Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Mkuu hii Lazima itakua intercontinental unapasua mabara mengine ya Afrika kama si Australia huko basi itakua mbali sana
 
Mkuu hii Lazima itakua intercontinental unapasua mabara mengine ya Afrika kama si Australia huko basi itakua mbali sana
Bara to bara mkuu sema ni ile ya kubadilisha ndege ndio ufike uendako
 
Masaa13 safarini, si unakaa mpaka makalio yanawaka moto!

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli, ni raha sana, hasa kwa aliyezoea.

Lakini kama ni mgeni na akawa ni mwoga, anaweza akatamani apatwe ghafla na usingizi mzito akazindukie mwishoni mwa safari.

Nashukuru kwa picha. Imenihamasisha na mimi niwe ninakumbuka kuchukua picha hewani.
 
Mkuu kwanza kutoka Zanzibar to Dar ni dakika 15 tu, Pili ndege inapaa futi 5000 tu ukilingalisha na Futi 25,000 hadi futi 38,000 anga za kimataifa, sasa huko si utakufa??🤣🤣🤣
 
Sikuwahi kupata changamoto maana aunt yangu alinielekeza taratibu masharti yote kuanzia kg ngapi nibebe na pia hand luggage ya kuingia kwenye ndege vitu kama perfume lotion ujazo upi haruhusiwi na nikifika transit Nairobi na nikifika OR Tambo South Africa uwanja wao mkubwa nifate watu na vibao sehemu za kuchukua begi Taxi ziko wapi na nauli rand ngapi alinipa address basi akiniona mlangoni tu akashangaa sana.
 
Bora ulikuwa na mwalimu
 
Endelea kumshukuru Mungu na kumuomba Mungu. Kuna mambo, utamuona aunt yako muongo!
 
Mkuu kwanza kutoka Zanzibar to Dar ni dakika 15 tu, Pili ndege inapaa futi 5000 tu ukilingalisha na Futi 25,000 hadi futi 38,000 anga za kimataifa, sasa huko si utakufa??🤣🤣🤣
Kwa nini nife mkuu? Maadam hizi za ndani hazinipi hofu tena, naamini hata za masafa marefu hazitanisumbua. Ikimpendeza Mungu, nitakuwa na safari ya kulivuka bara la Afrika siku za usoni, na naamini nitakuwa comfortable sana. Shuhuda za wadau kwenye huu uzi zimenitoa matongo tongo kwa kiasi kikubwa. Sitakuwa na sababu ya kuogopa. "Nimechagua" kutokuogopa.

Pengine taarifa zangu kwa safari ya kwanza kwa ndege zinaweza zisiwe "accurate", hasa ikichangiwa na hofu iliyonighubika siku hiyo. Ila kwa mujibu wa diary yangu (huwa nina kawaida ya kuandika matukio ya kila siku), tulitumia kama dakika kumi na mbili angani. Kwa kutumia neno kama, kunaashiria kuwa inaweza ikawa siyo hizo dakika exactly, kunaweza kukawepo na kautofauti kidogo. Neno kama linaashiria makadirio.

Hata hivyo, kwa siku hiyo, hizo dakika chache niliziona ni nyingi mnoo! Ila siku hizi si tatizo tena.

Siku hiyo pia, air host alitutangazia kuwa umbali ambao ndege yetu ingeruka ni 6,000 hadi 9,000.

Sijarudi tena Zanzibar tokea kipindi hichoe, ila ikitokea nikaenda huko kwa usafiri huo, niyafanya uhakiki kwa sababu huenda pia nilichosikia siku hiyo sicho kilichosemwa. Unapokuwa na hofu, unaweza ukasikia kitu cha tofauti na kilichosemwa.
 
Bora ulikuwa na mwalimu
Kwa kweli nashukuru Mungu changa moto nilokutana nayo ni uhamiaji wa Tz kunisumbua kuniona punda nahojiwa sana kwanini nasafiri sana na kipato gani niliwaambia tu sio swali la kuuliza mwanamke😁changamoto nyingine nchi za watu nikionekana Mtanzania tu naambiwa kaa pembeni napelekwa room napekunyuliwa begi mwili wangu mpaka sehemu za Siri kwa kweli ilikuwa ni usumbufu na udhalilishaji mpaka nikachukia kusafiri nikatulizana Hadi mwanangu mdogo alishapekuliwa labda nimetia drugs kwenye diaper.
 
Aisee!!! Nahisi kukasirika lakini sijui nimkasirikie nani! Pole sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…