Vipindi vya dini katika shule za msingi na Sekondari za Serikali vifutwe

Muda wa kuendeleza vipaji vya mtu ni wakati akiwa bado mtoto, huo muda ukishapita sio rahisi tena kuviendeleza. Taifa letu linazalisha watu wengi wasio na ujuzi/ufundi/ubunifu wowote wa ziada zaidi ya masomo waliyokariri darasani.

Badala ya kuwajazia watoto mambo ya dini shuleni ungewekwa mpango wa kuwapa ujuzi wa nje ya masomo.
Yoda toka uache skul ambapo vipindi vya dini vilikuwepo umekuwa huru na muda mwingi tuu umegundua nn cha maana ambacho wasoma bible na quruan hawajakigundua??
 
Katika maisha kila jambo lina muda wake na maana yake hata likiwa dogo kiasi gani so relax
 
Mashahidi wa YEHOVA hawashiriki vipindi vya dini shuleni,wamepata hasara gani? Lakini wao ndio wanaongoza kwa heshima kwa kila mtu.

Serikali haina dini basi swala la dini ziachiwe taasisi za dini. Kwani mashahidi watoto wao heshima na biblia wanajifunzia wapi?
 
Kila mtu na mtazamo wake ila kwa upande wangu hivi vipindi vya dini kuanzia O level,A level na mpaka chuo vimenisaidia sana,kwanza vilinijenga kiimani zaidi nikazidi kumwomba Mungu na nguvu za giza zilizonifatilia mda sana mpaka kutaka kukatisha uhai wangu nilizishinda
Pia kupitia vipindi hivo nilisoma kwa bidiii na kuzingatia mda wangu(haya yote tuliyapata kwenye mafundisho ya mkamate sana elimu na God can not help in empty vacuum )
Kupitia vipindi hivo nilikuwa muoga wa dhambi hasa uzinzi sikutaka kumuudhi Mungu hyo ilinisaidia kufanya kazi moja ya kusoma na kumwomba Mungu kwa hyo mkuu sikubaliani na wazo lako
 
Mwanao akiwa shoga ndio utajua umuhimu wa hofu ya Mungu.

Kumbuka kumcha Bwana/Mungu ni chanzo cha maarifa.

Maarifa yote chanzo chake ni Mungu.
Wee nae una mawazo mfu na duni, kwahiyo dini ndo inazuia mtu kuwa shoga?
Mbona sasa kwenye hizo shule zilizoshika dini, na zenye kulenga San dini hasa za bweni, ndo mashoga na wasagaji wapo wengi?

Unapotoa hoja, kuwa makini ktk uwasilishwaji wake, sio una hemkwa tyuuh.
 
Naungana na wee, uko sahihi sana.
 
Hakika umenena na ndio ukweli wenyewe, ubarikiwe sana.
 
Mojawapo wa faida za vipindi vya dini katika shule za msingi na sekondari ni kuwajengea utamaduni wa kutambua na kuvumilia itikadi za dini/imani zingine. Ndiyo maana tunaweza kuwa na staha dhidi ya imani ya mwingine.
Ni kazi ya nyumba za dini, shule za dini, na kwingineko sio shule za serikali.
 
Sio wakati huo tyuh, hadi sasa hivi ni lazima wanafunzi wote kuhudhuria vipindi vya dini, hili jambo sio sahihi kabisa.
 
Nakazia hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…