Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Mara ya kwanza kusafiri nilikuwa naenda Sehemu hivi kupitia Paris. Ila siku hiyo ndege ya Air France ikawa imeharibika na hivyo ikaja ndege ya Madagascar Airlines Boeng 747, mzinga wa pipa.

Uzuri ni kuwa nilipigwa shule nyumbani nzuri sana jinsi ya kufunga mkanda, kulaza kiti na kukirudisha, kufungua headphones na kuzitumia na wapi zipo tundu za kuchomeka.

Ila nakaa, pembeni kuna Dada wa Kiganda na Mudhungu wake, akawa anahangaika jinsi ya kufunga mkanda, bwana wake akamsaidia kufunga. Sijui siku hizi anajisikiaje akikumbuka ushamba huo wa siku ya kwanza.

Kasheshe ilikuwa wakati wa kula. Ila Mungu bariki nilishaambiwa kuwa kuna vikaratasi vya kufuta uso na asubuhi mnaletewa taulo za motomoto kufuta uso pia. Msosi kufika, maajabu matupu kwani nusu ya vyakula navifahamu na nusu sivifahamu. Mie na kundi langu lote tukawa tumekubaliana tutakula kila kitu na hatubakizi hata kama watakuwa CHURA wa Kifaransa maana hawa jamaa WALA VYURA hawakawii kumlisha mtu nyama zao.
Kila kitu kilienda safi ila ikawa kasheshe kuzila OLIVE ila nikajikaza nikazila. Kulikuwa na nyama nyeusi nyeusi, sikujali ni nini, nikazila bila huruma. Mwisho vikabaki vipaketi vitatu. Kimoja kukifungua ni Sukari, nikaibugia. Kingine kufungua ni jibini, nikaila bila huruma. Cha mwisho kufungua (nilikuwa nafahamu unafungua kwa kuvunja ncha iliyochomoza) ikawa kumbe maziwa ya kwenye kahawa ambayo nilishaimaliza mapema sana bila sukari wala maziwa. Basi nikaangalia kushoto kulia hakuna anayeangalia, nikabugia. Mwisho nikasema hata kama Mjinga fulani kaniona, sijali maana hatakuja kuniona tena. Mwisho sahani yote ikawa tupu na wakaja akina dada kuchukua makasha matupu.

Kuna jamaa alikuwa anawasumbua akina dada kuagiza pombe basi ilipofika saa 9 usiku, wakamuita na kumuonyesha Friji la Pombe lilipo na wakaenda kulala. Jamaa alipofika Paris, alikuwa anatambaa kutoka ndani ya ndege.
salute kwako kaka nimecheka sanaa aiseee 😂😂😊
 
Nimecheka had kulia..dah
 
Hv Emirates ishawahi kupiga nyama Chini?
Mkuu acha nuksi EK ndio usafiri wangu ingawa nilikuwa siipendi, mpaka ATC itakapoanza kuruka nje ya nchi. December nilipiga katrip Dubai na Boeing 747-300-ER, hili dude ni kubwa kasheshe mkifika Dubai inabidi lizunguke kidogo kabla ya kutua maana kuna traffic,basi hapo mara limekata kushoto mara limekata kulia unaona dunia chini inapanda na kushuka na ule mji ulivyokuwa mzuri unaona mistari ya taa tu!
 
EK mzinga wa ndege huduma kama zote.
DUBAI /Dubei/ mkiingia usiku hadi raha. Enzi za Mkwere tunaenda Ijumaa tunarudi jumapili Bongo. Mihela ilikuwa ina-flow tu. Mademu unajiokotea bila kuongea saaana
 
Nahisi Emirates siku hizi wanakula hasara asee enzi zile mnakutana halmashauri kama zote ndani ya pipa yaan mnaweza kufanya kikao Humo Humo kwenye ndege. Yaan ilikuwa ni kuvuna tu midola ya posho safari za ughaibuni
 
Ha ha ha mnafanya vikao vya quarter na kufunga kikao... Umenichekesha sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom