacheze uwanjani.
Sio wakati huo tyuh, hadi sasa hivi ni lazima wanafunzi wote kuhudhuria vipindi vya dini, hili jambo sio sahihi kabisa.
 
Mashahidi wa YEHOVA hawashiriki vipindi vya dini shuleni,wamepata hasara gani? Lakini wao ndio wanaongoza kwa heshima kwa kila mtu.

Serikali haina dini basi swala la dini ziachiwe taasisi za dini. Kwani mashahidi watoto wao heshima na biblia wanajifunzia wapi?
Nakazia hapa.
 
Back
Top Bottom