Vipindi vya dini katika shule za msingi na Sekondari za Serikali vifutwe

Kulazimishana au kulazimisha watu kuamini hiki au kile sio ustaarabu..., vilevile kuwanyima fursa watu kuamini / kujifunza wanachokiamini au kupata elimu ya imani hii au ile pia sio ustaarabu...

Cha maana tusilazimishane wala imani yako au yake isiwe kero kwa huyu au yule..., kila mtu kwa nafasi yake
 
Uko sahihi mkuu
 
Hii ni bullying. Inabidi bill of rights ifundishwe kuanzia darasa nne.
Hapa mie nakazia, hili la kulazimisha wanafunzi wote kwenda kwenye vipindi vya dini, sijawahi kuelewa kwa kweli.
 
Hata wapagani ni raia kamili na wana haki zote katika hii nchi. Kuna shule zinalazimisha kwa viboko wanafunzi wote waende kwenye vipindi vya dini. Hii sio sahihi.
Hapa naungana na wewe upo sahihi, Ila vipindi vya dini kufutwa sioni usahihi wa ilo.
 
Dini uleta ustaarabu kwenye Jamii
 
Ukwata imenilea nami nikaja kulea vijana kupitia Ukwata.

Binafsi nakiri kabisa vipindi vya dini shuleni vina msaada mkubwa sana.
 
Kama ishu ni muda bora kuviondoa vipindi vya michezo havina tija
Navyoona Mimi vipindi vya dini kwa wale wenye kutaka kujifunza dini wahudhurie na wale wasiohitaji wasilazimishwe kwa namna yoyote ile iwe kwa viboko au kwa adhabu ya aina yoyote ile sio sawa kumlazimisha mtu kuamini kitu asichotaka kuamini
 
Bora umuambie anadhan ushoga unahusiana na dini, khaaah.
Anachanganya mambo huyu vipi kuhusu mashekhe wanaolawiti watoto madrasa , mapadre,makadrinali wanaolawiti watoto, wachungaji wanaolawiti watoto hao wote wanadini na wanafanya Mambo ambayo yeye anaamini wasio na dini ndio hufanya

# HAUITAJI DINI ILIKUJUA KUWA KUUA MTU ASIYE NA HATIA SIO SAHIHI ILA UNAHITAJI UTU TU ILIKUJUA KUFANYA HIVYO SIO SAHIHI MWISHO.
 
Yoda, Yoda Yoda hata kama umeshuhudia matengano mbalimbali etc, kaa tu ukijua kuwa moja kati ya kitu kinachoweza kuliunganisha na kulinyanyua taifa ni dini! yes Dini ya kweli inajenga sana tu

Tena mi ningeshauri uboreshaji huu;mkwamba badala ya kila watu kujitenga na kakikundi kao ka kidini, wanafunzi wote wangekuwa wanabaki madarasani mwao na kunakuwa na zamu ya kila kikundi kuwafundisha wenzao mazuri/uzuri wa dini yao. Kunakuwa na sheria[tayari ipo] ya kutokashifiana tu. Hapa tunajenga uvumilivu/tolerance na harmonization baina ya dini mbalimbali
 
Yaan wa TZ ukitaka kuwaweza waweke kwenye Dini, hata mwenye PhD anakua mbulula tyuuh, wanakera mnooo.
 
Yaani wewe hamjajua vile ambavyo nipo na uwanda mpana utashangaa;

Yaani katika hivyo vipindi hata atheist nao wanaweza kupewa kuusema uzuri mazuri ya watu kuishi bila dini kama watakuwa nayo. Sikupendekeza watu fulani wakatazwe. La. Pendekezo langu lilikuwa tu ni sheria iwe kali kuzuia kukashifu dini nyingine. Technically atheist watabaki na mambo machache sana maana mara nyingi wao ni hamna/utupu wanasubiri hoja za wengine ndio wazipinge so wanaweza kuamua kutofundisha ila kuwa wasikilizaji
 
Atheist mnao mchango mkubwa tu tena mda mwingine mnafanya kazi ya MUngu bila kujijua. Unajua kazi ya kuzipinpointi errors/makosa katika ufikiri na mantiki zinazotawala kidini huwa ni kazi ya manabii!!

Hiyo ni kwa sababu watu waliozama katika kitu ni vigumu kuyajua makosa yao. You, it is harder to see the frame when you are in the picture.

Tuendelee na kazi watu wote wa Mungu😂😂
 
Shule zinapaswa kuwa sehemu za watoto kujifunza hesabu, sayansi, sanaa, historia na michezo. Dini wakajifunze makanisani, misikitini, mahekaluni na nyumbani kwao.
 
Shule zinapaswa kuwa sehemu za watoto kujifunza hesabu, sayansi, sanaa, historia na michezo. Dini wakajifunze makanisani, misikitini, mahekaluni na nyumbani kwao.
Kuna kitu hujakitafakari kwa upana hapo. Kukiwa na sehemu moja ya kufundishana dini hiyo ni hatua nzuri kwenye kuelewana. Tena mimi sipendekezi dini ziungane. La. Ila kuwe na uelewano na check and balance.

Tunakubaliana katika hoja za kisayansi, kihistoria na kihesabu kwa sababu tunajifunza sehemu moja.
Fikiria tu mfano hawa watu wakijifunza historia nyingine wanaanza kuja oof waafrika waliwachukua waligundua hiki, sijui nani alikuwa mweusi kunakuwa hakuna mshikamano tena

Na sisi tunataka mshikamano wa kitaifa hapa. Mi ningekuelewa kama ungesema labda badala ya dini wafundishwe falsafa fulani itakayokuwa imeunganisha mazuri ya dini zote tulizonazo - This sasa will be the game changer
 
Mmh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…