Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Daaah niko ofisini, yaani bosi wangu yuko pembeni ila haoni nafanya nini mezani kwangu, yaani nimesoma thread yote nilikuwa nachekea tumboni, ila kuna mda kule kujibana kisauti kikatoka ikabidi nijikaushe na kakikohozi nikijifanya ni kikohozi kimenishika, hahahahaaaaa mmenichekesha mnoo wachangiaji wa hii mada.

Mie bana mara ya kwanza kupanda pipa ilikuwa wakati niko mdogo hata darasa la kwanza sijanza, tulienda Moshi kulikuwa na msiba ilikuwa air Tanzania ilikuwa na giza mnoo na hakukuwa na A/C sina memory nayo sana ila sikuona tofauti yoyote na ussafiri mwingine labda kwakuwa nilikuwa mtoto.

Nilipata sarafi nyingine nje ya nchi na mzazi wangu alienda kikazi, ilikuwa tunaenda Italy kwanza tuliachwa na ndege mara ya kwanza, tulichukua taxi kumbe ahikuwa na mafuta kufika njiani ikazima wakati huo hadi kupata taxi nyingine na ilikuwa alfajiri saa kumi na moja hivyo kufika airport ndege ishaondoka saa nyingi na safari ikasogezewa hadi wiki iliyofuata ndo tukafanikiwa kuondoaka.
Kwenye ndege ilikuwa KLM tulihudumiwa vizuri sasa nikapewa walkman (viredio vidogo ambavyo unaplay casset unasikiliza mziki na headphones zake) Mie kupewa ile baada ya kupewa msosi nilianza kusikiliza hadi usiku watu wanalala mama ananiambia lala mie namwambia sina usingizi nikajifanya nunda bana nikakesha nasikiliza mziki. Ile kufika alfajiri ndo macabin crew wanapita kuwapa watu vitafunwa kabla ya kushuka looh mie lepe la usingizi na mama kufikiria kunibeba mie, na mizigo aliyonayo nilikula makwenzi hayo hadi usingizi ukaisha hheheheheheheee.

Tulipofika Italy nyumba tuliyofikia ilikuwa toilet wametenga sinki za haja ndogo na za haja kubwa. Mie na akili zangu za utoto pamoja na kuwa mama alishanipa melekezi jinsi ya kutumia nikabanwa na kubwa na ndogo sasa nikasema wacha nipige nikae kwenye sinki la ndogo kisha nikimaliza ndogo nahamia sinki la kubwa kisha naflash. Weeh ile nakaa namalizia haja ndogo si ikaunganisha na kubwa hapohapo, sasa ile sinki ya haja ndogo inakachujio kama ka chai ukiflash kubwa inabaki palepale weeeh jasho lilintoka na maza alikuwa makali balaa....

Usitake kujua nilisolve vipi hilo tatizo maana nilikaa huko toileta kwa masaa mawili looh sitakaa nisahau. Hizi safari za ukubwani zilianza wakati naenda dubei ilikuwa poa kwani nilikuwa na mwenyeji then hizi za kikazi za nchini na nairobi wala hazijanipa shida thanks kwa muanzisha mada looh!!!
U made my day.
 
Safari yangu ya kwanza ilikuw geita,dah...nilikuwa na mzukah!ila nilienjoy sana japo ushamba mzigo
 
Mkuu,
Kwa hivyo vitu umeandika hawawezi kukushusha hata siku moja. Ila kuna nchi ambazo hawataki kabisa ulete Nyama au vitu kama Senene, Samaki nk kwa kuogopa utaleta wadudu hatari kwao.

Wanakataza vitu vya Majimaji au tuseme liquid na hii ilianza baada ya jamaa kupanda na maji ambayo alipoingia ndani ya ndege, akataka kutengeneza bomu. Wanaruhusu si zaidi ya kichupa cha 100ml. ambapo unaweza kuwa umeweka dawa ya mswaki, shaving foam/gel, after shave, creams nk. Ila kama sikosei pia wanalimiti idadi ya chupa ila sikumbuki ni ngapi ila ukifika Airport zote wanaonyesha.

Mie pana wakati nilisafiri Dar Shinyanga na sikufahamu sehemu ya kukabidhi Sanduku. Basi nikaingia na wakataka kuninyan'ganya na nikawaambia nafahamu sheria ila hili sandugu nakabidhi, wakacheka na kuniambia niende chini kwani nilipoona wameandika Domestic nikadhani ni huko tunakabidhi masanduku. Nikashuka chini na kuwapa sanduku langu.

Hivyo kama una Perfume, sijui nn basi weka ndani ya sanduku na uwape. Ila ukishangia ndani, unaweza kununua tena MAJI au Perfume na ukatumia ndani ya ndege. Ila kama unataka kubadili ndege kwa mfano tuseme Kenya, basi usiufungue mfuko walioufunga na kuandika Duty Free kwani watakugomea tena kuubeba. Unaweza kununua kitu tuseme USA na ukafika Schiphol Airport na mzigo wako. Kama bado umefungwa hawakusumbui na wanakuwa wanajua umenunua nini kwa sababu kila unachonunua, wanachukua ticket yako na kureport kwenye shirika kuwa kuna Kilo kadhaa zimeongezeka. Hivyo unapobadili ndege, kama bado mfuko umefungwa, hawasumbui au kukunyang'anya.

Hivyo Mkuu, kama una mahindi, karanga, njugu..... wewe beba tu ule njiani. Ila tu cha muhimu, usizidishe kilo unazotakiwa kubeba mkononi na ukubwa wake pia usizidi ili zienee kwenye machanja ya ndani ya ndege.

Mean while, huko Mbeya................

IMG_5244.JPG

Kwahiyo mnataka kuniambia nikipanda na maindi yangu ya kuchemsha na tumuogo twangu twa kuchoma twa kulegezea njaa njiani watanshusha!!

Mwee!! Vibaya hivyooo!!
 
Mentor ameshawahi kupanda huyu, sema hataki tujue ushamba aliofanya!
...
Eti Munkari haujawai kukwea pipa?

miye nilipanda sasa nikashangaa mbona ndege yenyewe nipo peke yangu? Alafu haina mlango wala madirisha kuja kushtuka nipo ntwara bila nguo!! Ikabidi nishtuke watu wamenijalia!!
 
Last edited by a moderator:
mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...
hahahahahahaahh umenichekesha sana mdau
 
Sizinga,
Kisheria wanatakiwa wakusubiri/wakutafute kama wanajua hujatoka ndani ya Airport. Vinginevyo basi wanatakiwa washushe sanduku lako/mizigo yako na ndipo waondoke ili kuepusha yaliyotokea kwenye ndege ya Pan Am na wale magaidi wa Ghadaff. Pia ndege kuchelewa au kusubiri mtu ni kawaida sana ila inategemea wewe ni nani. Nilishakutana na Mzee mmoja tulikuwa tunamwita Small Great Man kwa sababu jamaa ni Mdogo wa umbo ila ni Mkubwa sana kwa matendo. Kuna siku ndege imemsubiri kama saa nzima hivi. Pia kuna dada alikwama London na wale wafanyakazi wa ndege pale Airport wakamjibu ovyo. Basi akapigiwa simu huyo jamaa na dakika kadhaa baadaye, wale akina dada walikuja wakiomba msamaha. Ndege ilisubiri, jamaa akapanda taratiibu.

Kuna mwingine alikodisha ndege na kufanya kila kitu kwa wafanyakazi wa shirika ila jamaa walitaka kumtapeli. Basi ndege ikiwa imeshasimama kwenye barabara wakisubiri wakanyage mafuta iruke, wakaamrisha warudi kwenye sehemu ya Ku-taxi na wasubiri. Ilibidi kwanza fedha zilipwe na ndiyo jamaa akaruhusu ndege iondoke.

Hizi ndege ukweli ni kuwa hazipishani kabisa na Basi au train. Kama mtu hufahamu, ndipo unapoogopa. Ndiyo maana watoto wa MUJINI hubebea POWDER zao na Bangi na kuziingia Uholanzi bila shida.
Kama unajua Ki-Dutch basi utasikia jamaa wakitamba kabisa kuwa wataingiza Cocaine kwenye ndege na mwenzao ataikuta humo ndani ila aseme tu anataka kilo ngapi: Documentaire over Crips in Den Haag - Crips, Strapped 'n strong - YouTube
mwaka 1999..haaikuwa mara yangu ya kwanza infact, nilienda kuiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la watoto(The World Parliament of Children-Paris), sasa ile program ilinifanya nichoke sana manake sikuwa na muda mzuri wa kupumzika mara zote tulikuwa tupo busy sana!! Sasa siku ya kurudi tumepanda Swiss Air mpaka Zurich- wakati tunasubiri connection aisee nilipiga usiingizi wa kufa mtu pale,hadi muda wa ndege umefika mi nimelala tu..wale wenzangu (wawili)wakawa wameshapanda ndege mi nakoroma pale kwenye kochi...sielewi ilikuwaje manake ndege yote bado mm tu kupanda na air hostess wameshaambiwa kwamba kuna mtu mmoja amemiss

Ikabidi ndege isiondoke wakatumwa askari wa airport kunitafuta mule ndani...nikaja kuamshwa nio na lepe la usingizi wakaniambia ndege inakusubiria...wakanipeleka hadi boarding ile naingia tu mlango ukafungwa na kila mdada ananishangaa ulikuwa wapi...!!
Kikubwa mpaka leo sijajua ile ndege kweli ikinisubiri mimi au muda wake wa kuruka ulikuwa bado haujafika.

Fundi Mchundo,

Inashauriwa kunywa hizo Nyanya kwani ukiwa angani, inasemekana kuna sijui kitu gani huwa kinapungua mwilini na hizo Nyanya ndiyo zimejaa hizo habari. Ndiyo maana siku zote, kwenye ndege wanakuwa na hizo Nyanya. Hata mie nilikuwa mpinzani sana ila tangu waliponiambia, basi nikaanza kuwa mtumiaji mzuri sana wa hizo nyanya.

Kama zinakupa shida, wewe weka chumvi kidogo na bugia tu, zitakusaidia sana.

Hahahah umenikumbusha mbali asee.

Ila juisi yao ya nyanya hawa jamaa sitokaa niinywe tena asilani.

Ni hayo tu kwa leo.
 
aisee nimecheka sana, mimi ilikuwa mwaka 2008 nilisafiri na mtoto na sikujua kama mtoto analipiwa nauli! jamani jamani nilipelekeshwa hadi mchakato wa kumlipia nilikuwa abiria wa mwisho kuingia kwenye ndege na wale wasaidizi wakiwa na mimi kila kona wengine wamenisaidia mtoto presha ipo juu yaani nimeingia kwenye ndege jasho hata handkerchief haitoshi!!!!!!!!!!
 
Haya tumewasikia wengi wenu mmepanda mkiwa wadogo hahhahhahgha
 
Nimecheka sana nilizani ni mimi tu kumbe tupo wengi. Daah thanx pple
 
Kwa kweli mimi hizi Local nimepanda sana,enzi hzo tunaishi Mwadui Mining,ile Mwadui ya Nyerere...iliyokuwa the second township in Southern Sahara,tuliokuwa tunasoma boarding ndege ilitubeba hadi Dar na wakati wa likizo iliturudisha nyumbani,nilipomaza Mwadui A Primary school nikapangiwa Ilboru then Tabora school Advance,sasa kila likizo ni ndege mpaka baaaasi....Ushamba ni siku napanda International Flights,nilipanda KLM,nikamimina juice ya nyanya nikijua ni Tomato sauce kwenye msosi,kwenda chooni kushusha gogo ngoma nikashindwa kuflash...ile kufika tu Amsterdam mageti karibu mia,nikapotea na kumiss connection...ikabdi nilale Airport siku mbili....kwa kweli upya ni ushamba

kaka mwadui mining?pia nimezaliwa huko aisee..i wish to know ur real name..maana pale tulikuwa tunajuana mji mzima...
 
kaka mwadui mining?pia nimezaliwa huko aisee..i wish to know ur real name..maana pale tulikuwa tunajuana mji mzima...

Mzee tutakuwa tunajuana tu,mana Mwadui tulijuana kwa mitaa na.namba za nyumba, ukisema nakaa Mabatini, Boidi ya Juu au ya Chini lazima useme na namba ya nyumba...mitaa ya Uhindini,Uzunguni,alamasi Road,Jamuhuri,Compaund,barabara mbili na Duka kubwa.

Tukianza story tutabadili mada mkuu,hapa ni ushamba wa ndege,i miss Mwadui..maziwa toka Daily Farm unaletewa kwa token hadi mlangoni,samaki sato zinafuatwa Mwanza kwa Ndege,mwalimu Toto,Chubwa,Nyabi,Masunga,miss Lewis...hebu tuache!!!Lini wewe ulianza pand ndege???
 
hahaha nimecheka sana Sikonge yaani umenifanya nicheke hadiiiiiiii

halafu joe. na wewe nimecheka sana ashukuriwe aloanzisha hii thread................
 
Last edited by a moderator:
Safari ya kurudi tukarudi na basi mara tushukie Chalinze kwa ba mdogo..mlandizi kwa shangazi...korogwe kwa ma mkubwa...nilikasirika sana.

Hadi leo nikiusikia wimbo wa 'aerosmith - I don't wanna miss a thing' unanikumbusha sana ile safari...I missed everything yet siwezi kubadili kuwa ilikuwa safari yangu ya kwanza ya ndege. #sad

hahaha Pole sana

ka una stress bora uingie kwenye hii thread kwa kweli
 
Back
Top Bottom