Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)


Hahahaha umenikumbusha mbali sana, mimi nilikuwa najifanya mjanja na tuviwanja twa Dar, Kenyatta na Entebe ndiyo ilikuwa uwanja wangu sasa siku moja nikawa naelekea Cape Town kwenye training.

Nakuambia usicheze na OR Tambo yaani kuna gate A1 mpaka sijui Z10 si nikajifanya mjanja eti sitaki kuulizia yaani kidogo nikose ndege ya kukonect Cape Town baada ya hapo somo ni moja hata niwe wapi mimi kama kitu sikijui na ni mshamba lazima niiulize ama nifanye research zangu kabla ya kuanza safari
 
Oh nawaoneaje wivu nyie...mimi mara ya kwanza ninapanda ndege nilikuwa shule ya msingi ndicho nnachokumbuka ila darasa sikumbuki...tulikuwa tunaenda daslam na baba.

Pale eapoti ya KIA kulikuwa na mlinzi na baba alitaka kwenda kujisaidia...akamuomba anichunge yeye aende. Kumbe yule mlinzi alikuwa na chupa ya kilevi ( baada ya kukuwa mkubwa ndo nimeweza kukonekti ile chupa ilifanana sana na chupa za GRANTs) akanipa nionje na mm kwa uroho wangu nikabugia fundo kubwa. Sikuhisi chochote tukapanda ndege....niliamka niko hotelini tayari hata sikujua utamu wa ndege kwa mara ya kwanza.

Safari ya kurudi tukarudi na basi mara tushukie Chalinze kwa ba mdogo..mlandizi kwa shangazi...korogwe kwa ma mkubwa...nilikasirika sana.

Hadi leo nikiusikia wimbo wa 'aerosmith - I don't wanna miss a thing' unanikumbusha sana ile safari...I missed everything yet siwezi kubadili kuwa ilikuwa safari yangu ya kwanza ya ndege. #sad
 
Namshukuru Mungu nimezaliwa kwenye familia yenye uwezo sana. Bibi yangu ana ndege mbalimbali, kuku, bata, kanga, kwale, njiwa etc

Bwahahahahh. We Bujibuji be serious banaaaaa!
 

Fundi mchundo.

Ahsante kwa kufanikiwa kunichekesha.

Hahahahahah
 
Mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...

hahaha! Sipati picha.
 
Loo nimecheka sana kwa wote walioshiriki humu kwa kweli mi sioni kama ni ushamba jamani ingawa mimi mara yangu ya kwanza nilikuwa na father( God bless him ) tulikuwa tunatoka nje ya nchi kwa sababu yeye alikuwa na uzoefu wa safari na nilikuwa only 19 I was so excited, pia utukutu nataka kila kitu nijue mara mbele mara nyuma mpaka nikaomba nikamuone rubani anavyoendesha ndege ambapo nilikubaliwa, Lakini kwa sasa ambapo umri wangu ni mkubwa na nimepanda ndege nyingi sana haya yanayotokea huwa nayaona kila wakati na siwashangai kama mtu hajui kufunga mkanda au kufungua screen aangalie movie au wakati wa mlo.
 

hahaha watu mnavituko
 
kuna mtu alipiga magoti Amsterdam wakati wanaunga ndege waende switz. Haya ni maneno waliokuwa karibu walimsikia akisema.
"eh baba! ushukuriwe kwa kunifikisha huku juu mbinguni baba! duniani dhiki na shida nyng baba! Mweh ndaga mwalafyale mweh"

hahahaha!! Mbavu zangu miye!
 
mimi 2010 nilikuwa natoka NAIROBI-JKIA KWENDA KISUMU hakika nilidata wakati inaanza kupaa na hasa tulipokuwa tumefika usawa wa kukatiza mawingu, nilikuwa kama naona maruwe ruwe vile , pia wakati wa kubadili mruko mmoja kwenda mwingine wa juu zaidi ilikuwa kama inashitua flani vile basi furu kudata. hakika pipa lina raha na karaha zake hasa upandapo kwa mara ya kwanza.
 
mi siku ya kwanza kupanda ndege ilikuwa 2010 natoka dar naenda mwanza usiku kabla ya safari sikulala maana sijui ndo furaha au kimuhe muhe cha ndege. Chezeya pipa wewe.

Hahahahahahahaaaaa!
 

hahaha! Huu uzi!
 
kuna mtu alipiga magoti Amsterdam wakati wanaunga ndege waende switz. Haya ni maneno waliokuwa karibu walimsikia akisema.
"eh baba! ushukuriwe kwa kunifikisha huku juu mbinguni baba! duniani dhiki na shida nyng baba! Mweh ndaga mwalafyale mweh"
Duniani kuna vituko sio mchezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…